MO atbelea uwanja binju

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ leo alitembelea viwanja vya klabu hiyo ambavyo viko kwenye matengenezo Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam

Mo ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa viwanja hivyo ambapo amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwezi ujao (Oktoba), Simba itaanza kufanya mazoezi

“Leo asubuhi nilitembelea viwanja viwili vya mazoezi vya Simba vilivyopo Bunju kuangalia maendeleo,” ameandika Mokwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instargam

“Nina habari njema, kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba, uwanja wa nyasi asilia na nyasi bandia pamoja na vyumba vya kubadilishia nguo vitakuwa vimekamilika”

“Insha’Allah! Natarajia kuona timu ikifanya mazoezi hivi karibuni”

Legendary wa Atlético Madrid, Diego Forlán..aagwa kwa heshima

Legendary wa Atlético Madrid, Diego Forlán akiagwa kwa heshima huko Wanda Metropolitano kuelekea Derby ya Madrid. Hii yote Ni kumtalia kheri kwani mchango wake wa kupendeza unaendelea kukumbukwa. Mkongwe huyo alitangaza kustaafu soka mwezi uliopita.
….
– Diego Forlán alifunga mabao 32 katika michezo 33 ya LaLiga katika Msimu wa 2008-09, Magoli mengi zaidi ya mchezaji yeyote wa Atlético Madrid karne hii kufunga katika msimu mmoja wa ligi msimu huu… Mshindi wa mwisho kubeba Pichichi kwa mchezaji asiye wa Barcelona au Real Madrid..
#AtleticoMadrid #Laliga
@Harunlugoyah

MATOKEO YA SOKA JANA.

#TanzaniaFDL
FT Rhino Rangers 1-0 Sahare
FT Mashujaa 1-0 Mawenzi Market
FT Arusha Fc 1-0 Transit Camp
FT Pamba 1-2 Geita Gold
FT Gwambina 2-2 Gipco
:
#VodacomPrimierLeague
FT Singida United 0-1 Allience Fc
FT Mwadui Fc 1-1 Mbao Fc
FT RuvuShooting 1-0 Polisi Tanzania
:
#FdlTanzania A
FT Mbeya Kwanza 2-2 Jkt Mlale
FT Cosmopolitan 3-3 PanAfrican
FT Friends Rangers 2-0 African Lyon
FT Boma Fc 1-0 Dodoma Fc
FT Ihefu 0-0 Njombe Mji
:
#EnglandPremierLeague @sokaplace__
FT Sheffield United 0 – 1 Liverpool
FT AFC Bournemouth 2 – 2 West Ham United
FT Aston Villa 2 – 2 Burnley
FT Chelsea 2 – 0 Brighton & Hove Albion
FT Crystal Palace 2 – 0 Norwich City FT Tottenham Hotspur 2 – 1 Southampton
FT Wolverhampton Wanderers 2 – 0 Watford
FT Everton 1 – 3 Manchester City
:
#SpainLaLigaSantander
FT Athletic Bilbao 0 – 1 Valencia
FT Getafe 0 – 2 Barcelona
FT Granada 1 – 0 Leganes
FT Atletico Madrid 0 – 0 Real Madrid
:
#ItalySerieA
FT Juventus 2 – 0 SPAL
FT Sampdoria 1 – 3 Inter
FT Sassuolo 1 – 4 Atalanta
:
#GermanyBundesliga @sokaplace__
FT Mainz 05 0 – 1 Wolfsburg
FT Augsburg 0 – 3 Bayer Leverkusen
FT RasenBallsport Leipzig 1 – 3 Schalke 04
FT SC Paderborn 07 2 – 3 FC Bayern München
FT Hoffenheim 0 – 3 Borussia Mönchengladbach
FT Borussia Dortmund 2 – 2 Werder Bremen
:
#FranceLigue1
FT Lyon 0 – 1 Nantes
FT Bordeaux 0 – 1 Paris Saint-Germain
FT Monaco 4 – 1 Brest
FT Angers 1 – 1 Amiens
FT Metz 2 – 2 Toulouse
FT Nice 1 – 1 Lille
FT Reims 1 – 2 Dijon
:
#BelgiumFirstDivisionA @sokaplace__
FT KV Mechelen 0 – 5 Club Brugge
FT Cercle Brugge 1 – 2 Eupen
FT Gent 2 – 0 Kortrijk
FT Royal Excel Mouscron 2 – 2 Zulte Waregem
FT St.Truiden 3 – 3 Genk
:
#AfricaChampionsLeague
FT UD Songo 2 – 4 Platinum FC
FT ZESCO United 2 – 1 Young Africans
FT Al Ahly 4 – 0 Cano Sport
FT Raja Casablanca 1 – 1 Al-Nasr Club
:
#AfricaConfederationsCup
FT CNaPS Sport 1 – 3 TS Galaxy FC
FT Proline 2 – 1 AS Kigali
FT Triangle United FC 1 – 0 Azam FC
FT Zanaco FC 3 – 0 Bolton City
FT Salitas FC 0 – 0 Esae *
FT Hassania Agadir 0 – 0 Al-Ittihad
FT RSB Berkane 2 – 0 Ashanti Gold

Imeandaliwa na @officialchristz wa @sokaplace__

AZAM YAONDOSHWA NA WAZIMBABWE SHIRIKISHO

Wawakilishi waliokuwa wamebaki katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika timu ya Azam FC imeondolewa katika mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha bao moja kutoka kwa Triangle United ya Zimbabwe.

Kipigo hicho kinaifanya Azam kutupwa nje ya mashindano hayo kwa jumla ya mabao 2-0 kufuatia kipigo kama hicho ilichopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex.

Hii inamaanisha Azam itarejea kikamilifu katika michuano ya ndani ikielekeza nguvu kwenye ligi na FA ili kutafuta nafasi ya kurejea katika mashindano hayo mwakani.

Yanga ambayo imetolewa na Zesco katika michuano ya klabu bingwa Afrika kwa kufungwa mabao 2-1 ndio wataiwakilisha nchi katika Shirikisho Afrika.

#wapendasokaupdates

YANGA YASHINDWA KUPINDUA MEZA ZAMBIA, YATUPWA NJE NA ZESCO

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika timu ya Yanga imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zesco United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Levy Mwanawasa.

Yanga ambayo imeondolewa kwa jumla ya mabao 3-2 kufuatia sare ya 1-1 nyumbani itashuka chini kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.

Wenyeji Zesco walikuwa wakwanza kupata bao dakika ya 24 lililofungwa na Jesse Were kwa kichwa akimalizia mpira uliorushwa na mlinzi wa kulia Mwila Phiri.

Sadney Khoetage aliisawazishia Yanga bao hilo dakika ya 30 kwa shuti kali la mguu wa kushoto kufuatia mpira wa krosi uliopigwa na Deus Kaseke kupanguliwa na mlinda mlango Jacob Banda kabla ya kumkuta raia huyo wa Namibia.

Kipindi cha pili Zesco waliongeza kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga ambao muda mrefu walikuwa wakizuia huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 78 Zesco walipata bao la pili baada ya kiungo Abdulaziz Makame kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Umaru.

#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started