Mason Greenwood aongeza makatabaManchester United

Klabu ya Manchester United inajipanga kumuongezea mkataba mpya kinda wake Mason Greenwood ambaye anaonekana kuwa na msaada mkubwa ndani ya kikosi hicho kwa miaka mingi ijayo.
:
Mbali na hilo baada ya kufunga goli pekee dhidi ya Astana lililoipa Utd alama tatu katika mchezo wa kwanza wa Europa League msimu huu Greenwood ameingia kwenye historia ya klabu hiyo kufunga goli katika michuano ya Ulaya akiwa na umri mdogo zaidi.
:
Orodha kamili iko hivi
:

🔴 Mason Greenwood (17Y 353D)
🔴 Marcus Rashford (18Y 117D)
🔴 George Best (18Y 158D)
:
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Tanzania yapanda viwango vya.ubora wa soka

✍️ Katika Orodha Mpya ya Viwango vya Ubora wa Soka Duniani “FIFA Ranking” vilivyotolewa hii leo na Shirikisho la Soka Duniani “FIFA”… Tanzania imepanda kwa Nafasi Mbili TU Duniani ikitoka nafasi 137 Mpaka Nafasi ya Sasa Ni 135..
..
✍️ Barani Afrika, Tanzania inakamata Nafasi ya 38, Huku Ukanda CECAFA Ni Nafasi ya 5/11 na Afrika Mashariki Tanzania 🇹🇿 ipo Katika nafasi ya tatu.
..
✍️ Majirani zetu, Burundi 🇧🇮 imepanda kwa Nafasi Nne, Sasa ipo Nafasi ya 144 Duniani, 40 Barani Afrika, 6 CECAFA.. Rwanda 🇷🇼 imepanda kwa Nafasi tatu, Sasa ipo Nafasi ya 130 Duniani, 36 Afrika, 4 CECAFA… Kenya 🇰🇪 ipo pale pale hakuna kushuka wala kapanda, Ipo Nafasi ya 107 Duniani na Nafasi ya 25 Barani Afrika, 2 CECAFA… Vinara ndio Uganda 🇺🇬 wakiongoza CECAFA na Afrika Mashariki, Hawa pia wapo nafasi ile ile, 80 Duniani na 16 Barani Afrika!..
#FIFARanking #WorldFIFARanking
@Harunlugoyah

Matokeo #UefaEuropaLeague

HT FC Porto 2 – 1 Young Boys
HT Rangers 1 – 0 Feyenoord
HT RCD Espanyol 0 – 1 Ferencvaros
HT Ludogorets Razgrad 0 – 1 CSKA Moscow
HT Gent 2 – 1 Saint-Etienne
HT Wolfsburg 2 – 0 Oleksandriya
HT Borussia Mönchengladbach 0 – 3 Wolfsberger AC
HT Roma 1 – 0 Istanbul Basaksehir
Europa League – Group K September 19
HT Slovan Bratislava 1 – 2 Besiktas
HT Wolverhampton Wanderers 0 – 0 SC Braga
HT Manchester United 0 – 0 FC Astana
HT HTPartizan Beograd 1 – 1 AZ Alkmaar
#sokaplaceupdates

Asamoah Gyan Sasa Kukipiga Ligi Kuu Nchini India

✍️ Nahodha wa zamani wa Ghana, Asamoah Gyan Sasa Kukipiga Ligi Kuu Nchini India, India Super League baada ya kujiunga na klabu ya NorthEast United kama Mchezaji Huru… Gyan atasafiri kwenda Guwahati mwishoni mwa wiki hii ili kuanza kazi yake mpya ambapo Mpaka Sasa amecheza vilabu kumi Katika mabara matatu. ..
🗣️ “Nimefurahi sana kuanza ukurasa huu mpya katika kazi yangu,” Alisema Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33… “Nimesikia mambo mazuri kuhusu NorthEast United FC na Indian Super League na nimefurahi sana kuwa sehemu yake kwa msimu ujao…. “Nina uhakika kwamba tunaweza kuwa bora na msimu mzuri ambao klabu ilikuwa nao mwaka jana.. Alisema Gyan.
..

✍️ Mshambuliaji huyo mwenye rekodi ya ufungaji wa Muda wote kwa Ghana na mfungaji bora wa Afrika kwenye Kombe la Dunia pia amecheza kwenye ligi kuu za England, Ufaransa na Italia pamoja na Uchina, Katua Katika Klabu hiyo iliyoanzishwa tu mwaka 2014 na kumaliza Nafasi ya Nne kwenye Indian Super League msimu uliopita… Gyan atarajia kuchukua nafasi ya mfungaji bora wa NorthEast msimu uliopita Raia wa Nigeria, Bartholomew Ogbeche, ambaye alifunga mabao 12 kabla ya kuondoka kwenda kujiunga na Klabu ya Klabu ya Kerala Blasters ya hapo hapo India!..
#TransferNewsUpdate
@Harunlugoyah

PSG vs Real Madrid .nani kuonyesha wamba

PSG vs Real Madrid
🏟Parc des Princess
⏰22.00
🏆UEFA Champions League
🛎Antony Taylor (Referee)
PSG imethibitisha wachezaji Kylian Mbappe, Edinson Cavani, Thilo Kehrer, Julian Draxler na Colin Dagba, hawatocheza kwenye mchezo wa leo dhidi ya Real Madrid kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

PSG ambao wamekuwa wakifeli sehemu ndogo baada ya kuwa na tabia ya kuanza hatua za mtoano vyema na kuja kuharibu baadaye wamesajili watu kama Idris Gueye Ander Herrera, Mauro Icadi na Keylor Navas na mashabiki wao wanahoji kama uwepo wa watu hao utaleta tofauti au la?

Neymar ataanza kutumikia adhabu ya kutocheza mechi 2 kwa utovu wa nidhamu aliouonesha kwenye mchezo dhidi ya Man United msimu uliopita hivyo hatocheza mechi ya Real Madrid na Galatasaray

Kwa upande wa Real Madrid itawakosa Sergio Ramos, Isco, Modric na Marco Asensio.

Kubaki kwa Neymar PSG kutakuwa na msaada? Usajili wa Eden Hazard pale Madrid sambamba na kubaki kwa Gareth Bale kutaleta tofauti kwenye kikosi cha Madrid msimu huu?

Mechi zote hizi zipo M-Bet kukupa ushindi! Tembelea http://www.m-bet.co.tz

#Mbet #NyumbaYaMabingwa

Aussems asema kager sugar ajipange

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hawawezi kurudia makosa yaliyopelekea msimu uliopita wapoteze michezo yote miwili dhidi ya Kagera Sugar

Septemba 26 Simba itasafiri mkoani Kagera kuwakabili Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kaitaba

Kagera Sugar ni moja ya timu ambazo zimekuwa zikiipa changamoto Simba katika misimu ya hivi karibuni

Aussems ambaye anakiandaa kikosi chake uwanja wa Gymkhana, amesema msimu huu hawatakubali kufungwa na Kagera Sugar

“Tunajiandaa vyema kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kwenye mchezo huo. Najua tunakwenda kucheza na timu ambayo msimu uliopita ilitufunga mechi zote mbili, lakini huu ni msimu mwingine, hatutarudia makosa ya msimu uliopita,” alisema

Simba inaendelea kujifua bila ya nyota wake nane ambao wameitwa timu ya Taifa ya Tanzania inayohusisha wachezaji wa ndani kwa ajili ya mchezo dhidi ya Sudan Jumapili

Design a site like this with WordPress.com
Get started