CEO mpya simba aomba. Ushirikiano

Mtendaji Mpya wa klabu ya Simba Senzo Mazingiza amewataka Wanasimba kuendelea kushirikiana ili kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika

Mazingiza ametambulishwa leo na uongozi wa Simba akichukua nafasi ya Crescentius Magori ambaye amemaliza muda wake

Akizungumza baada ya utambulisho huo uliofanyika Hotel ya Serena, Mazingiza amesema Simba ni klabu kubwa Tanzania yenye historia ya kipekee ukanda wa Afrika Mashariki

Amewataka Wanasimba kuendelea kushirikiana ili kuifanya klabu hiyo kuwa kubwa barani Afrika

“Simba ni timu kubwa sana, nimekuwa naifatilia kwa muda sasa. Nimejifunza kuwa ni timu kubwa, na tunaweza kuifanya kuwa kubwa zaidi, sio tu ukanda wa Afrika Mashariki bali kuwa klabu kubwa zaidi Afrika,” amesema

Aidha, Mazingiza ameeleza kufurahishwa na mwamko wa mashabiki wa Simba na kuwataka waendelee kuiunga mkono timu yao wakati wote

“Nilikuwa hapa simba day nilishangazwa na mashabiki wengi waliojitokeza naomba tuendelee hivi hivi siku zote tuisapoti timu”

Naye CEO aliyemaliza mda wake Crescentius Magori, amewashukuru Wanasimba wote kwa sapoti waliyompa kipindi chote alichokuwa katika nafasi hiyo

“Kuanzia wiki ijayo nitakuwa CEO mstaafu. Nawashukuru sana kwa ushirikiano mlionipa. Nawashukuru sana Wanasimba. Kwa tuliokwazana niwaombe radhi ilikuwa sababu ya kazi yangu.”

SEMENYA AACHANA NA RIADHA NA KUIJUNGA NA YA SOKA

Bingwa mara mbili wa mbio za mita 800 kwenye michezo ya Olimpiki, Caster Semenya (28) ameanza kujiandaa kwa maisha mapya nje ya riadha baada ya kujiunga na klabu moja ya soka ya wanawake

Mwanariadha huyo kwa sasa anakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama ya Kusikiliza kesi za michezo (CAS) iliyoidhinisha matumizi ya sheria za Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) zinazotaka wanawake walio na homoni za juu za β€˜testosterone’ kutumia dawa kuzipunguza kabla ya kushiriki mashindano yoyote kitu ambacho amekataa kufanya

R

aia huyo wa Afrika Kusini ameanza kufanya mazoezi na klabu ya JVW FC kutoka mjini Gauteng akinuia kusakata mechi yake ya kwanza msimu ujao kwa sababu wakati huu kipindi cha kusajili wachezaji kimefungwa

STARS ‘FULL NONDO’ KUISAMBATARISHA BURUNDI KESHO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kipo kamili kwa ajili ya kuivaa Burundi katika mchezo wa marudiano wa kufuzu fainali za kombe la dunia utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa

.Kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mgunda amesema mapungufu yaliyo jitokeza katika mchezo uliopita wameyafanyia kazi na wana imani kubwa ya kufanya vizuri na kutinga hatua ya makundi.Mgunda amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao Watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa.

“Kikosi kipo kamili wachezaji wote wapo katika hali nzuri, mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo uliopita tumeyafanyia kazi na tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri ili kuingia hatua za makundi,” alisema Mgunda.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa jijini Bujumbura; Burundi timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.#wapendasokaupdates
#fyekaburunditusongembele

Simba yatambulisha CEO mpya

Klabu ya Simba imemtambulisha Rasmi Ofisa Mtendaji wao mkuu Mpya aliyechukua nafasi iliyoachwa na Crescentius Magori

Ofisa Mtendaji huyo Senzo Masingizi ni raia wa Afrika Kusini

Masingizi amewahi kuwa mjumbe wa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika kusini, pia amewahi kufanya kazi katika vilabu vya Fc Platinum na Orlando Pirates

Amerithi mikoba ya Magori aliyemaliza mkataba na klabu ya Simba

Magori amesimamia hafla ya utambulisho wa Bosi huyo ambayo imefanyika Serena Hotel jijini Dar es salaam

ALICHOSEMA KOCHA WA BURUNDI KUELEKEA MECHI YA KESHO DHIDI YA STARS

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Burundi, Niyungeko Alain Oliver ana uhakika wa kusonga mbele katika kufuzu fainali za kombe la dunia kwa kuifunga Tanzania katika mchezo wa marudiano utakaofanyika uwanja wa Taifa kesho jioni.

Licha ya kukiri mchezo utakuwa mgumu kwakua Stars itakuwa nyumbani, Niyungeko amesema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanashinda na kutinga hatua ya makundi.

Niyungeko ameongeza kuwa amewaandaa wachezaji wake vizuri kwakua anajua Watanzania wengi watajitokeza kuisapoti timu yao na kuujaza uwanja hivyo wao wako tayari kuikabili Stars katika kila hali. “Mchezo utakuwa mgumu na Tanzania ipo nyumbani na itapata sapoti kubwa kutoka mashabiki lakini hiyo haitutishi, tumejipanga vizuri kuwakabili na lengo letu ni kupata ushindi,” alisema Niyungeko.

#wapendasokaupdates

VIINGILIO MECHI YA STARS DHIDI YA BURUNDI

Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mchezo wa marudiano wa kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Burundi utakaopigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili.

Katika mchezo huo ambao umepangwa kuanza saa 10 jioni mzunguko utakuwa shilingi 2000 wakati VIP B na C itakuwa shilingi 5000.

Viingilio vimewekwa mahususi ili kuwafanya Watanzania wengi kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu ili ifanye vizuri na kutinga hatua ya makundi.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa jijini Bujumbura juzi Jumatano timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

#wapendasokaupdates
#fyekaburunditusongembele

Man Utd kumpa Pogba Mkataba Mpya!.

πŸ‘‰


✍🏻 Manchester United wamewasiliana na wakala wa Paul Pogba – Mino Raiola juu ya mkataba mpya wa kiungo huyo, kwa mujibu wa L’Equipe, United inataka kumbakiza Mchezaji huyo waliyemsajili kwa Rekodi ya Klabu Kutoka Juventus.
.
✍🏻 Mfaransa huyo alionekana kuwepo njiani kutimka kabla ya Msimu Huu kuanza, lakini amebaki Old Trafford na Sasa The Red Devils wanatarajia kuanza kumshawishi abaki kwa muda mrefu.
.
✍🏻 Mkataba wa Sasa wa Kiungo huyo Mwenye Umri wa Miaka 26 unamalizika msimu wa joto wa 2021 na, ikiwa hatosaini United inaweza kulazimishwa kumuuza mwishoni mwa msimu ili kuzuia kumpoteza kama Mchezaji Huru..
#TransfersNews #ManUtd
@Harunlugoyah

Rasmi Eto’o astafu soka

OFFICIAL | Legendary wa Cameroon πŸ‡¨πŸ‡², Samuel Eto’o Amethibitisha Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 38… Eto’o alianza Safari yake ya Soka Barani Ulaya Mwaka 1996 akitua Real Madrid, Baada ya Miaka 23 katika Soka kuvitumikia Vilabu 13 tofauti ndani ya Mataifa Sita tofauti, Eto’o anastaafu Soka Akiwa Nchini Qatar katika Klabu ya Qatar SC!.
.
✍️ Eto’o ndio mfungaji Bora wa Muda wote wa timu yake ya taifa ya Cameroon πŸ‡¨πŸ‡².
✍️ Eto’o ndio mfungaji Bora wa Muda wote wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika “AFCON”.
✍️ Eto’o ndio mfungaji Bora wa Muda wote wa Klabu ya RCD Mallorca.
:
✍️ Katika Vilabu: Mafanikio yake katika Mpira wa Miguu!.
πŸ†Γ—3 Laliga:
πŸ†Γ—2 Copa Del Rey:
πŸ†Γ—2 Supercopa de EspaΓ±a:
πŸ†Γ—3 UEFA Champions League:
πŸ†Γ—1 Serie A:
πŸ†Γ—2 Coppa Italia:
πŸ†Γ—1 Supercoppa Italiana:
πŸ†Γ—1 FIFA Club World Cup:
πŸ†Γ—2 African Cup of Nations “AFCON”:.
πŸŽ–οΈΓ—1 Olympic Gold Medal:
:
✍️ Mafanikio Binafsi Katika Historia yake ya Soka:.
πŸ₯‡ Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka Afrika.
πŸ₯‡Γ—4 Mchezaji Bora wa Mwaka Afrika.
πŸ₯‡Γ—1 Pichichi.
πŸ₯‡Γ—2 Mfungaji Bora wa Michuano ya AFCON.
πŸ₯‡Γ—1 Mshambuliaji Bora wa UEFA wa Mwaka.
πŸ₯‡Γ—1 FIFA Club World Cup Golden Ball:
@Harunlugoyah

Design a site like this with WordPress.com
Get started