Breaking Rais wa zamani wa Simba, arudishwa magereza

#Breaking Rais wa zamani wa Simba, Evans Aveva na msaidizi wake, Geoffrey Nyange Kaburu, wamerudishwa tena gerezani baada ya dhamana waliyokuwa imefunguliwa kwa ajili yao kugonga mwamba. Hii ni baada ya mshitaki ambaye ni serikali kukata rufaa ya kupinga wao kufutiwa mashitaka ya utakatishaji.

Via @globalsokatz

Cameroon yatangaza mocha mpya timu ya taifa

OFFICIAL: Shirikisho la Soka Nchini Cameroon 🇨🇲 limemtangaza Mreno 🇵🇹, António Conceição da Silva Oliveira (Toni Conceicao) Kuwa Kocha Mkuu Mpya wa timu yao ya taifa..
..
✍🏻 Conceicao Mwenye umri wa Miaka 57, ametua kuiongoza The Indomitable Lions akichukua Mikoba ya Mholanzi, Clarence Seedorf ambaye alitimuliwa Baada TU ya kutupwa nje ya Michuano ya AFCON 2019 kwa kuishia hatua ya 16 Bora..

✍🏻 Kocha huyo Tangu Mwaka 2015 amezifundisha Klabu tatu TU, CFR Cluj ya Romania ambayo Ametoka Sasa kabla ya kutua Cameroon 🇨🇲, Klabu hiyo aliifundisha kwa Kipindi tofauti tofauti msimu wa 2015 & 2018… Vilabu Vingine Ni Nea Salamina ya Cyprus na FC Penafiel ya nyumbani kwao Ureno..
#transfers #TransfersNews
@Harunlugoyah

Habari mbaya Afrika na Nchini Guinea- Bissau

✍🏻 Habari mbaya Afrika na Nchini Guinea- Bissau Ni kwamba Mshambuliaji kinda wa Klabu ya FC Barcelona, Ansu Fati amepata utaifa wa Uhispania, ambao unamruhusu sasa kuichezea timu yao ya taifa ya Hispania.
..
✍🏻 Mchezaji huyo wa miaka 16 pia anastahili kucheza nchini Guinea-Bissau, ambapo alizaliwa na pia hata Ureno kupitia kwa babu yake… Maombi ya Fati ya uraia wa Uhispania yalishughulikiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi baada ya Kufikisha umri wa miaka 10 Kama ilivyo kawaida..
..

✍🏻 Hiyo inamaanisha kuwa anaweza kuwa sehemu ya kikosi cha Uhispania kwa Michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana wa U-17 kabla ya tarehe ya mwisho kuwasilisha majina wiki ijayo na Michuano kuanza kutimua vumbi Oktoba 26 Mpaka Novemba 17 Mwaka Huu Nchini Brazil… Ingawa anaichezea Uhispania chini ya miaka 17, kanuni za FIFA zinamruhusu Fati abadilishe Uraia kabla ya kucheza Senior team..
#fcbarcelona #AnsuFati #Updates
@Harunlugoyah

Nyota walioitwa stars wamvurugia mipango Aussems

Simba imetoa wachezaji nane kwenye kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Sudan michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili, Septemba 22 kwenye uwanja wa Taifa saa moja jioni

Upungufu wa wachezaji kwenye kikosi chake umemvurugia program za mazoezi kocha Patrick Aussems

Simba inajiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodazom dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Septemba 26

Aussems amesema kukosekana kwa nyota hao pamoja na wachezaji majeruhi, kunamfanya ashindwe kuandaa mbinu za mchezo huo

Simba ina wachezaji 16 tu waliosalia kwenye kikosi baada ya Haruna Shamte, Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Miraji Athumani kuingia kambini Stars

Aidha John Bocco, Meddie Kagere na Deo Kanda nao ni majeruhi

Asamoah Gyan ajiunga na klabu ya NorthEast United ligi kuu nchini India,

Mshambuliaji Asamoah Gyan amejiunga na klabu ya NorthEast United inayoshiliki ligi kuu nchini India, hii ni baada ya mkataba wake kumalizika Julai 1, kwenye klabu ya Kayserispor ya Uturuki.

Hii itakuwa ni klabu ya 10 kwa Gyan kuwahi kuchezea toka aanze soka la kulipwa, amecheza ligi ya Italia, England, Ufaransa, Uchina, Falme za Kiarabu na Uturuki

Asamoah Gyan nahodha wa zamani wa Ghana ndiye mfungaji bora wa muda wote kwenye mechi za kimatifa akiwa na timu ya taifa ya Ghana, Mechi 107, magoli 51.

MANARA: KWENYE TIMU YA TAIFA TUACHE USIMBA NA UYANGA

Mwenyekiti wa kamati ndogo ya hamasa ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Hajji Manara amewaomba Watanzania kuacha kushangilia kwa kuangalia wachezaji kutoka Simba na Yanga.

Manara ambaye pia ni msemaji wa Simba amesema dhana hiyo sio nzuri kwa mustakabali wa soka la nchi kitu ambacho kinapaswa kuachwa mara moja.

Msemaji huyo ameongeza kuwa mchezaji anapofanya kosa au akifanya vizuri haipaswi kushangiliwa au kukoselewa kutokana na kutoka Simba au Yanga.

Manara amesema Jonas Mkude akifanya vizuri anashangiliwa na watu wa Simba wakati Kelvin Yondani akifanya kosa anazomewa na mashabiki kutoka Simba na hivyo hivyo kwa watu Yanga. “Dhana ya Usimba na Uyanga kwa sasa kwenye timu ya Taifa haina nafasi, mchezaji asishangiliwe na watu wa Simba au Yanga kutokana na kutoka kwenye timu yao isipokuwa wachukuliwe sawa sawa na wengine. “Juzi kwenye mchezo dhidi ya Burundi, Yondani alifanya kosa Kaseja akaokoa hakuna watu waliomzomea lile ni jambo zuri na linatakiwa liendelezwe kwa mustakabali wa nchi,” alisema Manara.

#wapendasokaupdates
#TunakanyagaMpakaCHAN🇹🇿

Design a site like this with WordPress.com
Get started