KOCHA SIMBA AELEZA KINACHOMSUMBUA KUHUSIANA NA SAFU YA USHAMBULIAJI

SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa bado anasumbuliwa na tatizo la safu ya ushambuliaji kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza pamoja na safu ya ulinzi kushndwa kulinda lango.
Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi, jana Februari,4 walishinda mabao 2-1 mbele ya Polisi Tanzania ya Moshi ambao walianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kufunga bao lao pekee dakika ya 22 kupitia kwa Sixtus Sabilo aliyefunga mtaa akiwa na mabeki wawili Haruna Shamte na Keneddy Juma.

Kwa upande wa Simba, John Bocco aliweka mzani sawa dakika ya 56 kabla ya Ibrahim Ajibu kufunga bao la ushindi dakika ya 90.

Sven amesema: “Kuna tatizo ambalo lipo na nimeliona kwenye mechi zangu zilizopita na hii pia nimeliona, nitazungumza na wachezaji wangu kuona namna gani tutalimaliza tatizo hili,”.

Simba imecheza jumla ya mechi 19 ipo kileleni ikiwa na jumla ya pointi 50, imepoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui FC kwa kuchapwa bao 1-0 na ilitoa sare mbili mbele ya Yanga kwa kufungana mabao 2-2 na Tanzania Prisons ya bila kufungana.

Kamata Ratiba Ya Soka Leo

:
👉VodacomPrimierLeague
19:00 YangaSc Vs Lipuli FC
16:00 Azam Fc vs Tanzania Prison
16:00 Ndanda Fc Vs Mbao Fc
16:00 Kagera Sugar Vs Mwadui Fc
16:00 Biashara united Vs Singida United
16:00 Ruvu shooting Vs Mtibwa Sugar
16:00 Namungo Vs Alliance Fc
16:00 Mbeya City vs KMC
:
England FA Cup
22:45 Tottenham Hotspur vs Southampton
:
👉Spain – Copa del Rey
23:00 Mirandes vs Villarreal
:
👉Italy – Serie A
22:45 Lazio vs Verona
:
👉Germany – DFB Cup
20:30 Bayer Leverkusen vs VfB Stuttgart
20:30 SC Verl vs 1. FC Union Berlin
22:45 1. FC Saarbrucken vs Karlsruher SC
22:45 FC Bayern München vs Hoffenheim
:
👉France – Ligue 1
21:00 Toulouse vs Strasbourg
21:00 Montpellier vs Metz
21:00 Lyon vs Amiens
21:00 Nimes vs Dijon
21:00 Brest vs Bordeaux
21:00 Reims vs Nice
23:00 Saint-Etienne vs Marseille
:
👉Algeria – Ligue 1
20:45 JS Kabylie vs NA Hussein Dey
:
👉Egypt – Premier League
20:30 El Zamalek vs El Hodood
:
👉Morocco – Botola Pro
19:00 Raja Casablanca vs OCK Khouribga
21:00 Hassania Agadir vs Ittihad Tanger
:
👉Tunisia – Ligue I
16:00 Esperance vs US Monastir
:
👉Ghana – Premier League
18:00 Berekum Chelsea FC vs Karela United FC
18:00 Ebusua Dwarfs vs Aduana Stars
18:00 Eleven Wonders FC vs Inter Allies FC
18:00 King Faisal vs Accra Great Olympics
18:00 Legon Cities FC vs Elmina Sharks
18:00 Liberty Professionals vs Dreams FC
18:00 Medeama SC vs Bechem United
18:00 Sogakope Wafa vs Asante Kotoko
:
👉Nigeria – NPFL
18:00 Lobi Stars vs Enugu Rangers
18:00 MFM FC vs Enyimba
:
Prepared by @officialchristz
#SokaplaceUPDATES
@danirito_thomson

JOSE MOURINHO AANZA MIKWARA YAKE KWA NYOTA WAKE MPYA SASA

JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Spurs amesema kuwa anaamini nyota wake mpya Steven Bergwijn ataonyesha makubwa mbele ndani ya timu yake.

Raia huyo wa Netherlands aliyekuwa akikipiga PSV Eindhoven alifunga bao lake la kwanza akiwa na timu yake ya Spurs mbele ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.

Mourinho amesema kuwa hakuna haja ya kujiuliza maswali mengi juu ya kijana huyo ana amini ataonyesha kazi kubwa ndani ya Uwanja.

Bao la kwanza alifunga Bergwijin dakika ya 63 na la pili lilifungwa na Son Heung-Min dakika ya 71 na kuwafanya Spurs kufikisha jumla ya pointi 37 nafasi ya tano huku City wakiwa na pointi 51 nafasi ya pili.

Visit website

MNAOCHIPUKIA MSIZIPE NAFASI PROPAGANDA ZA HUMUD WA MTIBWA SUGAR

MNAOCHIPUKIA MSIZIPE NAFASI PROPAGANDA ZA HUMUD WA MTIBWA SUGAR

Na Saleh Ally
TUMEKUWA na kawaida ya kubadilisha uchukuliaji wa mambo. Yale ya kawaida tukayapa uzito sana na mazito tukayachukulia kuwa mepesi tu, nafikiri ni utamaduni.
Kuna wakati unalazimika kubadili mambo kadhaa ili kuwa kwenye utaratibu mzuri ambao ni sahihi. Si jambo jema kufanya mambo bila ya kutafakari.
Kiungo wa Mtibwa Sugar, Abdulhalim Humud, amefanya kitu ambacho hakikuwa sahihi na kinatengeneza makwazo kwa mashabiki wa Mtibwa Sugar lakini inawezekana viongozi, makocha na hata wachezaji wenzake.
Wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga mwishoni mwa wiki iliyopita, Mtibwa Sugar walilala kwa bao 1-0 na baada ya mchezo huo, Humud ambaye ni kiungo mkongwe, alibadilishana jezi na kiungo wa Yanga, Papy Tshishimbi.
Baada ya hapo, Humud alikwenda moja kwa moja kuhojiwa na Azam TV na alionekana akiwa na jezi hiyo. Hili si jambo baya, soka si uadui na hiyo ndiyo fair play.
Alipotoka katika mahojiano hayo, Humud alikwenda moja kwa moja hadi eneo walipo mashabiki wa Yanga na kuanza kupiga nao picha akiwa anaonekana amevaa jezi ya Yanga.
Hakuna ubishi, tunaona jambo hili ni la kawaida lakini katika maisha ya kiushindani na hasa kwa wachezaji, makocha na viongozi halileti picha nzuri.
Jaribu kuwaza, kwamba baada ya mechi kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham mara tu baada ya kwisha, Salah anavaa jezi ya Tottenham halafu anakwenda upande walipo mashabiki wa Spurs na kuanza kupiga nao pia! Hili linawezekana kweli?
Au leo hii, mechi kati ya Aston Villa dhidi ya Arsenal, baada ya mechi Samatta abadilishane jezi na David Luiz halafu anakwenda upande walipo mashabiki wa Arsenal anaanza kupiga nao picha. Unaamini hili litakuwa sahihi? Najua unaweza ukasema hapana lakini kwa kuwa kule ni England. Mpira una misingi na miiko na lazima ifuatwe.
Humud ni mchezaji wa Mtibwa Sugar, ingependeza kama atapiga picha na mashabiki wake wa Mtibwa Sugar ambao walikuwa pale uwanjani kumuunga mkono. Wakati mashabiki wako wanashindana na wale wa timu pinzani baada ya mechi, unavaa jezi ya timu pinzani na kwenda kupiga picha na wale wanaoshangilia timu pinzani.
Kuvaa jezi inawezekana, ingawa nayo si sahihi zaidi kwa mchezaji wa Azam FC kuwa anahojiwa akiwa amevaa jezi ya Simba au yule wa Simba aende kuhojiwa akiwa amevaa ya Mtibwa. Inapendeza kuwa na jezi ya timu yako ndiyo maana unaona wachezaji wengi hawabadilishani jezi pale uwanjani, wanafanya hivyo baada ya kuingia vyumbani ili kuepuka matukio kama hayo ya Humud.
Unaweza kusema mashabiki waliniita wenyewe, kama mchezaji unayejielewa unaweza kutambua kuwa si sahihi kufanya hivi kwa wakati huu. Mfano, Humud angeweza kupiga picha na mashabiki wa Yanga wakati mwingine barabarani au kwingineko lakini si siku wametoka kucheza na Yanga na papo hapo unakwenda kupiga na mashabiki wao.
Kuna watu wamekuwa na hisia kwamba, Humud anajipigia debe siku moja atue Yanga. Inawezekana lakini kwa mchezaji hahitaji vituko kusajiliwa na timu fulani. Huenda wengi wanaweza wakawa wanafananisha na lile tukio la Mrisho Ngassa kuvaa jezi ya Yanga wakati akiwa Azam FC tena akionyesha wazi alikuwa akifanya visa na baadaye kweli alisajiliwa Yanga.
Kama kweli Humud atakuwa anafanya hivyo kwa kufanya vituko hivyo ili atue Yanga, atakuwa hajitambui na anapaswa kubadilika. Yanga ya sasa watakuwa tofauti kidogo na watakachoangalia ni uwezo wa wachezaji na si wale wanaoipenda tu (kama sijakosea).
Unaona wakati wenzake wakiwa vyumbani, Humud alikuwa akipiga picha na mashabiki wa timu pinzani. Wakati wachezaji wakiingia vyumbani, walimu hupata nafasi ya kuzungumza na wachezaji wao kabla ya kufanya maandalizi kidogo na kuondoka uwanjani hapo.
Humud kuendelea kupiga picha na mashabiki hata kama wangekuwa wa Mtibwa Sugar wakati wenzake wakiwa vyumbani ambao ni utaratibu sahihi, nayo ni sehemu ya utovu wa nidhamu.
Hata kama maandishi haya yatamkwaza, sitajali sana kwa kuwa mimi namuona Humud ni mchezaji mkongwe, anapaswa kuwa mfano katika mengi kuhusiana na soka na hasa suala la nidhamu na kufuata weledi wa anachokifanya ili awe mfano kwa vijana wanaochipukia.
Niliwahi kuandika kuhusiana naye aliposema maneno ya dharau kwa Didier Drogba nikimkumbusha hakuwa kiwango chake na baadaye naamini aliona.

Visit website

Azam yatuma ujumbe kwa Tanzania prisons


AZAM FC, leo Februari,5 itakuwa Uwanja wa Taifa saa 10:00 Jioni kumenyana na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Februari,2 ilianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Samora.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wanatambua wana kibarua kizito leo ila watapambana kupata matokeo mazuri.
“Kazi ni nzito na ushindani ni mkubwa, wachezaji wapo sawa na wanatambua kazi yao ni kutafuta matokeo uwanjani, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema,
Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza jumla ya mechi 18 imejikusanyia pointi 37,

NYOTA MPYA WA MANCHESTER UNITED APEWA MUDA WA MWEZI MMOJA NA KOCHA WAKE

QUIQUE Sanchez, aliyekuwa Kocha Mkuu wa nyota mpya wa Manchester United, Odion Ighalo amesema kuwa itamchukua muda wa mwezi mmoja mchezaji huyo kufikia mafanikio anayoyafikiria ndani ya Ligi Kuu England.
Sanchez alikuwa Kocha wa Odion wakati akikipiga ndani ya Klabu ya Watford na raia huyo wa Nigeria alitupia jumla ya mabao 17 ndani ya msimu alipokuwa akikipiga ndani ya Klabu ya Shanghai Shenua ya China kwa muda mfupi aliokuwa hapo.
Manchester United ina matumaini makubwa kwa nyota huyo mwenye miaka 30 ambaye ametua hapo kwa mkopo kuwa mbadala wa Marcus Rashford ambaye anasumbuliwa na majeruhi.
“Tatizo ni kwamba mafundisho aliyokuwa anayapata ndani ya ligi ya China pamoja na ligi ya England jambo ambalo linamfanya awe kwenye wakati mgumu kwenye mechi zake za mwanzo atahitaji muda wa mwezi mmoja kurejea kwenye ubora.
“Uzuri ni kwamba ninamtambua vema kwa upande wa uwezo wake ndani ya Uwanja pamoja na mwili wake ulivyo atafanya mambo makubwa,” amesema.

Visit website

VIRGIL VAN DIJK KUONDOKA LIVERPOOL

HUKO ughaibuni, taarifa inayosambaa kwa kasi ni Juventus kujipanga kumng’oa beki wa Liverpool, Virgil van Dijk katika dirisha lijalo la usajili wa majira ya joto barani Ulaya.
Taarifa iliyoandikwa na Gazeti la The Sun la Uingereza jana, ilieleza kuwa Juve wamemtengea beki huyo donge nono la pauni milioni 150, sawa na Sh bilioni 456.
Miamba hiyo ya Serie A inaamini kuwa Mholanzi huyo atakuwa tayari kutafuta changamoto mpya kama timu yake ikibeba ubingwa wa Premier msimu huu na wanataka kumfanya awe beki ghali zaidi duniani kwa mara nyingine tena.
Tangu atue Anfield, Van Dijk ameisaidia Liverpool kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Dunia la Klabu na Uefa Super Cup huku wakiwa mbioni kubeba ubingwa wa kwanza wa Premier baada ya kupita miaka 30.

Visit website

DAKIKA 90 SIMBA SC VS POLISI TANZANIA FC .

Timu iliyokuwa bora imepoteza mchezo, Simba hawakuwa katika kiwango bora
.
Kocha wa Polisi Tanzania alikuwa jasiri sana, kuja ugenini na 4-3-3 na kumpa Simba wakati mgumu kwa kucheza na front three yenye kasi kubwa ambayo kwa muda mwingi walikaa juu kabisa
.
Sabilo kushoto, Matheo Anthony kati, kasi yao ilifanya beki za Simba wasisogee mbele mara kwa mara na kumfanya Dilunga na Kahata kutopata support ya movements wakati wa mashambulizi
.
Lucian na Yassin walifanya kila njia winga za Simba zisipate mpira wakiwa comfortable, kila mpira ulipoenda pembeni basi Kaheza ama “RPC” Hassan Nassor alisogea kuongeza nguvu
.
Hivyo pasi zilirudi kwa mabeki wa pembeni wa Simba wakiwa karibu na eneo la kati, hii ikapunguza hatari kwa Polisi
.
Polisi kupossess mpira kwa kadri wawezavyo, na hata baada ya kupata goli walijitahidi kukaa na mpira na kui-frastuate Simba
.
Siri ilikuwa moja tu, walipiga pasi nyingi kwenda pembeni na kuswitch uwanja kwa pasi ndefu kila Simba wakisogea, pale kati ilikua ni one touch mwisho two touch mpira umeondoka
.
Kaheza alikuwa akigusa mara moja, Pato Ngonyani yeye alikua akihamisha itoke kulia iende kushoto, “RPC” Hassan Nassor ndie pekee alikua na kibari cha kukaa na mpira
.
Sabilo na Matheo walikimbia sana kwenye migongo ya mabeki wa Simba kwa faida ya kasi zao
.
Yule Sabilo, wow, ana kasi ya hatari, ile ni kasi ya treni za Standard Gauge, hakika Shamte leo hatolisahau jina lake
.
Simba katika 4-2-3-1, Shiboub, Dilunga hakuwa na siku nzuri, pia kwa Kennedy utulivu ulikuwa chini
.
Gerson Fraga “The Grip” kazi ni moja tu kukata umeme, kidogo ajisahau akazima na taa za uwanja 😂
.
Sub za kocha Sven zilibadili mechi. Ajib, Chama, Bocco walionyesha utulivu sana, kama vile walijua magoli yapo. Goli la pili movement ya Kagere kwenda pembeni ndiyo chachu, alikimbia nyuma ya mgongo wa Yassin na kumuacha Bocco aingie kati, hii ilivuruga utulivu wa mabeki
.
Ni mwendelezo wa tamthilia ya OFFSIDE RULE, waamuzi wa pembeni bado wanapata shida kutafsiri sheria namba 11, ipo shida kubwa, japo wapo under pressure sana, ila bado sio kisingizio
.
Imeandikwa na @danirito_thomson
.
#simba #vpl #yanga

KISA YANGA MZAMIRU HALI TETE SIMBA

KIUNGO wa Simba, Mzamiru Yassin, ataendelea kuzikosa mechi za timu hiyo, kutokana na kusumbuliwa na tatizo la goti analodaiwa kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga Januari 4, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Tangu siku hiyo, Mzamiru hajaonekana uwanjani akiwa amevaa jezi nyekundu na nyeupe katika mbio za timu hiyo za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Hata hivyo, baadhi ya mashabiki wa Simba ambao walikuwa hawajui kama Mzamiru ni majeruhi, tayari walikuwa wameanza kuutolea shutuma uongozi wa timu hiyo, wakiutuhumu kuwa umemsimamisha kutokana na kosa la kimchezo alilofanya uwanjani katika mechi dhidi ya Yanga.
Kosa hilo ni lile lililoiwezesha Yanga kupata bao baada ya kupokonywa mpira na Mapinduzi Balama ambaye aliifungia timu yake moja kati ya mabao iliyoyapata kwenye mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, Mzamiru ni majeruhi na anaendelea na matibabu ya goti na wala hakuna tatizo lingine dhidi yake.
“Mzamiru ni majeruhi na yupo nje ya uwanja akiendelea kupata matibabu, yeye pamoja na wachezaji wengine ambao ni Miraji Athumani ‘Sheva’ pamoja na Deo Kanda.
“Hata hivyo, hali zao kwa pamoja wanaendelea vizuri na muda wowote pindi watapokuwa wamepona, watarejea uwanjani kuendelea kuitumikia timu yetu, hayo mengine yanayosemwa ni uzushi tu na siyo kweli,” alisema Rweyemamu.
Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, amesema kuwa anawamisi wachezaji hao katika kikosi chake kutokana na majareha yanayowasumbua.
Lakini alisema kuwa, anawaombea waweze kupona haraka na kurudi uwanjani kuendelea kuitumikia timu hiyo katika harakati zake za kutetea ubingwa wake.

Visit website

Design a site like this with WordPress.com
Get started