




CAF Confederation Cup :
First Round 2nd Leg :
Al Masry SC 🇪🇬 3-1 🇹🇿 Malindi SC (Agg 7-2)
[Ahmed Yasser 2X, Austin Amutu || Ebrahim Ali]
:
● Al Masry SC imefuzu hatua inayofuata itacheza playoff na vilabu vingine vilivyofuzu katika Kombe la shirikisho.
:
Hongereni @malindisports Msimu huu mmeonyesha ukomavu katika mashindano haya Mjipange tena mwakani.
:
#TotalCAFCC #sokaplaceupdates

CAF Champions League :
First Round 2nd Leg :
Gor Mahia FC 🇰🇪 0-2 🇩🇿 USM Alger (Agg 1-6)
[Aymen Mahious 2X]
:
■ Baada ya ushindi wa leo klabu ya USM Alger imetinga katika hatua ya Makundi klabu Bingwa barani Afrika.
:
Majirani zetu Gormahia wanaungana na klabu ya Yanga Sc katika kombe la shirikisho Barani afrika.
:
#TotalCAFCL#sokaplaceupdates

Hippos
[ 25’, 60’ Andrew Albart Simchimba, 88’, 90’ Kelvin Pius John | 46’, 74’ Abdul Aziz Kayondo ]
.
Eritrea 🇪🇷 5️⃣ – 0️⃣ Zanzibar
….
– Timu ya taifa ya Vijana ya Tanzania 🇹🇿 na vijana wa Eritrea 🇪🇷 wanafanikiwa Kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya Michuano ya vijana ya CECAFA U20 inayoendelea nchini Uganda 🇺🇬.. Timu zilizofuzu kucheza hatua hii ni Kenya 🇰🇪, Tanzania 🇹🇿, Eritrea 🇪🇷 na Sudan 🇸🇸.
#CECAFAU20ChallengeCupUganda2019 #CECAFAU20
@Harunlugoyah

– René Weiler raia wa Uswisi amekuwa kocha wa kwanza ambaye sio Raia wa Misri 🇪🇬 kuweka rekodi ya kushinda game zake Nne za mwanzo katika Klabu ya Al Ahly ya Nchini Misri tangu kocha Manuel José, Mreno huyo ni miongoni mwa makocha wenye heshima kubwa sana ndani ya Ahly, wao wanamuita Legendary wao.
….
– Rekodi nyingine za makocha wasio wazawa kuiongoza Ahly katika game Nne za Mwanzo..
Juan Carlos Garrido 🇪🇸
2W – 2L
José Peseiro 🇵🇹
2W – 1L
Martin Jol 🇳🇱
3W – 1D
Patrice Carteron 🇫🇷
3W – 1D
Martin Lasarte 🇺🇾
3W – 1D.
…
– Maneno na Vitendo, wakati anatambulishwa kuwa kocha mpya wa Ahly, René Weiler 🇨🇭 alitangaza hili balaa, kwamba yoyote anaekuja mbele ajipange na kombe lolote linalokuja mbele yao atahakikisha linatua ndani ya Klabu hiyo na tayari kombe Moja lumetua… Jana kocha huyo kawaongoza Mabingwa hao wa Kihistoria Afrika Kufuzu kucheza hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuitupa nje Klabu ya Cano Sport… Al Ahly jana ilishinda 4-0 nyumbani huko Borg El-Arab na ilishinda 2-0 mechi ya kwanza ugenini huko Equatorial Guinea.
#Alahly #CAFCL #TotalCAFCL
@Harunlugoyah

✍ Mpaka Sasa, vilabu vilivyofuzu kucheza hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika “CAF Champions League”..
Petro Atletico 🇦🇴
Mamelodi Sundowns 🇿🇦
Espérance de Tunis 🇹🇳
FC Platinum 🇿🇼
ZESCO United 🇿🇲
Al Ahly SC 🇪🇬
Raja Casablanca 🇲🇦
….
– Bado vilabu Tisa (9️⃣) kukamilisha idadi ya timu 16 ambazo itafanyika Droo ya kupanga Makundi Manne yenye timu Nne Kila Kundi… RATIBA ya game za hii leo.
Gor Mahia FC 🇰🇪 vs 🇩🇿 USM Alger (Agg 1-4)
TP Mazembe 🇨🇩 vs 🇲🇬 Fosa Juniors (Agg 0-0)
AS Vita Club 🇨🇩 vs 🇹🇬 ASC Kara (Agg 0-0)
Etoile Sahel 🇹🇳 vs 🇬🇭 Asante Kotoko SC (Agg 0-2)
Horoya AC 🇬🇳 vs 🇩🇿 JS Kabylie (Agg 0-2)
Primeiro de Agosto 🇦🇴 vs 🇿🇲 Green Eagles (Agg 2-1)
Al Hilal Club 🇸🇩 vs 🇳🇬 Enyimba Int’l FC (Agg 0-0)
Wydad AC 🇲🇦 vs 🇲🇷 FC Nouadhibou (Agg 2-0)
#TotalCAFCL #CAFCL
#SokaPlaceUpdates @Harunlugoyah

Gigi Buffon: 9️⃣0️⃣3⃣
Paolo Maldini: 9⃣0⃣2⃣
– Mlinda lango mkongwe, Gigi Buffon akiwa na umri wa miaka 41, ameweka rekodi mpya ya kucheza mechi yake ya 903 katika maisha yake.
…
– Kwa idadi ya game hizo Sasa, Buffon ndio Mchezaji Raia wa Italia 🇮🇹 ambaye kacheza mechi nyingi zaidi katika Historia… Buffon kaikuta na kuipita rekodi hiyo iliyokuwa inashikiriwa na beki wa zamani wa AC Milan, Paolo Maldini ambaye alicheza mechi 902.. 👏🇮🇹
…
– Jana, Buffon alikaa langoni mwa timu yake ya Juventus na kuisaidia kupata ushindi na clean sheets, 2-0 dhidi ya SPAL, Juve wakiendelea kuwakimbiza Inter Milan katika mbio za Ubingwa wa Serie A.
#SerieA #Juventus #SerieAUpdates
@Harunlugoyah

NILICHOKIONA NDOLA,ZAMBIA..
:
Na Octa ayubu jr..
:
Nyumbani ni nyumbani,na mcheza kwao hutunzwa.Sina maana kama Zesco kabebwa au kupendelewa na refa wa mchezo lahasha! Ila kitendo cha kucheza uwanja wa nyumbani ndicho kilichowabeba ila kiubora ni maeneo madogo tu ndipo walipowazidi Yanga.
:
Kuna siku niliandika kwamba shikalo lazima afanye kazi ya ziada kujihakikishia namba kikosi cha kwanza.kama wataangalia kigezo cha proffesional basi shikalo ataanza ila kiubora,mpaka sasa naweza kusema metacha ndiye golikipa namba moja wa yanga.Anakuwa bora kila mechi.
:
Tangu nimemfahamu ally ally nimemshuhudia akicheza pembeni akiwa yanga lakini inafahamika ni beki wa kati.Mapungufu yake yamekuwa yaleyale,mzito kufanya maamuzi,lakini anachoka mapema jambo linalofanya awatese wengine kwasababu kuna wakati zesco waligeuza upande wake kama barabara sio njia tena.
:
Ally Sonso,Naam huyu ndio sonso niliekuwa namsubili.akiwa lipuli alitumika kama kitasa na alikuwa bora,kwasasa anacheza beki wa pembeni bila shaka anawafanya wananchi wamsahau Gadiel michael mapema mno.
:
Huyu Lamine Moro ndio yule aliefeli majaribio upande wa pili? Anyway mimi na wewe hatujui kocha alikuwa anahitaji beki wa aina gani ila ni miongoni mwa beki bora VPL kwasasa.pacha yake na Yondan itaibeba Yanga kwasasa.
:
Football, Naam huu ndio mchezo uliokosa usawa, unaweza kuufanyia kila unachoweza lakini bado ukaharibu.Abdulaziz makame,hii ndio Engine ya timu licha ya kujifunga huyu ndio Man of the match kwangu.Alikuwa bora sana na hakika atawasaidia yanga.
:
Deus kaseke,utu uzima dawa, ndivyo unavyoweza kumzungumzia kaseke.Amejitahidi japo ni ngumu kuufikia ubora aliokuwa nao huko nyuma.
:
Fei toto,huyu ni kiungo bora ndani ya yanga kwasasa hususani kwenye eneo la kuchezesha.Partinership yake na Abdulaziz makame ilikuwa bora bahati mbaya zaidi kwao walikutana na mtu anaewajua mno ndio maana Kamusoka aliwawin.
:
Sadney,movement zake ni nzuri na hatari kwa mpinzani ila bado sio mchezaji anaeweza kuibeba timu katika wakati mgumu.lakini pia linapokuja suala la kufunga bado amekuwa hana uwezo mzuri wakupiga.
:
Tshishimbi,Siwezi kumlaumu ila nafikili eneo alilotumika liligeuka mzigo kwake.movement zake nyingi zilikuwa na faida kwa zesco kuliko Yanga.
:
Patrick Sibomana,Kama walimuacha kusubuli penati sawa,lakini kisoka mpira Leo PS ulimkataa na huyu nilitegemewa angefanyiwa sub mapema kala hata makame hajajifunga.
:
Inawezekana kweli kamsoko akawa mzee kwetu,lakini kwa wenzetu wanaoweza kutunza na kumhudumia wakamfaidi miaka miwili mpaka mitatu Ijayo.
:
Yanga ametolewa klabu bingwa lakini kuna nafasi nyingine ya kufanyia marekebisho makosa tuliyoyaona kwenye klabu bingwa.Ila kama hawatabadilika katika baadhi ya maeneo hususani eneo LA ushambuliaji basi hata mechi ya playoff kuelekea makundi kombe la shirikisho bado itakuwa ngumu. ✍🏻 @octa_ayubu_jr
#sokaplaceupdates

:
#VodacomPremierLeague
16:00 KMC FC vs Ndanda FC
16:00 Mtibwa Sugar vs Mbeya City
16:00 Biashara United vs Simba Sc
16:00 Lipuli Fc vs Tanzania Prison
16:00 Kagera Sugar vs Jkt Tanzania
:
#EnglandPremierLeague
18:30 Leicester City vs Newcastle United
:
#SpainLaLigaSantander
13:00 RCD Espanyol vs Real Valladolid
15:00 Eibar vs Celta Vigo
17:00 Deportivo Alaves vs Mallorca
19:30 Levante vs Osasuna
22:00 Sevilla vs Real Sociedad
:
#ItalySerieA
13:30 Napoli vs Brescia
16:00 Lazio vs Genoa
16:00 Lecce vs Roma
16:00 Udinese vs Bologna
19:00 Cagliari vs Verona
21:45 Milan vs Fiorentina
:
#GermanyBundesliga
16:30 Fortuna vs Freiburg
19:00 FC Köln vs Hertha BSC
:
#FranceLigue1
16:00 Strasbourg vs Montpellier
18:00 Nimes vs Saint-Etienne
22:00 Marseille vs Rennes
:
#NetherlandsEredivisie
13:15 RKC Waalwijk vs Vitesse
15:30 FC Utrecht vs Willem II
15:30 PEC Zwolle vs PSV Eindhoven
17:45 AZ Alkmaar vs Heracles
17:45 Feyenoord vs FC Twente
:
#BelgiumFirstDivisionA
15:30 Anderlecht vs Waasland-Beveren
19:00 Standard Liege vs Sporting Charleroi
21:00 Oostende vs Royal Antwerp
:
#AfricaChampionsLeague
16:00 Gor Mahia vs USM Alger
16:30 TP Mazembe vs SOM Fosa Juniors FC
17:30 AS Vita Club vs Kara
19:00 Etoile du Sahel vs Asante Kotoko
19:00 Horoya vs JS Kabylie
19:00 Primeiro de Agosto vs Green Eagles FC
20:30 Al Hilal Omdurman vs Enyimba International FC
22:00 Wydad de Casablanca vs Nouadhibou
:
#AfricaConfederationsCup
17:30 Ben Guerdane vs Bandari
18:00 Enugu Rangers vs Pelican
19:00 Djoliba AC Bamako vs Maranatha Fiokpo
19:00 FC San Pedro vs Santoba
19:45 CR Belouizdad vs Pyramids FC
20:00 CS Sfaxien vs Paradou AC
:
#KenyaPremierLeague
15:00 AFC Leopards vs Chemelil Sugar
15:00 KCB vs Kakamega Homeboyz
15:00 Zoo FC vs Wazito FC
:
#MoroccoBotolaPro
18:00 Rapide Club Oued Zem vs OCK Khouribga
20:00 MAT Tetouan vs Renaissance Club Zemamra
:
#SouthAfricaPremierLeague
16:00 Black Leopards vs Bloemfontein Celtic
16:00 Highlands Park FC vs Polokwane City
Imeandaliwa na @officialchristz wa @sokaplace__

