Nkana FC yasgambuliwa na mashabiki baada ya kutolewa klabu bingwa

– Wachezaji wa Klabu ya Nkana FC ya Zambia 🇿🇲 wakijificha kukwepa kupigwa mawe pamoja na Chupa za Bia kutoka kwa Mashabiki wao waliokasirishwa na kitendo cha timu hiyo kufungwa bao 1-0 na klabu ya Forest Rangers katika mchezo wa Ligi Kuu Nchini Humo..

– Huu ni Mchezo wa Pili kupoteza kwa Nkana msimu huu katika Game zao Nne na mbili nyingine wakiibuka na Ushindi wakikamata nafasi ya nane katika Msimamo wa Ligi yao..
#NkanaFC #ZambianSuperLeague
@Harunlugoyah

ZAHERA AFUNGUKA KUHUSU JUMA ABDUL KUSUGUA BENCHI DHIDI YA ZESCO

Baada ya malalamiko ya wadau wengi wa soka juu ya sababu ya mlinzi wa kulia wa Yanga, Juma Abdul kutocheza katika mchezo wa marudiano wa mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Zesco waliolala kwa mabao 2-1 mjini Ndola siku ya Jumamosi.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera amesema alishindwa kumtumia mlinzi huyo kutokana na kushindwa kupata muda mwingi wa kucheza kipindi kirefu.

Rai huyo wa DR Congo amesema katika kupindi cha mwaka mmoja Abdul amecheza dakika 10 tu hivyo ndio maana hakumpa nafasi badala yake akampanga Ally Ally upande wa kulia. “Juma Abdul katika mwaka mmoja amecheza dakika 10 pekee kule Moshi kwahiyo nisingeweza kumtumia katika mchezo mgumu wenye kutoa maamuzi,” alisema Zahera.

Msimu mzima uliopita Juma alishindwa kupata namba mbele ya Paul Godfrey ‘Boxer’ ambaye alikuwa kwenye kiwango bora lakini kwa sasa nyota huyo ni majeruhi.

#wapendasokaupdates

Luis Suarez…afikisha goli 400…tangu aanze soka

Mshambuliaji wa FC Barcelona, Luis Suarez Sasa kafikisha idadi ya Magoli 400 katika Mashindano yote kwenye maisha yake akicheza ngazi ya vilabu.
🇺🇾 Nacional (12)
🇳🇱 Groningen (15)
🇳🇱 Ajax (111)
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Liverpool (82)
🇪🇸 Barcelona (180)
#fcbarcelona #LuisSuarez #liverpool

Droo ya hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika…kufanyika octoba 8

OFFICIAL | Droo ya hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika “CAF Champions League” na Raundi ya Mtoano “Play-off” ya Kombe la Shirikisho Afrika “CAF Confederation Cup” rasmi itafanyika Siku ya Jumatano October 08, 2019, huko Hilton Pyramids Resort mjini Cairo, nchini Misri 🇪🇬… Muda ni Saa 20:00 EAT.
#TotalCAFCL #TotalCAFCC
@Harunlugoyah

Salim kikeke kuwa balozi wa simba sc jijini lonson

Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba SC chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mohammed Dewji imetangaza kumteua Mtangazaji wa BBC, Ndg. Salim Kikeke kuwa Balozi wa klabu ya Simba Sports Club katika mji wa London, Uingereza… MO Dewji amesema kuwa anaamini kwamba Kikeke ataipeperusha vyema bendera ya Simba..
#SimbaSC #Updates

JOSE MOURINHO: Eto’o ni mchezaji wa kipekee…


– Mchezaji huyo wa zamani wa Everton na Chelsea ni miongoni mwa wachezaji wa Afrika akiwemo Didier Drogba, Michael Essien na John Obi Mikel ambao walitia fora chini ya ukufunzi wa Jose Mourinho lakini ‘The Special One’ anaamini kwamba nahodha huyo wa zamani wa Cameroon alikuwa mchezaji tofauti.
.
– Kipindi cha mchezo, Samuel Eto’o alikuwa na kitu muhimu kama mchezaji akiwa na mchango wake katika timu yake kupata ushindi.. Alikuwa akitumia kila njia timu yake kuweza kupata ushindi. Samuel alikuwa mchezaji aliyekuwa na kipaji lakini alishirikiana sana na wenzake. Alishinda mataji yote muhimu..
🗣 ”Akiichezea Inter tulicheza dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya ligi ya mabingwa, tulikuwa na wachezaji 10 na Eto’o alicheza mechi yote akiwa beki wa kulia. Alijitolea na kucheza katika safu hiyo ili kuhakikisha kuwa tunapata ushindi. Hicho ndio ambacho timu ilihitaji wakati huo”.
.
🗣 ”Mjini Milan tulikuwa tumeshinda magoli 3-1, tulipokuwa tukielekea Camp Nou, hatukuhitaji kufunga, tulihitaji kutinga fainali na alielewa hilo, Alifanya kila kilichohitajika kwa timu kufuzu fainali. Hii ni tabia nzuri kwa binadamu na nina hakika Eto’o atafanikiwa baada ya kustaafu”. Alisema Jose Mourinho
.
– Samuel Eto’o alichezea klabu 13 katika mataifa sita na kufunga jumla ya magoli 56 katika mechi 118 akiichezea Cameroon Kipindi chake akicheza soka… Sasa hivi Amesema kwamba anachukua likizo ya soka ili kuwa karibu na familia na kufikiria kuhusu maisha yake ya baadaye..
#SamuelEtoo #joseMourinho #Updates

Mechi ya Zamalek vs Generation Foot ya Senegal 🇸🇳. ..yashinda chezeka.

– Shirikisho la Mpira wa miguu Barani Afrika, CAF limesema kwamba linafuatilia kwa ukaribu sana, kufuatia mchezo wa Mkondo wa pili wa klabu Bingwa Afrika kushindwa kufanyika, game hiyo ni kati ya Wenyeji Zamalek ya Misri dhidi Generation Foot ya Senegal 🇸🇳.

– Taarifa kutoka CAF jioni ya jana Jumapili ilitolewa na kusema kwamba “CAF imekuwa ikifuatilia kwa Ukaribu hali ya kuhusu mechi ya Mkondo wa pili ya Raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20, kati ya Zamalek (Egypt) na Generation Foot (Senegal), ambayo ilitakiwa ifanyike mwishoni mwa wiki”… “Baraza na Wawakilishi wa CAF wanachunguza hali hii na habari zaidi zitatolewa kwa wakati muhafaka”. Sehemu ya Taarifa hiyo ilisomeka.
….
– Klabu hiyo ya nchini Senegal 🇸🇳, Génération Foot ilikataa kucheza mechi ya Marudiano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Zamalek kwenye uwanja wa Borg Al Arab huko jijini Alexandria jana Jumapili… Game hiyo Awali ilitakiwa ifanyike juzi Jumamosi kwenye uwanja wa Petrosport huko Jijini Cairo..
..
– Klabu hiyo iliambiwa na Shirikisho la Soka Afrika “CAF” Masaa 24 tu kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwamba mchezo wao utaahirishwa na uwanja pia Utabadilishwa, jambo ambalo lilizua hasira kwa viongozi wa klabu na kuamua kutocheza game hiyo.. Mpaka Sasa hakuna uamuzi uliotolewa na CAF Mpaka Bodi hiyo itakapokutana.
#CAFCL #TotalCAFCL
@Harunlugoyah

MATOKEO YA SOKA JANA

#VodacomPrimierLeague
FTKagera Sugar 0-1 JKT Tanzania
FTKMC 1-1 Ndanda SC
FTBiashara United 0-2 Simba SC
FTMtibwa Sugar 1-1 Mbeya City
FTLipuli FC 2-2 TZ Prisons
:
#CECAFAU20 @sokaplace_
FT Uganda 2-4 Tanzania
:
#EnglandPremierLeague
FT Leicester City 5 – 0 Newcastle United
:
#SpainLaLigaSantander
FT RCD Espanyol 0 – 2 Real Valladolid
FT Eibar 2 – 0 Celta Vigo
FT Deportivo Alaves 2 – 0 Mallorca
FT Levante 1 – 1 Osasuna
FT Sevilla 3 – 2 Real Sociedad
:
#ItalySerieA @sokaplace_
FT Napoli 2 – 1 Brescia
FT Lazio 4 – 0 Genoa
FT Lecce 0 – 1 Roma
FT Udinese 1 – 0 Bologna
FT Cagliari 1 – 1 Verona
FT Milan 1 – 3 Fiorentina
:
#GermanyBundesliga
FT Fortuna Düsseldorf 1 – 2 Freiburg
FT FC Köln 0 – 4 Hertha BSC
:
#FranceLigue1@sokaplace_
FT Strasbourg 1 – 0 Montpellier
FT Nimes 0 – 1 Saint-Etienne
FT Marseille 1 – 1 Rennes
:
#NetherlandsEredivisie
FT RKC Waalwijk 1 – 2 Vitesse
FT FC Utrecht 2 – 0 Willem II
FT PEC Zwolle 0 – 4 PSV Eindhoven
FT AZ Alkmaar 2 – 0 Heracles
FT Feyenoord 5 – 1 FC Twente
:
#BelgiumFirstDivisionA @sokaplace_
FT Anderlecht 0 – 0 Waasland-Beveren
FT Standard Liege 1 – 1 Sporting Charleroi
FT Oostende 1 – 1 Royal Antwerp
:
#AfricaChampionsLeague
FT Gor Mahia 0 – 2 USM Alger
FT TP Mazembe 3 – 1 SOM Fosa Juniors FC
FT AS Vita Club 1 – 0 Kara
FT Etoile du Sahel 3 – 0 Asante Kotoko
FT Horoya 2 – 0 JS Kabylie *
FT Primeiro de Agosto 0 – 1 Green Eagles
FT Al Hilal Omdurman 1 – 0 Enyimba
FT Wydad de Casablanca 4 – 1 Nouadhibou
:
#AfricaConfederationsCup @sokaplace_
FT Al Masry 3 – 1 Malindi FC
FT Ben Guerdane 2 – 1 Bandari
FT Enugu Rangers 3 – 1 Pelican
FT AC Bamako 1 – 1 Maranatha Fiokpo
FT FC San Pedro 3 – 0 Santoba
FT CR Belouizdad 0 – 1 Pyramids FC
FT CS Sfaxien 0 – 0 Paradou AC
:
#KenyaPremierLeague
FT AFC Leopards 4 – 0 Chemelil Sugar
FT KCB 2 – 1 Kakamega Homeboyz
FT Zoo FC 0 – 2 Wazito FC
:
#MoroccoBotolaPro @sokaplace_
FT Rapide Club Oued Zem 0 – 1 OCK Khouribga
FT MAT Tetouan 1 – 0 Renaissance Club Zemamra
:
#SouthAfricaPremierLeague
FT Black Leopards 1 – 0 Bloemfontein Celtic
FT Highlands Park FC 2 – 0 Polokwane City

Design a site like this with WordPress.com
Get started