
James Maddison baada ya mashuti 31 aliyopiga msimu huu bila kupata goli lolote hatimaye shuti la 32 linazalisha bao na kuipa ushindi Leicter City mbele ya Spurs
FT | Leicter 2-1 Tottenham
Kane⚽ | ⚽Ricardo ⚽Maddison

James Maddison baada ya mashuti 31 aliyopiga msimu huu bila kupata goli lolote hatimaye shuti la 32 linazalisha bao na kuipa ushindi Leicter City mbele ya Spurs
FT | Leicter 2-1 Tottenham
Kane⚽ | ⚽Ricardo ⚽Maddison

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Juma Kaseja kuelekea mchezo wa kesho wa kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) dhidi ya Sudan hawataangalia historia ingawa ina wabeba.
Mwaka 2009 Stars iliitoa Sudan katika michuano hiyo ambayo ilifuzu na kwenda kushiriki nchini Ivory Coast kitu ambacho Kaseja anafahamu haitakuwa kazi rahisi.
Kaseja anasema Sudan iliyokuja ni tofauti ya mwaka 2009 na wachezaji ni wengine kwahiyo wamejipanga kuwakabili bila kuangalia historia kwakua haichezi uwanjani. “Sisi tumejipanga kuwakabili Sudan katika mchezo wa kesho bila kuangalia historia, tunafahamu hata wao watakuwa wamejipanga ili kulipa kisasi lakini kwa mafunzo tuliyopewa na makocha tunaamini tufanya vizuri,” alisema Kaseja.
Katika kikosi cha Stars kilichocheza na Sudan mwaka 2009 ni wachezaji wawili tu ndio wapo mpaka leo ambao ni Erasto Nyoni na Kelvin Yondani.
@tanfootball @official_juma_kaseja
#wapendasokaupdates
#TunakanyagaMpakaCHAN🇹🇿. #habarizamichezo

Kikundi cha Waandishi wa Habari za Michezo limetoa tiketi 50 kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Kurasini kwa ajili ya kushangilia kwenye mchezo wa kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kati ya Tanzania dhidi ya Sudan.
Tiketi hizo ni miongoni mwa zile 500 ambazo zimetolewa na kampuni ya uuzaji wa malori ya GF Trucks kwa ajili ya makundi maalum ili kuongeza hamasa.
Kiongozi wa Waandishi, Pascal Kabombe amewaomba watu au makampuni kutoa misaada mbali mbali kwa wenye uhitaji ili wajione ni watu wa kuthaminiwa kwenye jamii. “Tumekuja kutoa tiketi 50 kwa wadogo zetu wenye mahitaji maalum kwa ajili ya kuhamasisha katika mchezo dhidi ya Sudan,” alisema Kabombe.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii ambaye ndiye mratibu wa kituo hicho, Flora Mutagwaba amewashukuru Waandishi kwa moyo walio uonyesha huku akiwaasa waendelee kufanya hivyo mara kwa mara ili kuwapa faraja watu hao.

@gftrucks @karmali_i @pascal_kabombe @2official6 @alikamwe @giftmacha_official @devjaykihwelo_ @clifordmariondimbo
#wapendasokaupdates
#TunakanyagaMpakaCHAN🇹🇿

#EnglandPremierLeague
HT: Leicester City 0 – 1 Tottenham Hotspur
Harry Kane ⚽
#habarizamichezo

– Rais wa Real Madrid anamfikiria mchezaji wa zamani wa Liverpool na Uhispania, Xabi Alonso kuchukua mahala pake Zinedine Zidane.
.
– Mkufunzi wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho pamoja na mkufunzi wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri pia wameorodheshwa kumrithi Zidane iwapo raia huyo wa Ufaransa atafutwa kazi.
#TransferNewsUpdate

KaimuKocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, amesema mkakati wake wa kwanza ni kupata ushindi mnono nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitazofanyika mwakani nchini Cameroon.
Stars itakuwa nyumbani kumenyana na Sudan katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali hizo kwa mara pili, utakaopigwa kesho Jumapili saa moja jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Stars ambayo bado haijapata ushindi katika muda wa kawaida tangu ilipoanza kunolewa na Ndayiragije, kocha huyo wa Azam Fc amesema amefanyia marekebisho safu yake ya ushambuliaji ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo
Amesema timu iko tayari kuelekea mchezo huo
“Kikosi kipo kamili kwa ajili ya mchezo huo, wachezaji wote wako katika hali nzuri. Kikubwa ni kuhakikisha tunapata ushindi mnono nyumbani ili kujipunguzia kazi ugenini,” amesema
“Mchezo huu tutaanzia nyumbani, hivyo lazima tutumie vema faida hiyo, tunatakiwa kwenda ugenini tukiwa na mtaji mkubwa wa mabao, tulishindwa kufanya hivyo dhidi ya Kenya, tukajipa mzigo mzito ugenini, lakini safari hii tunataka kuanza vizuri kwa ushindi nyumbani”
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa Oktoba 18 nchini Uganda

Mlinda lango namba moja wa Simba Aishi Manula amemtakia kila la kheri mkongwe Juma Kaseja katika mchezo wa kesho dhidi ya Sudan
Kaseja aliyerejeshwa timu ya Taifa na Kaimu Kocha Mkuu Etienne Ndayiragije, ameendelea kuaminiwa akidaka mechi zote za hivi karibuni
Kaseja aliitwa kuchukua nafasi ya Manula ambaye mwanzoni mwa msimu alikabiliwa na majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa
Katika kikosi cha Stars kitakakochoivaa Sudan, walinda lango wote wa Simba Manula na Beno Kakolanya hawakujumuishwa kwenye kikosi hicho
Uamuzi huo ulizua mjadala mkali miongoni mwa wadau wa soka nchini wengi wakiamini Manula alistahili kurejeshwa Stars hasa baada ya kuwa amepona majeraha
Wakati mjadala huo ukiendelea, Manula amesema Kaseja ni kipa mzoefu, anamuheshimu na kama Taifa wote tunapaswa kuwaunga mkono wachezaji wa Stars kwani wanawakilisha nchi
“Unapozungumzia timu ya taifa maana yake umegusa Watanzania wanaohitaji matokeo mazuri, nawaombea baraka kwa wote walioitwa Stars wakafanye kazi kubwa”
“Sina wasiwasi na Kaseja, ameaanza muda mrefu kudaka kabla yangu na mafanikio yake yameonekana namtakia baraka tele akafanye vizuri kwa niaba ya Watanzania, ” amesema
Manula alisema kwa sasa akili yake imezama zaidi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Kipa huyo alisema anahitaji kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya na vizuri na hatimaye kutetea taji lao.
Alisema watataendelea kupambana ili mwakani waweze kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mwaka huu, kutolewa hatua ya awali na timu ya UD Songo

Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea leo kwa mechi tano kupigwa katika viwanja tofauti
Namungo Fc na Kagera Sugar zina nafasi ya kuongoza ligi kama zitashinda michezo yao leo
Namungo Fc itashuka dimba la Majaliwa kuumana na Mwadui Fc wakati Kagera Sugar iko Mwanza kuumana na Mbao Fc
Mabingwa watetezi Simba, Azam Fc na Yanga hazichezi wikiendi hii kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye kikosi cha timu ya Taifa ambacho kesho Jumapili kitaumana na Sudan kwenye mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani


Matukio kwa Picha Yaliyojiri Mwanza kwenye mchezo kati ya Alliance dhidi ya Biashara United jana
#wapendasokaupdates
#VodacomPremierLeague





Leo #PremierLeague itaanzia huko King Power ambako mabingwa wa EPL 2016 Leicester City watacheza na wanafainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya Spurs.
Leicester wanafaida ya kuwa na muda wa kutosha kupumzika tofauti na Spurs ambao wametoka Ugiriki katikati ya wiki kucheza michuano ya Ulaya huku Leicester wakiwa wamecheza Jumamosi iliyopita walipofungwa na Manchester United.
Mabingwa wa EPL Manchester City ambao wametoka kufungwa na Norwich Jumapili iliyopita watakuwa nyumbani kucheza na Watford ambao wametoka kuibania Arsenal pointi 3 muhimu katika mchezo uliopigwa Jumapili iliyopita.