Droo ya Kombe la Dunia la Soka la Ufukweni Imepangwa

✍️ Droo ya Kombe la Dunia la Soka la Ufukweni Imepangwa “Beach Soccer World Cup”… Afrika Kuna Wawakilishi Wawili TU 😬 Nigeria 🇳🇬 na Senegal.
.
✍️ Timu zote Mbili hizi zimefanya vizuri Sana zinaposhiriki Michuano hii, Mwaka 2007 na 2011 timu ya taifa ya Nigeria 🇳🇬 ilifika Robo Fainali Huku Mwaka 2007, 2011 na 2017 timu ya taifa ya Senegal ilifika Nusu fainali.
.

✍️ Jumla ya Mataifa 16 kuwania Ubingwa wa Dunia wa Soka la Ufukweni huko Nchini Paraguay kuanzia Novemba 21-26 zitapigwa game za hatua ya Makundi, Novemba 28 Ni game za Robo fainali, November 30 Ni game za Nusu fainali na Disemba Mosi Mwaka Huu Ni kipute Cha fainali na kutafuta Mshindi wa tatu na wa Nne.
#BeachSoccerWC
@Harunlugoyah

Mkwabi ajiuzuli.uwenyekiti sba

TAARIFA
Uongozi wa klabu ya Simba unatoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wananchi wote kwamba Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi kwa uamuzi wake mwenyewe amejiuzulu nafasi ya Uenyekiti.

Katika barua ambayo Swedi ameiandikia Bodi ya Wakurugenzi kupitia Mwenyekiti wa Bodi amesema sababu kuu ya kijiuzulu nafasi hiyo ni kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi.

Bodi ya Wakurugenzi na Sekretarieti ya Simba inamtakia kila la heri katika shughuli zake, na tunatumaini kwamba ataendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za klabu kama ilivyokuwa awali kabla kupata nafasi hiyo.

Utaratibu wa kumpata Mwenyekiti mpya tutawatangazia hapo baadae.

KATWILA ATAJA SABABU YA KIPIGO TOKA KWA SIMBA

Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Shaban Katwila amesema Simba iliwazidi kwenye kasi ya mashambulizi na kupelekea kulala kwa mabao 2-1 katika mchezo wa pili wa ligi kuu.

Katwila amesema Simba walikuwa bora zaidi yao na walifanya mashambulizi mengi ya haraka yaliyowafanya wachezaji wake kufanya makosa ambayo wamewagharimu. “Simba ilikuwa bora zaidi yetu, walitengeneza nafasi nyingi na walishambulia kwa kasi na kusababisha tufanye makosa ambayo yametugharimu,” alisema Katwila.

Kocha huyo amesema kwa sasa hawafikirii kilichotokea isipokuwa wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania wakiwa nyumbani.

Kuhusu kucheza mechi mbili wakipoteza zote Katwila amesema jambo hilo halimtishi kwakua anajua atafanya vizuri kwenye michezo ijayo ambayo imebaki mingi.

#wapendasokaupdates

POGBA, MARTIAL KUIKOSA LEICESTER KESHO

Meneja wa Manchester United, Ole Gunner Solskjaer amethibitisha kuwa katika mchezo wa kesho wa ligi kuu dhidi ya Leicester City atawakosa nyota wake Paul Pogba na Anthony Martial.

United itakuwa Old Trafford kuwakaribisha ‘The Foxes’ ambao wapo kwenye kiwango bora huku wao wakiwakosa baadhi ya nyota wake.

Martial alipata majeraha karibia mwezi uliopita wakati Pogba akipata maumivu kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa siku chache zilizopita.

Solskjaer amesema mbali na Pogba na Martial pia atamkosa Luke Shaw huku Aaron Wan-Bissaka na Diogo Dalot wakiwa na hati hati ya kutocheza.

#wapendasokaupdates #insideunited

ZAHERA: NAIFAHAMU VIZURI ZESCO HAINITISHI

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema anaifahamu vizuri timu ya Zesco United ya Zambia ambayo watakutana kesho katika mchezo wa kwanza wa klabu bingwa Afrika utakaofanyika uwanja wa Taifa.

Zahera amesema msimu uliopita amewaona Zesco katika mechi zote mbili za ligi dhidi ya Zanaco pamoja na ile ya klabu bingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe hivyo anawafahamu.

Mkongomani huyo ameweka wazi kuwa wachezaji wake wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na wapo kwenye hali nzuri kuelekea mechi hiyo. “Naifahamu Zesco niliiona katika mechi mbili dhidi ya Zanaco na ile ya TP Mazembe, ni timu nzuri lakini tumejipanga kuwakabili vilivyo. Tunahitaji kupata ushindi katika mchezo wa nyumbani,” alisema Zahera.

#wapendasokaupdates

Amunike haidai.TFF

Katibu mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Wilfred Kidao amesema hawajapokea rasmi taarifa inayosambaa mitandaoni kuhusiana na aliyekuwa kocha mkuu wa Timu ya taifa, Taifa Stars, Emanuel Amunike kudai mishahara yake na kwamba wao kama Shirikisho pia wameiona mitandaoni tu. .
.
“Hatujapokea taarifa yoyote kutoka FIFA kuhusiana na swala hilo. Hata hivyo tunachodauwa na Amunike ni Bonus ya kufuzu michuano ya AFCON na pesa ya makubaliano ya kuifundisha @taifastars_ kwa maana ya Signing

Fee.” – Kidao.

Via @boiplusmedia

Design a site like this with WordPress.com
Get started