NANI ANAJARIBU KUZIMA MOTO?

Mwambie acha, acha kabisa. Haikuwa kazi rahisi kuuwasha, acha uendelee kuteketeza vilivyosalia tuzoe majivu. Nakukumbusha tu, Afrika nzima inautamani moto wetu.

Hakuna anayetamani kukanyaga nchi hii akiwa na lengo la kupata ushindi. Wanaujua moto wetu Watanzania linapokuja suala la HAMASA waulize Waburundi watakuambia walichoshuhudia kwenye majukwaa ya uwanja wa Taifa, ulikuwa moto mkubwa. Wale ndio sisi Watanzania sasa.

Sasa tunarejea CHAN mnakumbuka tuliishia wapi?, ni pale tulipowawashia moto Wakenya kwenye majukwaa ya uwanja wa Taifa kisha tukaenda kuwawashia tena Moi Kasarani. Tunauzimaje dhidi ya Sudan?, hapana, hawa pia wanastahili moto ndani na nje.

Tunaanza nao hapa Jumapili hii Septemba 22, mshtue Mzalendo mwenzako, mwambie leo tunaanza kukusanya ‘kuni’ kwa ajili ya kuwawashia moto Sudan. Tukaujaze uwanja, tushangilie.

Moto ni ule ule….. @tanfootball @taifastars_

#wapendasokaupdates
#TunakanyagaMpakaCHAN🇹🇿

Rwanda kukipiga na DR Congo…maandalizi ya CHANI

✍️ Timu ya taifa ya Rwanda hii leo inachuana na DR Congo katika mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kwenye Uwanja wa Stade de Martyrs huko Kinshasa wakati timu zote mbili zinajiandaa na mchezo wao wa kuwania Kufuzu kwa Michuano ya CHAN 2020.
..
✍️ Ni mara ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana tangu Januari, 2016 katika robo fainali ya CHAN kwenye uwanja wa Amahoro, ambapo DR Congo ilishinda 2-1 kisha Kwenda Mpaka Fainali na kutwaa taji lao la pili la CHAN.
..
✍️ Baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Amavubi, Vincent Mashami na timu yake watasafiri kuelekea Ethiopia Siku ya Alhamisi asubuhi kwa ajili ya pambano lao la kwanza dhidi ya Ethiopia, hiyo ni Siku ya Jumapili kwenye Uwanja wa Mekelle, na mchezo wa marudiano umepangwa Oktoba 18 huko Kigali.
..
✍️ Mshindi wa Jumla wa game zote Mbili atafuzu moja kwa moja fainali za CHAN 2020 huko Cameroon 🇨🇲.. DR Congo 🇨🇩 wao watakuwa na kibarua mbele ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR- Central African Republic)..
#FriendMatch #RWNDRC
@Harunlugoyah.

Brazili…kucheza michezo ya kirafiki na timu za afrika

✍️ Mabingwa Mara tano wa Dunia, Timu ya taifa ya Brazil 🇧🇷 inatarajia kucheza mechi Mbili za Kirafiki za Kimataifa dhidi ya Mataifa ya Afrika mwezi Ujao Katika Kipindi Cha International Break huko Uwanja wa Taifa Nchini Singapore, Shirikisho la Soka Nchini humo Limethibitisha hii leo.
.
✍️ Brazil ambao Ndio Mabingwa wa Copa America Mwaka Huu, pia wakishika Nafasi ya Pili Katika viwango vya Ubora wa Soka Duniani “FIFA Ranking”, watacheza dhidi ya Nigeria 🇳🇬 siku ya Oktoba 13 na game ya Pili watacheza dhidi ya Senegal 🇸🇳 Siku ya Oktoba 10.
.
✍️ Game nyingine iliyothibitishwa Ni timu ya taifa ya Colombia 🇨🇴 itacheza Mechi ya Kirafiki ya Kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Afrika, timu ya taifa ya Algeria!.
#FriendMatch #Updates
@Harunlugoyah

Frank Lampard atangaza mpiga penati chelsea rasmi

✍🏻 Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Frank Lampard amesema Kuwa, Kiungo Ross Barkley Ndio mpigaji wa penati wa Klabu hiyo iwapo atakuwa ndani ya Uwanja.. Pia Lampard aliongeza Kuwa Kiungo kinda wa Klabu yake, Mason Mount alipata Majeraha ya kifundo Cha mguu wake na Ni Mapemaa Sana kuthibitisha itachukua Muda gani Kupona labda Baada ya Masaa 24-48 Majibu yatatoka, lakini anaamini sio Majeraha makubwa.
.

✍🏻 Mount Aliumia Mapemaa TU na kulazimika kutolewa Baada ya Dakika 16 TU Katika mechi yake ya kwanza kabisa ya Champions league dhidi ya Valencia ambapo The Blues ilipoteza usiku Jana 1-0 huko Stamford Bridge.. Wakati Chelsea iko nyuma kwa goli 1-0, Barkley alikosa Mkwaju wa penati Dakika tatu kabla ya Mpira Kumalizika!.
#chelseafc #UCLUpdates
@Harunlugoyah

RATIBA YA SOKA LEO.

#ChampionsLeague – Group A
19:55 Club Brugge vs Galatasaray
22:00 Paris Saint-Germain vs Real Madrid
:
#ChampionsLeague – Group B
19:55 Olympiacos vs Tottenham Hotspur
22:00 FC Bayern München vs FK Crvena Zvezda
:
#ChampionsLeague – Group C
22:00 Dinamo Zagreb vs Atalanta
22:00 Shakhtar Donetsk vs Manchester City
:
#ChampionsLeague – Group D
22:00 Atletico Madrid vs Juventus
22:00 Bayer Leverkusen vs Lokomotiv Moscow
:
Prepared by @officialchristz

MATOKEO YA SOKA JANA JUMANNE

#ChampionsLeague – Group E
FT Napoli 2 – 0 Liverpool
FT Salzburg 6 – 2 Genk
:
#ChampionsLeague – Group F
FT Inter 1 – 1 Slavia Prague
FT Borussia Dortmund 0 – 0 Barcelona
:
#ChampionsLeague – Group G
FT Lyon 1 – 1 Zenit St. Petersburg
FT Benfica 1 – 2 RasenBallsport Leipzig
:
#ChampionsLeague – Group H
FT Ajax 3 – 0 Lille
FT Chelsea 0 – 1 Valencia
:

Kikosi cha @yangasc dhidi ya Zesco United

1. Metacha mnata
2. Mapinduzi balama
3. Ally Mtoni
4. Lamine moro
5. Kelvin Yondani
6. Feisal salum
7. Mohammed Issa
8. Abdullaziz Makame
9. Sadney khotage
10. Pappy Tshishimbi (c)
11.Patrick Sibomana

Wachezaji wa Akiba

Farouk Shikhalo
Deus Kaseke
Mrisho Ngasa
Juma Balinya
Ally Ally
Maybin Kalengo
Muharami Issa
#wapendasokaupdates
#CAFCL

SHABIKI YANGA AAHIDI KUMPA JINA MWANAE LA NYOTA ATAKAYE IFUNGA ZESCO LEO

Shabiki wa Yanga, Akili Jumanne ameahidi kumpa jina mtoto wake aliyazaliwa usiku wa kuamkia leo mfungaji wa bao la kwanza vijana hao wa Jangwani dhidi ya Zesco United.

Shabiki huyo ametoka mkoani Iringa kwa miguu ili kuja Dar es Salaam kuisapoti Yanga katika mchezo wa klabu bingwa dhidi ya Zesco utakaofanyika leo jioni.

Akili amesema mkewe amejifungua mtoto wa kiume usiku wa kuamkia leo bado hajapewa jina na mchezaji wa Yanga atakaye funga bao la kwanza kwenye mechi ya leo atampa jina lake. “Mchezaji wa kwanza wa Yanga atakayefunga goli nitampa jina lake mwanangu aliyezaliwa jana. Ikitokea mechi imeisha kwa sare ya bila kufungana basi ataitwa Mwinyi Zahera,” alisema shabiki huyo.

#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started