MCHEZAJI COASTAL UNION ALIVYOWAFANYIA KITU MBAYA SIMBA


Jumamosi iliyopita kikosi cha Simba kilipambana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Mbrazili, Gerson Fraga, lakini washambuliaji wa timu hiyo, John Bocco pamoja na Meddie Kagere kamwe hawatamsahau kipa wa Coastal Union, Sud Abdallah kwa kile alichowafanyia.
Kabla ya mchezo huo, Abdallah alimwambia kocha wake mkuu, Juma Mgunda kuwa atafanya kila liwezekanalo asifungwe na Kagere lakini pia Bocco ili aweze kuandika rekodi katika maisha ya kutofungwa na wachezaji hao ambao alidai kuwa ni washambuliaji wanaotisha kwa sasa katika ligi kuu.
Hata hivyo, mpango wake huo alifanikiwa kuutimiza kwani alifanya kazi kubwa ya kuzuia michomo iliyokuwa ikipigwa na washambuliaji hao jambo ambalo liliwafanya baada ya mechi hiyo kumalizika, wamfuate na kumpongeza.
Abdallah alisema kuwa anajivunia rekodi yake hiyo, lakini pia anasikitika kwa kufungwa mabao mawili na Fraga.
“Niliweka nadhiri kabla ya mechi kuwa nitahakikisha Bocco na Kagere hawanifungi na nimeweza kufanya hivyo, hakika najivunia hilo lakini nasikitika pia kufungwa na Fraga mabao mawili.
“Bao la kwanza alilofunga, nilikosea hesabu kidogo tu za kuuwahi mpira wa faulo uliokuwa umepigwa na Chama (Clatous Chama), lakini lile la pili naweza kusema kwamba mabeki wangu walikosa umakini kidogo.
“Baada ya mimi kupangua shuti la Hassan Dilunga walitakiwa kuuondoa katika eneo la hatari, lakini walichelewa na kumkaba Fraga ambaye alikuwa peke yake akafanikiwa kunifunga bao la pili, nampongeza pia kwa hilo,” alisema Abdallah.

Visit website

Mambo 10 nilioyaona Simba vs Polisi Tanzania

1: Sixtus Sabilo🙌 Usiku bora kabisa katika maisha yake👏 Kasi yake ilikua silaha nzito iliyowatesa sana mabeki wa Simba. Kama angekua na utulivu zaidi, angeondoka Taifa leo na bao zaidi ya moja
.
.
2: Kocha Malale Hamsini🙌 Ile plan ya 4-2-1-3 kipindi cha kwanza iliwapa wakati mgumu viungo wa Simba. Pato, Nassoro Maulid, walifanya kazi chafu sana. Walilainisha sana kazi ya Kaheza. Kama line ya ushambuliaji ya Polisi ingekua makini, wangeimaliza mechi kipindi cha kwanza.

3: Moja katika kosa kubwa atakalolijutia Malale ni ile sub ya kumtoa Jimmy Shoji na kumuingiza Mkopi🤔 Dhidi ya Simba, tena Taifa, muda ambao Simba wamewaingiza Ajib na Kagere, ilikua ni kujitengenezea kitanzi kupunguza kiungo na kuweka straika wawili. Simba inaweza kucheza vibaya kwa dakika 89, lakini dakika 1 tu watakayocheza vizuri ni hatari
.
.
4: William Lucian ‘Gallas’🙌 Uzoefu na ‘Udaresimala’ ulimtoa mchezoni kabisa Kahata. Alikata kabisa nguvu ya Simba upande wa kushoto.

5: Fraga🙌 Alikua na mechi ngumu sana. Licha ya kuwa kwenye jela ya Kaheza bado aliwasaidia sana kina Tairone kucheza na ‘movement’ za Matteo

6: Kuitambua kazi kubwa ya Pato na Nassoro ni kuhesabu ni mara ngapi Shiboub aligusa mpira kwenye dakika 45 za kipindi cha kwanza. Nilimuelewa sana Sven alipochagua kumleta Ajib mapema

7: Tarion na Kenned🤔 Dah! To be honest, ile sio quality ya wachezaji wanaostahili kuvaa jezi ya Simba. Kwa jinsi walivyokua nje kipindi kirefu, ulitegemea wawe na energy ya kutosha kuwasaidia Simba. Sasa unaelewa kwanini Nyoni na Wawa, licha ya kuwa na mchoko bado ni chaguo la kwanza kwa Simba

8: Ajib 🙌 The game changer👏 Achana na bao alilofunga, tazama jinsi alivyoivuruga kiungo ya Polisi kwa skills zake. Hakua na kasi lakini alikua na uwezo mkubwa wa kutunza mpira na kuanzisha mashambulizi ya haraka

9: Beno Kakolanya🙌 Bado nahisi shida yake kwenye kuipanga safu yake ya ulinzi lakini mikono yake imeendelea kuikoa sana Simba. Alifanya saves 2 bora sana za mechi

10: Yule Mshika kibendera😠 Naanza kupata wasiwasi na watu wanaowafundisha hawa waamuzi wetu.. This is too much aisee

Nb: Itabidi tuzoee tu😀

KOCHA POLISI TANZANIA AFICHUA KILICHO NYUMA YA KUSHINDWA MBELE YA SIMBA

MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa mchezo wake wa jana Februari,4 mbele ya Simba ulikuwa ni mzuri walichoshindwa ni uzoefu tu kupata pointi tatu mbele ya Simba.

Polisi Tanzania ilikubali kufungwa mabao 2-1 mbele ya Simba kwenye mchezo uliochezwa Uwanja Taifa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Hamsini amesema kuwa wachezaji walionyesha uwezo wao wote na walijitahidi kupambana mbele ya wapinzani wao.

“Nawapa pongezi wachezaji wangu wameonyesha kile ambacho niliwaambia wafanye na walijitahidi kwa kweli. Kilichotushinda ni uzoefu tu kwani bado timu inajijenga taratibu na kuendelea kutafuta matokeo mazuri,” amesema.

Polisi Tanzania imecheza jumla ya mechi 19 imefikisha pointi 30 ipo nafasi ya saba kwenye msimamo.

Kwenye mchezo huo walianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Sisxtus Sabilo aliyekuwa msumbufu mwanzo mwisho dakika ya 22 na yale ya Simba yakifungwa na John Bocco dakika ya 56 na Ibrahim Ajibu dakika ya 90.

Visit website

KonaYaKiufundi Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania

#

……
.
1. Mechi ilikuwa wazi kwa timu zote,kila timu ilijaribu kupigania mipango yake,ilikuwa mechi nzuri kuitazama,kila timu ilikuwa na nafasi ya kupata pointi kwenye mchezo huu..
.
2. Kwa Polisi Tanzania naweza kuwapa pongezi benchi lao la ufundi,walikuja na mpango poa sana,kipindi cha kwanza waliichukua gem kabisa,kama wachezaji wa Polisi wangekuwa na ukomavu mkubwa basi wangeweza kwenda mapumziko na zaidi ya goli moja…
.
3.Simba walionekana kuwapumzisha baadhi ya nyota wake,huku wakija na mpango ambao haukuwanufaisha sana hasa kipindi cha kwanza,bado tensition yao kutoka kushambulia kuja kukaba ni tatizo kubwa,Chama,Kahata,Shiboub kukaba ni changamoto kwao…
.
4.Polisi walijua sana kuwatumia full back wao,tunaita (inverted full back) utaona Yassin Mustapha na Wiliam Lusian walivyokuwa bora sana,lengo hasa la kiufundi ni kuwazuia full back wa simba ambao ndio msingi mkubwa wa mashambulizi ya simba,wasije juu kwa wao kupanda zaidi na kuongezeka kati,na kweli walifanikiwa,Polisi walikuwa wengi sana katikati kwenye first half,iliwapa sana simba wakati mgumu kupenya kupitia kati….
.
5. Kwenye eneo la kati mzigo ulikuwa mkubwa sana kwa Fraga,simba wakiwatumia holding midifielder wawili(double pivot) kwa maana ya Mkude na Fraga wanatulia zaidi,makosa mengi ya mabeki hupungua,lakini kwa leo eneo hili liliwapa faida kubwa polisi,walikuwa wanacheza kwa utulivu sana wakifika hapa…
.
6.Pato Ngonyani 🙌 leo ameweza kuwamudu simba kwenye eneo lake,alifanya kile alichotumwa,hatoki akishafika kwenye mtari wa kati,alikiwa bora sana leo hii..
.
7. Ajib 🙌 kwa dakika alizocheza ametukumbusha ubora aliokuwa nao msimu mmoja nyuma,ameonyesha ukomavu wa hali ya juu,anakuja kuiongezea kitu simba kwenye eneo la ubunifu,anaamua mchezo….
.
8. Kiujumla mchezo ulikuwa mzuri,Polisi walicheza muda mwingi,simba wanapata matokeo mwisho wa mchezo…
.
NB: kona hii leo inawapa 👊Pato Ngonyani na Ibrahim Ajib kwa kazi nzuri walizofanya…
.
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo

vipigo vizito hadi hivi sasa ligi kuu Uingereza msimu wa 2019/20.

#JichoLaMwewe • Vipigo Vizito
.
✍️ Jicho la Mwewe leo limekuletea vipigo vizito hadi hivi sasa ligi kuu Uingereza msimu wa 2019/20.
.
.
Mnamo tarehe 21/09/2019 Man CITY iliitandika Watford goli 8-0 katika dimba lao la Etihad.
.
Mnamo tarehe 26/10/2019 Leicester City wakiwa ugenini walitoa dozi nene ya goli 9-0 dhidi ya Southampton, hali iliyowapelekea Southampton kwenda kutoa sadaka kanisani.
.
Hivyo ndivyo vipigo vikubwa msimu huu.
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Hawa ndio Wabrazili wenye Pasi nyingi za magoli (Assists 🎯) kunako Historia ya ligi kuu Uingereza

#JichoLaMwewe • Wabrazili .
.
Hawa ndio Wabrazili wenye Pasi nyingi za magoli (Assists 🎯) kunako Historia ya ligi kuu Uingereza.
.
✍️ Coutinho > 35
✍️ Firmino > 34
✍️ Willian > 30
✍️ Oscar > 19
✍️ Juninho > 18
✍️ Fernandinho Leiva > 14
✍️ Gabriel Jesus > 14
✍️ Elano > 12
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo#JichoLaMwewe • Wabrazili .
.
Hawa ndio Wabrazili wenye Pasi nyingi za magoli (Assists 🎯) kunako Historia ya ligi kuu Uingereza.
.
✍️ Coutinho > 35
✍️ Firmino > 34
✍️ Willian > 30
✍️ Oscar > 19
✍️ Juninho > 18
✍️ Fernandinho Leiva > 14
✍️ Gabriel Jesus > 14
✍️ Elano > 12
.
#bakinasisi__ #NjooKwetu #TupoNawePaleUlipo

Mambo MATANO nilioyaona JKT vs Coastal Union

1: Yes, winning team never change, lakini kwa nature ya wachezaji wetu, Mgunda anatakiwa kuwa na plan nyingine tofauti ya kucheza ugenini. Hii 4-2-4 inawapa tabu sana ugenini. Ni kama baadhi ya wachezaji wameanza kukata upepo (hasa eneo la katikati ya kiwanja)

2: Adam Adam! Kasi yake ni tishio kwa beki yoyote yule Ligi Kuu. Changamoto yake kubwa ni maamuzi mazuri kwenye eneo la mwisho. Hana utulivu kabisa. Anafunga nafasi ngumu, anakosa nafasi rahisi

3: Ibrahim Ame🙌 Bonge la beki. Pacha wake na Mwamnyeto imeiva mno. Kama si ubora wao, makosa mengi ya mabeki wa pembeni (Kabailo na Omari) yangeigharimu sana Coastal

4: Hafidh Mussa na Mgandila waliwapa wakati mgumu sana Mtenje na Salum Ali. Walilazimisha soka la juu na nguvu. Si aina ya mpira ambao viungo wa Coastal wanapenda kuucheza

5: Edward Songo🙌 Kwangu ndie Man of the match kwenye mchezo huu. Nguvu, kasi yake iliwapa wakati mgumu sana mawinga wa Coastal kumsogelea

Kamata Matokeo Ya Soka Jana

:
👉VodacomPremierLeague
FT Simba Sc 2-1Polisi Tanzania
:
👉England – FA Cup
FT Birmingham City 2 – 2 Coventry City
P (4-1)
FT Cardiff City 3 – 3 Reading
P( 1-4)
FT Derby County 4 – 2 Northampton Town
FT Liverpool 1 – 0 Shrewsbury Town
FT Oxford United 2 – 3 Newcastle United
:
👉Spain – Copa del Rey
FT Granada 2-1 Valencia
:
👉Portugal – Cup
FT Benfica 3 – 2 Famalicao
FT Academico Viseu 1 – 1 FC Porto
:
👉Germany – DFB Cup
FT 1. FC Kaiserslautern 2 – 5 Fortuna Düsseldorf
FT Eintracht Frankfurt 3 – 1 RasenBallsport Leipzig
FT Schalke 04 3 – 2 Hertha BSC
FT Werder Bremen 3 – 2 Borussia Dortmund
:
👉France – Ligue 1
FT Monaco 1 – 0 Angers
FT Lille 1 – 0 Rennes
FT Nantes 1 – 2 Paris Saint-Germain
:
👉Tunisia – Ligue I
FT Etoile du Sahel 1 – 1 CS Sfaxien
:
👉Algeria – Ligue 1
FT ES Setif 3 – 1 USM Alger
:
👉Egypt – Premier League
FT El Gounah 1 – 0 Wadi Degla FC
:
👉International – Club Friendlies
FT OB 1 – 1 FK Radnik Surdulica
FT KF Shkendija 3 – 3 Randers FC
FT Arsenal Tula 1 – 1 Pribram
FT Stabaek 2 – 0 Banik Ostrava
FT Rapid Wien 2 – 0 Maribor
FT Partizan Beograd 1 – 3 FC Rostov
FT Ural 1 – 1 Cukaricki
:
Prepared By @officialchristz
#sokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

Design a site like this with WordPress.com
Get started