



#

Repost from @officialfelixtz :
Hili la Kapteni Diego si sawa ! Mtanisamehe
:
Sioni kama kuna kitu cha ajabu kwa mashabiki wa Tanzania kwenda kuattack page za klabu pamoja na baadhi ya wachezaji wa Aston Villa
:
Ni kweli Samatta ni mchezaji wetu pekee kuwahi kucheza EPL lakini kitu kinachoendelea kwasasa kinafanywa na mashabiki wa soka duniani kote
:
Sijaona kipya na cha ziada kwa watanzania ambacho ni tofauti na tulichokizoea kwa mashabiki wengi duniani
:
Nitakupa mfano mdogo, Unafikiri Ronaldo na Messi wanavyoshindanishwa kwa matusi, kejeli, lugha chafu na kauli ambazo si za kiungwana wao wanafurahishwa?
:
Unafikiri wao hawaoni kama inaweza kuleta sintofahamu katika timu zao wanazozitumikia? Na vipi wachezaji wengine waliochini yao wanalichukuliaje suala la wao kudharauliwa na kuitwa majina ya ajabu ambayo kikawaida hata wewe ukiitwa unaweza ukadondosha machozi
:
Lakini mwisho wa siku wanachukulia kama changamoto za wao kuzidi kupambana, huwezi kuwapangia mashabiki kufanya unachotaka wewe
:
Mashabiki ni kitu fulani ambacho huwezi kushindana nacho, unaacha wafanye wanavyoona wao sahihi wewe endelea songa mbele
:
Sidhani kama wazungu (Uongozi wa Aston Villa pamoja na wachezaji wao hawalijui hili la mashabiki) na sitaki kuamini kwamba ni mara ya kwanza katika historia yao ya klabu
:
Wanachokijua huo ndo mpira na hao ndio mashabiki, ni vitu vya kawaida na vinatokea sehemu yoyote
:
Wao ni watu wa mpira na wanauelewa wa mpira wenyewe zaidi tunavyoujua sisi, tunaweza tukawa tunacomplain sisi wao mambo yako poa na wanaendelea na program zao hawajafikiria wala kulizungumzia suala kama hilo
:
Ninachomshauri Samatta huu ni wakati wa kipimo chake cha kucheza soka la ushindani zaidi, na soka la ushindani limebeba vitu vingi kucheza Under Pressure ni kawaida katika mpira, kikubwa ni kuona namna ya kuzihandle hizo pressure
:
Lakini suala la kuwazuia watanzania kufanya wanachokifanya ni sawa na kutaka kuyafagia maji ya bahari, kinachotokea ni kupoteza muda wako wa kuyafanya mambo ya msingi
:
NB | Manara umewakosea sana watanzania kuwaita hawajui mpira wawaachie wenye nao
:
USICHOKIJUA | Always mashabiki hawajawahi kuwa watu wakuujua mpira, wanaendeshwa na hisia za mpira 🙏
.
Kilometa 630 kutoka Zanzibar mpaka Moshi kiungo mwenye dimba lake kutoka Zenji amesafiri na kipaji chake majarab mpaka safu za mlima Kilimanjaro, mlima uliosimama mita 5,895 kutoka usawa wa bahari kwao Zenji
.
Mgongoni anayo ile jezi namba 8 jina likisomeka MACHEZO, hii jezi namba 8 wanavaa mafundi, na mafundi wapo Zanzibar bhana, Rio de Janeiro ya Tanzania
.
Kocha SELEMAN MATOLA “Veron” akiwa pale Polisi alimnunua kiungo huyu kutoka klabu ya Ndanda, si unajua tena wazungu wanasema “real recognise real”, sasa kama fundi MATOLA kamuona fundi MACHEZO basi tuendelee tu kufurahia ufundi wenye mamlaka ya RPC pale dimbani
.
Pale @polisitanzaniafootballclub yeye ndiye “RPC”, naomba mnielewe kidogo, nina maana ya RPC dimbani
.
Jina RPC ni sifa tatu za kiungo yani RADIUS, PLAYMAKER, CORPORAL
.
R – Radius, kwa wataalamu wa hesabu ‘geometry’ huu ni mstari unaoelekea popote toka katikati ya kitovu cha duara, kama nimekuacha basi chukulia picha ya spoku katika tairi la baiskeli
.
Kama lilivyo gurudumu la baiskeli basi pale dimbani MACHEZO anao uwezo wa kuwepo popote pale dimbani mithiri ya spoku, anayo ball control, mzuri mipira ya juu, speed, pasi zilizojaa upendo, na stamina kubwa
.
P – Playmaker, ana sifa ya kiungo mchezeshaji, jicho la ile killer pass, ukiwa juu we kimbia tu tafuta chumba atautuma mpira utakufikia popote ulipo, ni aina ile ya kiungo pasi mbaya anaigeuza dhahabu
.
C – Corporal, unajua kazi ya Corporal kwenye kikosi? basi nakujuza, anakazi mbili kuu CARE & CONDUCT, basi MACHEZO ndie conductor, anajua muda gani timu itembee ama ikimbie, muda gani wa pasi fupi ama ndefu, pia ndiye carer, mkiona hali ni ngumu mpeni mpira he will take good care of it, simple tu kama ABC
.
Huyu ndie RPC wa timu, akipokea pasi kutoka IGP nahodha IDDY MOBBY na kupeleka pasi za amri kwa FFU wake washambuliaji pale mbele
.
Kwenye 4-3-3 anakaa kama namba 8 kulia ama kushoto, kwenye Plan B ya 4-2-4 anaongezeka kama mshambuliaji katika box kwa mipira mirefu
.
At is!, Attention!, Salute kwa RPC @abal_machezo
.
IMEANDIKWA NA @danirito_thomson
.
#vpl #simba #yanga #polisitanzaniafc

Ndani ya mzunguko wa kwanza kuna wachezaji ambao wameonyeshwa kadi za njano na nyekundu pia orodha yao kamili ipo namna hii:-


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amepata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Azam Media na Influencer (Mtu wa ushawishi kwenye mitandao) wa La Liga Experience 2020.
Mkataba huo amesaini leo Februari,3,2020 kwa ajili ya kufanya kazi na kampuni ya Azam Media.
Manara amesema kuwa ni mkataba mwingine utakaompa fursa adhimu ya kufanya kazi na kampuni kubwa zaidi ya habari lakini pia anaamini utaiwezesha kampuni kuendelea kutangaza bidhaa zake sambamba na ligi kuu ya Spain La Liga ambayo Azam tv wanaionyesha.
HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amepata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Azam Media na Influencer (Mtu wa ushawishi kwenye mitandao) wa La Liga Experience 2020.
Mkataba huo amesaini leo Februari,3,2020 kwa ajili ya kufanya kazi na kampuni ya Azam Media.
Manara amesema kuwa ni mkataba mwingine utakaompa fursa adhimu ya kufanya kazi na kampuni kubwa zaidi ya habari lakini pia anaamini utaiwezesha kampuni kuendelea kutangaza bidhaa zake sambamba na ligi kuu ya Spain La Liga ambayo Azam tv wanaionyesha.
HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amepata dili la kuwa balozi wa bidhaa za Azam Media na Influencer (Mtu wa ushawishi kwenye mitandao) wa La Liga Experience 2020.
Mkataba huo amesaini leo Februari,3,2020 kwa ajili ya kufanya kazi na kampuni ya Azam Media.
Manara amesema kuwa ni mkataba mwingine utakaompa fursa adhimu ya kufanya kazi na kampuni kubwa zaidi ya habari lakini pia anaamini utaiwezesha kampuni kuendelea kutangaza bidhaa zake sambamba na ligi kuu ya Spain La Liga ambayo Azam tv wanaionyesha.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael amesema kuwa ana amini katika uwezo wa wachezaji wake kutokana na kile ambacho wanamuonyesha uwanjani jambo ambalo linampa matumaini ya kupata matokeo kwenye mechi zake.
Kwenye jumla ya mechi nne ambazo amekaa benchi, Eymael ameshinda mechi mbili na kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu Bara.
Alianza kwa kufungwa mbele ya Kagera Sugar mabao 3-0, akafungwa na Azam FC bao 1-0, alishinda mbele ya Singida United kwa mabao 3-1 na mbele ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0.

ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa ushindani wa msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara ni mkubwa jambo ambalo linafanya kila timu kupambana kutafuta matokeo.
“Ligi kiujumla kwa sasa imechangamka kila timu inaonyesha kile ambacho inastahili kukipata ndani ya uwanja. Timu nyingi zimegunuda siri ya kupata matokeo ni kujituma jambo hili linafanya ligi izidi kukua.
“Kwa upande wetu nasi pia tupo vizuri licha ya kupoteza mbele ya Yanga haina maana kwamba tumeshindwa. Matokeo ya mpira yanatupa mwanga wa kufanya kitu kingine,” amesema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 imecheza jumla ya mechi 18 na imejikusanyia pointi 23 kibindoni.

SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kuzisaka pointi tatu leo mbele ya Polisi Tanzania.

Kesho Jumatano, Februari,5 itakuwa na kibarua cha kumenyana na Tanzania Prisons ambayo ilishinda mchezo wake wa kwanza mwezi Februari mbele ya KMC kwa bao 1-0.

PARIS Saint-Germain (PSG) itamkosa mshambuliaji wake raia wa Brazil, Neymar Jr kwenye mchezo wa Ligue 1 utakaochezwa leo dhidi ya Nantes kutokana na majeruhi.Neymar alicheza dakika 90 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Montpellier ambao walikubali kichapo cha mabao 5-0.
Neymar alicheza dakika 90 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Montpellier ambao walikubali kichapo cha mabao 5-0.