Pogba kuikosa west Ham.weekends hii

OFFICIAL: Kocha Mkuu Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer Amethibitisha Kuwa atawakosa Wachezaji wake, Paul Pogba, Luke Shaw na Anthony Martial Katika safari ya kuifuata West Ham huko LONDON UK Kati game yao ya Premier League wikendi hiii.

✍️ Daniel James pia 50/50 kuwepo au kutokuwepo Katika Mtanange huo.. #PremierLeague
@Harunlugoyah

kipa yupi ni bora kwa timu ya taifa ya Ujerumani unazidi kupamba moto.

Mjadala wa kipa yupi ni bora kwa timu ya taifa ya Ujerumani unazidi kupamba moto.

Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness amesema Marc- Ter Stegen hana lolote na hastahili nafasi ya kuanza katika timu ya taifa ya Ujerumani.

Kutokana na ubora aliouonesha kwa misimu kadhaa ndani ya Barcelona, mashabiki wengi wa Ujerumani wanaamini Ter Stegen anapaswa kuanza mbele ya mkongwe Manuel Neuer.

Ter Stegen hadi sasa amecheza michezo 22 akiwa na timu ya Ujerumani, mkogwe Manuer Neur amecheza mechi 90 hadi sasa. Ter Stegen amecheza dakika 45 tu kwenye timu ya Ujerumani ndani ya mwaka huu, 2019.

Kwa upande wako unadhani, nani anastahili kuanza kati ya Ter-Stegen na mkogwe Manuel Neur?

Manual-tutatetea ubingwa wetu

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amesema wamedhamiria kuchukua ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Manula aliyerejea kikosi mwanzoni mwa msimu baada ya kupona majeraha, amesema anaamini wana kikosi imara kitakachoweza kutwaa ubingwa

Amesema kila mchezaji aliyesajiliwa na Simba, ana uwezo wa kupambana na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo watacheza.

“Kiwango cha timu yetu hakikuwa duni, kwa namna mechi zetu mbili za mwanzo tulizocheza, tumecheza vizuri, nadhani tutaendelea kupambana katika mechi zote ili tutimize malengo yetu,” alisema Manula.

Aliongeza kwamba wachezaji waliokuwa majeruhi wamerejea katika kikosi hicho, na wameendelea kuifanya timu hiyo kuonekana kuwa na mwanzo mzuri wa msimu.

Simba imeshinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya JKT Tanzania (3-1) na Mtibwa Sugar (2-1)

Inaendelea na maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Septemba 26 uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera

RATIBA YA SOKA IJUMAA

RATIBA YA SOKA LEO
#TanzaniaFDL
16:00 Ashanti United vs Iringa United
16:00 Pamba Sc vs Arusha Fc
16:00 Gipco Fc vs Mshujaa Fc
:
#EnglandPremierLeague
22:00 Southampton vs AFC Bournemouth
:
#SpainLaLigaSantander
22:00 Osasuna vs Real Betis
:
#ItalySerie A
21:45 Cagliari vs Genoa
:
#GermanyBundesliga
19:30 Schalke 04 vs Mainz 05
:
#BelgiumFirstDivision A
19:30 Kortrijk vs KV Mechelen
:
Prepared by @officialchristz

Madrid yashindwa piga shot on target hata Moja Katika mechi ya UEFA kwa Mara ya kwanza

0 – Real Madrid imeshindwa kupiga shot on target hata Moja Katika mechi ya UEFA Champions League kwa Mara ya kwanza Tangu 2003/04… Jana walivurugwa na PSG huko Paris na Kushindwa kupata shuti lolote wakilala kwa kipigo Cha Magoli 3-0..
#UEFAChampionsLeague #RealMadrid

Ibrahim rajabu..(jeba)..afariki

SHIKAMOO KIFO,TANGULIA JEBA… Na Octa ayubu Jr…. Ibrahim rajabu “Jeba” Huenda wengi wamelisikia hili jina baada ya mishipa ya damu ya Jeba ilipokata ushirikiano na moyo wake na umauti ukatengeneza urafiki na mwili wake.

Nilitamani nikutane na Jeba nipige nae story kwa kifupi afurahi labda ningepata hata bahati ya kushuhudia tabasamu lake,anyway nahisi bado isingewezekana kutokana na userious aliokuwa nao.

Nenda Jeba,Wachache tutakukumbuka ila kariakoo utasahaurika baada ya masaa 72 tu.Utazungumziwa sana kwa kipi ulichokifanya? Ungepita kariakoo hata kusalimia miezi mitatu tungekukumbuka sana.

Nenda Jeba,mwambie Mh Joel bendera Tanzania imeshiriki Afcon ila imeambulia magoli mawili tu bila point yoyote.Mwambie kocha aliyeipeleka Misri alivorudi tu alikutana na mabegi mlangoni kwa amri ya waziri.

Mwambie Patrick mafisango,Jezi yake imemaliza mafao ya kustafishwa na sasa inatumika tu.Mwambie Simba imecheza robo fainali na msimu huu imesajili wabrazil kwa ajili ya ligi kuu maana klabu bingwa hawapo tena.

Usiishie hapo kama mtakutana na Ismail mrisho mwambie Tff yetu ilishaisahau mpaka familia yake.Mwambie Abdul suleiman anaelekea kupotea na mbao ishamsahau,hii ndio bongo.

Mwambie Godfrey Boni (Ndanje )Yanga yake ipo klabu bingwa japo hawana ubingwa wowote.mwambie viongozi wake wameshasahau hadi tarehe aliyoondoka katika hii sayari wako bize na michango ya klabu.

Nakumbuka kuna kipande cha wimbo nilimsika Ngwea akisema akifa pengo lake halina spea.Basi mwambie kweli tumekosa spea na tumeshindwa kumtengeneza ngwea mwingine.

Tangulia Jeba,Zanzibar watakukumbuka mno,Nani ataandika lile bango la “Nani kama Jeba?” Kwenye michuano ya mapinduzi? Daah ! Nimeamini chanda chema hakidumu.

Nitajitahidi nikutane na Thobias kifaru aniambie wana mpango gani kama klabu juu ya kuifariji familia ya jeba na jamii ya wazanzibar.Maana mtibwa ndio iliyomtambulisha jeba kwenye macho ya watanzania.

Mungu amlaze mahala pema fundi halisi wa soka Ibrahim Rajabu “JEBA”Niliwahi kuandika na naludia “Kariakoo ilitufanya tukamsahau Jeba”

#SokaPlaceTanzania

MATOKEO YA SOKA JANA.

:
#UefaEuropaLeague
FT APOEL Nicosia 3 – 4 F91 Dudelange
FT Qarabag FK 0 – 3 Sevilla
FT Dynamo Kyiv 1 – 0 Malmoe FF
FT FC Koebenhavn 1 – 0 Lugano
FT Basel 5 – 0 FC Krasnodar
FT Getafe 1 – 0 Trabzonspor
FT LASK 1 – 0 Rosenborg
FT PSV Eindhoven 3 – 2 Sporting CP
FT CFR Cluj 2 – 1 Lazio
FT Rennes 1 – 1 Celtic
FT Eintracht Frankfurt 0 – 3 Arsenal
FT Standard Liege 2 – 0 Vitoria de Guimaraes
FT FC Porto 2 – 1 Young Boys
FT Rangers 1 – 0 Feyenoord
FT RCD Espanyol 1 – 1 Ferencvaros
FT Ludogorets Razgrad 5 – 1 CSKA Moscow
FT Gent 3 – 2 Saint-Etienne
FT Wolfsburg 3 – 1 Oleksandriya
FT Borussia Mönchengladbach 0 – 4 Wolfsberger AC
FT Roma 4 – 0 Istanbul Basaksehir
FT Slovan Bratislava 4 – 2 Besiktas
FT Wolverhampton Wanderers 0 – 1 SC Braga
FT Manchester United 1 – 0 FC Astana
FT Partizan Beograd 2 – 2 AZ Alkmaar
:

Design a site like this with WordPress.com
Get started