
Ukata mkubwa ndani ya GOR MAHIA
Katika hali inayoashiria ni kuyumba kiuchumi, klabu ya Gor mahia mabigwa Γ18 wa Ligi kuu ya Kenya, imeandika barua kupitia shirikisho la soka Kenya kwenda kwenye Wizara ya michezo Kenya ikiomba msaada wa kifedha.
Wizara ya michezo Kenya imesema kwa sasa haina fedha wala bajeti ya kusafirisha timu ya Gor Mahia, hivyo safari ya mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa wa Caf dhidi ya USM Algers Jumapili sasa iko kwenye hatihati ya kushindikana.
Gor Mahia imefanya harambee Jumanne ya ukusanyaji fedha katika ukumbi wa Nairobi Charter kwa ajili ya kupunguza gharama kwa timu na kulipa madeni ya wachezaji.
Kwa ujumla hali ya kiuchumi si njema ndani ya Gor Mahia tangu kuondoka kwa waliokuwa wadhamini wakuu SportPesa, kujiondoa kutokana na kutofikia makubaliano na Mamlaka ya mapato Kenya (KRA).



















