Na
@josejose189
:
Baada ya Yanga juzi kupotea kwa Ruvu Shooting hatimaye jana umepigwa mchezo mwingine wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (Vodacom Premier League) ambapo mnyama Simba ameanza Ligi vyema kwa kuwachapa maafande wa JKT Tanzania 3-1.
:
Dalili za Simba kushinda mchezo huo zilianza mapema mno mwanzoni wa dk ya kwanza tu ambapo mnyarwanda Meddie Kagere alifanikiwa kuzitikisa nyavu za maafande hao baada ya kazi nzuri ya Mzamiru Yassin iliyotokana na counter attacks iliyofanywa kupitia pembeni.
:
Erasto Nyoni akisimama vizuri kwenye safu ya ulinzi yeye na Tairone huku Tshabalala na Haruna Shamte wakikamilisha idadi ya walinzi ambalo walikuwa na jukumu la kumlinda Aishi.Bado hapajawa na combination kati ya Nyoni na Da Silva maana hawajawahi kucheza pamoja na kwa muda mrefu ila uimara wa Erasto as both senior and a key player ulimbeba na kumsaidia kutuliza timu na kui command ile defense line ya Simba,huku akisa hihisha baadhi ya makosa ya walinzi wa pembe(Tshabalala na Shamte) ambao walikuwa aggressive sana kutokana na mfumo.
:
Leo hii Aussems alianza na Mbrazil Fraga Gerson aliyekuwa akicheza chini kwenye nafasi ambayo mara nyingi amekuwa akicheza Mkude ambaye ni injured na hakuwa sehemu ya mchezo wa Leo.Uwepo wake ulimlazimu Mwalimu kumchezesha Mzamiru mbele yake kidogo huku Chama,Dilunga na Deo Kanda wakipewa jukumu la kui push timu na Kagere akisimama kama mshambuliaji wa kati.Hawa viungo ndio hazina kubwa ya Simba kwa sasa.Idadi ya viungo wengi inasaidia na kufanya timu ikabe ama ishambulie na kusaidia pia kuficha mapungufu kadhaa ya safu ya ushambuliaji.
:
Idadi hii iliwafanya JKT Tanzania kushindwa kuhimili pressure ya Simba kutokana na Simba kumiliki mpira kwa muda mrefu na kufika kwa urahisi kwenye eneo la adui.Hali hii iliwafanya JKT kujikiuta wakifanya makosa mengi kutoka kwenye safu ya kiungo hadi safu yao ya ulinzi na kuwafanya Simba kucheza kwa ari na confidence ya hali ya juu.Kazi ya Dilunga na Chama always ni kui drive timu.Wao huwa ni wepesi,wana kasi maamuzi na jicho la kuamua nini kifanyike,wapi na kwa muda gani.Kagere hakuwa na kazi ngumu zaidi ya kujiweka kwenye nafasi na kutafuta target maana walinzi wa JKT walikuwa wameshaingia kwenye mkasa wa woga uliosababisha wajiingize kwenye makosa na kuadhibiwa na wapinzani wao.
:
Kagere ni yule yule,tuliye muona msimu uliopita.Nadhani JKT walimchukulia poa.Ukabaji wake unaanzia kwa kina Dilunga na Chama.Pia inahitaji kuwepo kwa uwiano wa viungo kama waliokuwa nao Simba,kuzidiwa idadi ya viungo ni kukaribisha makosa kama yaliyo wakuta.Kazimoto na wenzake hawakuwa na kazi nyingine zaidi ya kuwa watumwa na kulazimika kutumia nguvu nyingi dhidi ya wapinzani wao.Ukiruhusu viungo was Simba wa dominate game,basi impact ya kupata matokeo lazima itakua kubwa pia kama kutakuwa na clinical finishing kwenye eneo la mwisho.
:
Game discipline pia ni moja ya jambo ambalo limewa gharimu JKT Tanzania,walitakiwa waingie kwa kuwaheshimu zaidi Simba kama timu kubwa na wao kukingia kama underdog.Kitendo cha wao kuingia uwanjani wakiwa wamekariri matokeo ya Simba dhidi ya Ud do Songo kilimfanya mwalimu wao aonekane kushiwa mbinu na wachezaji wake kushindwa kutumia uwezo wa ziada.Ujenzi wa Saikolojia ulikua wa muhimu mno kuelekea mechi hii.Nadhani mwalimu wao ameliona na atalifanyia kazi.Pia eneo lake la mwisho pia kuonekana kukosa utulivu chini ya Lyanga Danny ambaye alishindwa kutumia nafasi kadhaa za wazi.

Magoli mawili ya Kagere ni mwanzo mzuri japo ndio kwanza Ligi imeanza,lakini inamsaidia kuongeza ile ari ya kujituma na kujiamini mno hasa akijipigia hesabu za kuwania nafasi ya mfungaji bora.Pia ana play nafasi kubwa kama mchezaji muhimu anae tegemewa kwenye eneo la mwisho la timu ya Simba.Kuhusu magoli yake inabidi kabla hatuja laumu safu ya kiungo na ya ulinzi ya JKT ni vyema tukaanza kumsifia yeye kwanza,kwa kutumia akili kubwa wakati wa kufanya finishing. Ndivyo inavyotakiwa kwa mfungaji.
:
Kuhusu goli la Edward Songo wa JKT ni vyema na yeye tukampongeza,maana itakuwa sio jambo jema kuanza kumlaumu Aishi kama hatujasifia ile fantastic drive and shout out ambayo alifanya maamuzi akiwa mbali na semicircle .Mshambuliaji lazima uwe na akili ya ziada kama alivyofanya Songo Leo na yule Saadat Mohammed wa Ruvu Shooting jana aliye wafunga Yanga kwa kutumia akili binafsi.
:
Hadi mwisho wa game,Simba 3-1 JKT Tanzania.
:
Nadhani bado timu zinajipanga na ndio na Ligi ndio imeanza.Walimu watakuwa makini kifanyia kazi mapungufu yaliyo onekana ili kujenga vikosi bora na vyenye kutoa ushindani kwa mustakabali bora wa Ligi yetu.
:
Powered by @bikotanzania
Jose Jose @sokaplace_


.


















