
Mchezaji Bora wa shirikisho la soka barani ulaya wa Mwaka 2018/19 kutangazwa leo.
1:Lionel Messi Fc Barcelona
2:Christiano Ronaldo Juventus
3:Virgil Van Dijk Liverpool
Unazania nani ataibuka kidedea leo?


Mchezaji Bora wa shirikisho la soka barani ulaya wa Mwaka 2018/19 kutangazwa leo.
1:Lionel Messi Fc Barcelona
2:Christiano Ronaldo Juventus
3:Virgil Van Dijk Liverpool
Unazania nani ataibuka kidedea leo?


✍🏽Msimu huu hakuna adui mkubwa wa mashetani wekundu kama MAJERUHI, ndio, majeruhi ndicho naona atakua adui mkubwa wa United
:
✍🏽Hii yote inatokana na kupungua kwa ukubwa wa kikosi hasa kwa kuuza watu ambao kwa namna moja ama nyingine umpa kocha Ole machaguo mbadala na yenye ubora. :
✍🏽Manchester imewauza Herrera, Sanchez, Lukaku, Fellaini na hawa wote wanakupa kitu tofauti, ila cha ajabu hawajafanya usajili wa kuziba mapengo :
✍🏽Man United inaonekana imebaki na wachezaji wanaompa faida mwalimu katika plan A, ila napata wasiwasi kuhusu plan B, sion benchi lenye ubora wa plan B madhubuti.
:
✍🏽Hivi sasa Shaw amepata majeraha na nafasi ya beki wa kushoto kwa sasa haina mbadala sahii ila ina mbadala wa kujazia yani wale ambao si nafasi yao ila tu wanaweza cheza, akiwemo Young na Rojo
:
✍🏽Vipi kuhusu Martial ambae pia ana majeruhi? Hapa ndipo alihitajika Lukaku, Ok tunaeza sema atakaa Rashford, ila je kwa Rashford nani atacheza? Hapa ndipo alihitajika Sanchez ila kwa sasa Lukaku na Sanchez wanakunywa mvinyo kunako jiji la Milan nchini Italia
:
✍🏽Oyaa washabiki wa Manchester United kama kuna sara ya kuomba kujiepusha na majeruhi basi sasa inabidi kusali kutwa mara tatu kujikinga na yule adui MAJERAHA.
:
✍🏽Ila JE WAJUA, Majeruhi ndiyo chanzo cha kumleta kinda Rashford kipindi kile cha Van Gal, je vipi sasa tutegemee kinda mwingine kuibuka!? Swala ni muda tu. Tuwe na subra
:
✍🏽Written by: Daniel Mtani Thomson
IG: @danirito_thomson wa @sokaplace_

– Alexis Sanchez ametua jijini Milan kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya na kujiunga na Klabu ya Inter Milan kwa mkopo akitokea Manchester United.
.
– Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Chile alikuwa akihusishwa vikali na kuhiama Klabu hiyo ya Old Trafford msimu wote huu wa joto, baada ya kufanya vibaya chini ya kocha wa zamani, Jose Mourinho na kicha wake wa sasa Ole Gunnar Solskjaer.
#TransferNewsUpdate
@Sokawaytz

✍🏻 Droo ya hatua ya Makundi ya Michuano ya UEFA Champions League itafanyika Siku ya leo tarehe 29 Agosti 2019, Muda Ni Saa 18:00 CEST (19:00 EAT) , kwenye Ukumbi wa Grimaldi huko mjini Monaco.
:
✍🏻 Jumla ya Timu 32 zitapangwa katika Makundi nane, ambapo kila Kundi Litakuwa timu Nne, na kizuizi Katika hatua hii ni kwamba timu kutoka chama kimoja haziwezi kukutana… Timu zimepangwa kwenye vyungu Vinne… Pot 1, Inahusisha Bingwa wa Ligi ya Mabingwa na Bingwa wa Europa League, pamoja na mabingwa wa vyama sita vya juu Katika UEFA!.
:
✍🏻 Atalanta ndio wageni wapya, kwa Mara ya Kwanza kabisa Katika historia ya Klabu, wanatarajia kucheza hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya..
#ChampionsLeague #UefaChampionsLeague
@Sokawaytz

Baada ya kukaa nje kwa muda akiuguza majeraha yake, nyota wa Real Madrid Eden Hazard huenda akarejea dimbani kwenye mchezo wa Ligi kuu nchini Hispania siku ya Jumapili wakati timu yake itakapovaana na Villarreal baada ya kuonekana afya yake kuimarika (Mail)
:
Majeruhi wa Real Madrid mpaka sasa 🤕 🚑 Brahim
🚑 Asensio
🚑 Hazard
🚑 Rodrygo
🚑 James
🚑 Isco

✍️ Kiungo, Tiémoué Bakayoko wa Klabu ya Chelsea anaripotiwa kufunga safari ya kurudi Monaco, na makubaliano ya The Blues na Monaco Ni kwamba Mfaransa huyo anajiunga kwa mkopo na Kipengele Cha kumnunua Baada ya mkopo kumalizika ni €35m.
.
✍️ Bakayoko alijiunga na Blues mnamo mwaka 2017 kufuatia msimu mzuri na Monaco, Klabu hiyo ya Ufaransa ilikuwa imeshinda taji la ligi Ikiwa na Nyota kibao ambao wengi wametimka Kama, Kylian Mbappe, Bernardo Silva, Benjamin Mendy, Thomas Lemar, Joao Moutinho, Fabinho, Guido Carrillo na Djibril Sidibé…. pia walikuwa vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa kwa kufika Hatua ya Nusu fainali.
.
✍🏻 Baada ya kujiunga na Chelsea, Bakayoko alipata taabu sana kuanza katika kikosi cha kwanza… Hiyo ilisababisha mchezaji kuondoka na kujiunga na AC Milan kwa mkopo… Ingawa, amerudi Chelsea msimu huu wa joto, na sasa anaonekana Hana nafasi na anaweza kurudi tena kwa mkopo, Lakini safari hii Ni Katika Klabu yake ya zamani!.
#TransferNewsUpdate #chelsea #monaco
@Sokawaytz

✍🏻 Michuano ya Copa Libertadores Sasa imefikia hatua ambayo kuikosa Ni bahati mbaya, Ni Nusu fainali za kukata na Shoka, kwetu Tanzania Muda ndio kikwazo kwa wengi, game zinapigwa Alfajiri… Hatua hii tutaamka tu.
.
✍🏻 Klabu ya @Flamengo kutoka nchini Brazil, imefuzu Kucheza Nusu fainali Baada ya kuwatupa nje Internacional pia ya Brazil Katika mechi ya Robo Fainali kwa Aggregate ya 3-1 (2-0, 1-1)… Katika hatua ya Nusu fainali, Flamengo watavaana na Wabishi, Gremio ambao wamepita sehemu ngumu Sana kwa kuwatupa nje Klabu ya Palmeiras kutoka Brazil kwa Mikwaju ya Penati 3-1 Baada ya game Kuisha na ya Aggregate ya 2-2 (0-1, 2-1).
.
✍🏻 Miamba, Boca Junior kutoka Argentina wapo hatua hii Baada ya kuwatupa nje ya Mashindano Klabu ya LDU Quito ya Ecuador kwa Aggregate ya 3-0 (3-0, 0-0)… Katika hatua ya Nusu fainali Sasa huenda wakakutana na Mahasimu wao wakubwa ambao wakikutana huwa Ni balaa tupu nje ya Uwanja Mpaka ndani ya Uwanja, River Plate Ikumbukwe walicheza fainali iliyopita ya Michuano hii huko Jijini Madrid Baada ya Kushindwa kufanyika kwao kufuatia zile vurugu… Sasa River Plate game yao Wanacheza leo dhidi ya Cerro Porteño kutoka nchini Paraguay, River Plate wanaongoza 2-0 Katika mechi ya kwanza..
:
✍🏻 Game ya Nusu fainali ya kwanza Ni Boca Junior vs Mshindi wa Jumla Kati ya River Plate au Cerro Porteño, Nusu fainali ya Pili ni Gremio vs Flamengo… Mechi zote zitapingwa Alfajiri ya Oktoba 1-2 na kurudiana Oktoba 22-23 Mwaka Huu… Fainali kupigwa huko Santiago Chile ndani ya Dimba la Taifa na mkubwa Zaidi nchini humo, Estadio Nacional Julio Martínez Prádanos.. #Libertadores #bocajuniors #riverplate
@Sokawaytz

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara (Vodacom), Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuanza kampeni ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo wakiwakabili maafande wa JKT Tanzania
Ni mchezo muhimu sana kwa Simba kupata ushindi ili kurejesha shamrashamra kwa mashabiki wake baada ya machungu ya kutolewa mapema michuano ya ligi ya mabingwa
Lakini pia ni wakati mahsusi kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru ili kuonyesha sapoti yao kwa wachezaji
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kikosi chake kiko kamili kwa mchezo huo
Amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwaunga mkono

– Champions League – Qualification.
FT Ajax 2 – 0 APOEL Nicosia
FT Club Brugge 2 – 1 LASK
FT Slavia Prague 1 – 0 CFR Cluj
.
– England – EFL Cup.
AP AFC Bournemouth * 0 – 0 Forest Green Rovers
FT Burnley 1 – 3 Sunderland
FT Lincoln City 2 – 4 Everton
AP Newcastle United 1 – 1 Leicester City *
FT Queens Park Rangers 0 – 2 Portsmouth
FT Rotherham United 0 – 1 Sheffield Wednesday
FT Swansea City 6 – 0 Cambridge United
.
– France – Ligue 1.
FT Nice 1 – 2 Marseille
.
– Egypt – Cup.
FT El Zamalek 1 – 0 Misr El-Maqasa
.
– South Africa – Premier League.
FT Baroka FC 0 – 2 SuperSport United
FT Bidvest Wits 2 – 1 Stellenbosch FC
FT Bloemfontein Celtic 1 – 2 Mamelodi Sundowns FC
FT Chippa United FC 0 – 0 Polokwane City
FT Maritzburg United 0 – 1 Black Leopards
FT Orlando Pirates 0 – 0 Lamontville Golden Arrows
.
– Tunisia – Ligue I.
FT AS Slimane 1 – 1 US Tataouine
FT CS Hammam-Lif 0 – 1 Club Africain
FT Stade Tunisien 0 – 0 Sportif de Chebba
FT CS Sfaxien 1 – 0 Etoile Metlaoui
.
– Tanzania – Vodacom Premier league.
FT Yanga SC 0 – 1 Ruvu Shooting
:
RATIBA YA HII LEO ALHAMISI. – Europa League – Qualification.
19:00 Qarabag FK
Linfield
19:45 Riga FC
FC Koebenhavn
20:00 AIK
Celtic
20:00 Apollon Limassol
PSV Eindhoven
20:00 BATE Borisov
FC Astana
20:00 Bnei Yehuda Tel Aviv
Malmoe FF
20:00 Molde
Partizan Beograd
20:00 PAOK Thessaloniki FC
Slovan Bratislava
20:00 Zorya Luhansk
RCD Espanyol
20:15 Spartak Moscow
SC Braga
20:30 Hapoel Beer Sheva
Feyenoord
20:30 Royal Antwerp
AZ Alkmaar
20:30 Trabzonspor
AEK Athens
21:00 F91 Dudelange
Ararat Armenia
21:00 Ferencvaros
Suduva
21:00 Rijeka
Gent
21:15 Maribor
Ludogorets Razgrad
21:30 Eintracht Frankfurt
Strasbourg
21:45 Rangers
Legia Warszawa
21:45 Wolverhampton Wanderers
Torino
22:00 Vitoria de Guimaraes
FC FCSB
.
– International – Friendlies :: women.
20:30 Belgium
England
.
– Tanzania – Vodacom Premier league.
16:00 JKT Tanzania
Simba SC
#Updates #fixtures
@Sokawaytz

Leo alhamis Simba inaanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa tatu mfululizo ikishuka uwanja wa Uhuru kucheza na JKT Tanzania
Mabingwa hao wa Tanzania Bara wana kazi moja tu, kuhakikisha wanaanza vizuri msimu
Wakati Yanga leo imeanza kwa kubomolewa bao 1-0 na Ruvu Shooting, ushindi kwa Simba kesho utawaweka mbele mabingwa hao wa nchi kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya watani zao mapema tu
Uongozi wa Simba umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa Uhuru kesho kuiunga mkono timu yao
Baada ya kipindi kigumu cha kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, Wanasimba wanapaswa kujitokeza kwa wingi kesho ili kuwaonyesha wachezaji kuwa wako nao