ALLY SALIM AREJEA KIKOSINI NGORONGORO HEROES

Golikipa namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara chini ya umri wa miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ Ally Salim amerejea kikosini baada ya kukaa nje ya uwanja kwa siku tatu kufuatia kuumia bega kwenye mechi dhidi ya Kenya.

Golikipa huyo wa Simba leo Jumamosi amefanya mazoezi na wenzake kujiweka fiti kwaajili ya mechi ya robo fainali ya michuano ya CECAFA Chalenji dhidi ya wenyeji Uganda utakaopigwa kesho Jumapili.
Daktari wa timu hiyo, Shecky Mngazija, amesema, “Tulimpa Ally mapumziko ya siku tatu baada ya kuumia lakini sasa yuko fiti na amefanya mazoezi yote. Kuhusu kuwa atacheza ama la, ni maamuzi ya kocha Mkuu.” Akizungumzia maandalizi ya mechi ya kesho, Kocha Mkuu, Zuberi Katwila amesema anafahamu kuwa kucheza na wenyeji ni kazi, lakini atatumia dakika 10 za mwanzo kuwasoma ili aweze kujua mbinu zaidi za kuwamaliza. “Tumesafiri jana, haikuwa safari nyepesi lakini leo tumefanya mazoezi mepesi kuwaweka wachezaji sawa kwaajili ya mechi. Utakuwa mchezo mgumu maana tunacheza na mwenyeji na hatujabahatika kumuona akicheza,” amesema Katwila. “Siwezi kubadili mbinu ambazo zimetufikisha hapa. Tunajipanga kushinda na vijana wako kwenye hali nzuri kushindana,” Mechi nyingine za robo fainali hapo kesho ni Burundi dhidi ya Kenya, Zanzibar na Eritrea zitakazochezwa Jinja wakati mechi nyingine hapa mjini Gulu ni Sudan dhidi ya Sudan Kusini.

#wapendasokaupdates

WABABE WA SIMBA UD SONGO WAPINGWA NGUMI ZA USO NA WAJUKUU WA MGABE. . :

CAF Champions League :
First Round 2nd Leg
UD Songo 🇲🇿 2-4 🇿🇼 FC Platinum (Agg 2-5)
:
Ifren Matola⚽
Stélio Marcelino Telinho⚽
Rodwell Chinyengetere ⚽⚽⚽
Never Tigere ⚽
:
Klabu ya FC Platinum inafuzu katika hatua ya Makundi katika klabu bingwa barani Afrika.

#TotalCAFCL

Livepool…yaweka rekodi mpya EPL

Georginio Wijnaldum sasa kafunga magoli 22 katika Maisha yake ndani ya Premier League… Magoli Matatu TU kati ya hayo yote kafunga viwanja vya Ugenini.

– Ni timu mbili tu sasa katika Historia ya Premier League zimeshinda game sita mfululizo tangu kuanza kwa msimu wa Ligi…
👉Chelsea 2005/06:
WWWWWWWWW

👉Liverpool 2019/20:
WWWWWWW
.
– Liverpool imeshinda mechi sita za mwanzo wa msimu wa Ligi kwa Mara ya Pili pekee katika Historia ya Klabu – Walishinda kwa Mara yao ya kwanza mechi nane mfululizo msimu wa 1990-91.
#PremierLeague #liverpool
@Harunlugoyah

Mambo yaliyojitokeza wakati wa mechi ya yanga vs zesco

Mambo kadhaa niliyogundua kwenye mchezo wa klabu Bingwa Barani Afrika.
.
.
Approaching ya Mwinyi Zahera, Ilikuwa inaonyesha kwenye makaratasi wanatumia mfumo wa 4-3-3 wakiwa wanashambulia pale wanapokuwa hawana mpira walikuwa wakicheza 4-2-3-1.
.
.
Abdul Azizi Makame, ni kiungo mzuri sana ana pora mpira ana nguvu ila amekosa utulivu nafikiri tuendelee kumpa mda ana kitu mguuni mwake ilikuwa kombineshi nzuri baina yake na Feisal Toto.
.
.
Sifa ya kwanza ya beki ni kufanya majukumu ya ulinzi alafu vingine ndo vinafuata Sonso, ametuaminisha leo alifahamu ubora wa Zesco, eneo la pembeni.
.
.
Ukiachana na Azizi Makame, kujifunga bao hilo me cha kwanza namlaumu Ali Ali, alitakiwa acheze faulo ambayo ingekuwa na faida kwao na wachezaji wa Yanga, wangerudi kukaba, huwa tunasema kadi ya Timu.
.
.
Safu ya ulinzi ya kati sina shida yao Lemina, ni mwamba atakayekuja kuvaa viatu vya Cotton, hapo badae ile kadi nyekundu ilikuwa sahihi kwa sababu alikuwa na kadi moja ya njano. .
.
Metacha Mnacha, leo kwangu ndo nyota wa mchezo katika timu ya Yanga, anazidi kuimaliki kwenye michezo mikubwa kama hii.
.
.
Yanga, wanatumia nguvu nyingi kipindi cha kwanza, kipindi cha pili wanachoka sana rudi katika mchezo wa kwanza utagundua hichi kitu. .
.
Yule Kalengo wa Zesco, ni mwiba sana kwa upande wa Yanga, huenda wasimsahau afungi yeye ana kazi ya kutengeneza tu mipango.
.
.
Kila mabadiliko ya Zesco, yalikuwa yana faida kubwa sana kwao wachezaji wao wengi wana uwezo wa mchezaji moja moja.
.
.
Yanga, walihitaji waendelee kushambulia na kuzidi kutengeneza presha kwa Zesco, na sio kuzuia unapozuia muda wote unampa nafasi mpinzani akushambulie. .
.
✍🏻@azizi_mtambo_15 wa @sokaplace__

TSHABALALA ASEMA WALIINGIA KWA TAHADHARI KUBWA DHIDI YA KEGERA JANA

Nahodha msaidizi wa timu ya Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ amesema katika mchezo wa jana wa ligi dhidi ya Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba waliingia kwa tahadhari kubwa kwakua hawakutaka kupoteza tena mbele yao.

Katika miaka miwili Simba haikupata ushindi kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kagera kitu ambacho kiliwafanya kujipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda ili kufuta jinamizi la kupoteza mechi mbele ya ‘Wanankurukumbi’ hao.

Tshabalala ambaye katika ushindi wa mabao 3-0 waliupata Simba jana yeye alifunga bao la pili aliongeza kuwa ilibidi wachukue tahadhari kuhakikisha washambuliaji wa Kagera hawaleti madhara langoni kwao huku wakitumia kila nafasi watakayoipata. “Tulijua hatuna historia nzuri dhidi ya Kagera ikabidi tuchukue tahadhari, tutumie kila nafasi tutakayopata na tuhakikishe hatufanyi makosa ambayo yatatugharimu kitu ambacho tulikifanya, tunamshukuru Mungu tulifanikiwa,” alisema mlinzi huyo wa kushoto.

Nahodha huyo amewataka Wana Simba wenye uwezo wa kwenda kuwapa sapoti katika mchezo unaofuata dhidi ya Biashara United kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili.

@simbasctanzania @official_mohamedhussein15
#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started