Tottenham kwa mara ya kwanza yaruhusu kupoteza 7-2 nyumbani

7 – Tottenham Hotspur wameruhusu Kufungwa mabao saba katika mechi ya nyumbani kwa mara ya kwanza kwenye mashindano yoyote makubwa..

7 – Tottenham Hotspur ndio klabu ya kwanza ya Kiingereza kufungwa mabao saba katika mashindano yoyote ya Ulaya, Mara ya mwisho walifungwa wao wenyewe Tottenham walipo poteza 0-8 kutoka FC Koln kwenye mchezo wa UEFA Intertoto Cup mnamo Julai 1995 ..

5 – Kipigo cha Magoli 2-7 walichopata Tottenham kutoka kwa Bayern Munich ndio kipigo kikubwa zaidi inapokea timu ya Kiingereza nyumbani kwenye mashindano yoyote ya Ulaya.
#tottenham #UEFAChampionsLeague
@Harunlugoyah

Lewandowski kawa mchezaji wa 6 kufunga mechi 40 UEFA

– Robert Lewandowski amekuwa mchezaji wa sita kufunga katika mechi 40 tofauti za Ligi ya Mabingwa… Orodha kamili ya Wachezaji hao waliofunga katika game 40+ tofauti.
πŸ‡΅πŸ‡Ή Cristiano Ronaldo (82)
πŸ‡¦πŸ‡· Lionel Messi (68)
πŸ‡ͺπŸ‡Έ RaΓΊl (56)
πŸ‡«πŸ‡· Karim Benzema (45)
πŸ‡³πŸ‡± Ruud van Nistelrooy (42)
πŸ‡΅πŸ‡± Robert Lewandowski (40)
#ChampionsLeague
@Harunlugoyah

SHAFFIH DAUDA APATA SHAVU STARTIMES

Kampuni ya Star Media Limited kupitia chapa yake ya Startimes imeingia makubaliano ya ushirikiano na mtangazaji nguli wa michezo nchini Shaffih Dauda na inakuwa mara ya pili kufanya hivyo.

Startimes ambayo inarusha michuano ya Europa inayoendelea pamoja na michuano ya Euro2020 imeingia makubaliano hayo na Mtangazaji huyo nguli kutokana na umahili wake pamoja na mvuto kwenye jamii.

Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa amesema kwa sasa michuano ya Europa ambayo ni ya pili kwa ukubwa barani Ulaya inayofanyika siku ya Alhamisi imekuwa na mvuto mkubwa kutokana na aina ya timu zinazoshiriki ndio maana wameamua kuirusha kupitia chanel yao.

Malisa amesema ili kufaidi uhondo huo ndani ya ‘Wababe wa Burudani’ utalipia kifurushi cha Uhuru shilingi 18,000 kwa wanaotumia antena na shilingi 21,000 kwa wanaotumia Dish kwa kifurushi cha Smart.

@shaffihdauda_ @startimestz
#wapendasokaupdates

Orodha ya timu zilizoingia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika:

CAF Champions league | Orodha ya timu zilizoingia hatua ya makundi klabu bingwa Afrika:

ZESCO United πŸ‡ΏπŸ‡²
Primeiro de Agosto πŸ‡¦πŸ‡΄
Petro Atletico πŸ‡¦πŸ‡΄
Mamelodi Sundowns πŸ‡ΏπŸ‡¦
Etoile Sahel πŸ‡ΉπŸ‡³
EspΓ©rance Tunis πŸ‡ΉπŸ‡³
FC Platinum πŸ‡ΏπŸ‡Ό
Al Ahly SC πŸ‡ͺπŸ‡¬
Wydad AC πŸ‡²πŸ‡¦
Raja CA πŸ‡²πŸ‡¦
TP Mazembe πŸ‡¨πŸ‡©
AS Vita Club πŸ‡¨πŸ‡©
JS Kabylie πŸ‡©πŸ‡Ώ
USM Alger πŸ‡©πŸ‡Ώ
Al Hilal Club πŸ‡ΈπŸ‡©
β€’
*Zamalek / Generation Foot mchezo aukuchezwa, unasubilia maamuzi kutoka CAF)

Droo ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika na Raundi ya Mtoano ya Kombela Shirikisho Afrika itafanyika wiki ijayo Oktoba 9, mjini Cairo.

Manchester united kuhitaji muda ili kurudi katika ubora wake

Mashabiki wengi wa Manchester United ni kama hawaelewi hivi ni tatizo gani linaisumbua timu yao kwa sababu kama ni makocha wamekuja wengi na kuondoka, wachezaji vilevile lakini Man United bado ipo vilevile.

Mchezaji wa zamani wa vilabu kadhaa vya Tanzania na timu ya taifa @amrikiembatz yeye anasema, Manchester United inahitaji muda ili kurudi kwenye maisha yake ya zamani.

Manchester United ilifanya vizuri sana miaka ya nyuma, sasa watu bado wanaishi kwenye miaka ile. Kwa hiyo kila mchezaji anayekuja anabebeshwa jukumu la miaka hiyo wakati anatakiwa apewe muda wa kutengeneza kama ilivyokuwa kwa waliopita ambao walipewa muda wakafanya walivyofanya.

Ukiangalia Sir Alex Ferguson hadi anakuja kufanikiwa alipewa muda na akapambana na wachezaji wake lakini leo kumbebesha Martial jukumu ambalo anafanya Ronaldo sasa hivi ni kumuumiza na kumuondoa kwenye kucheza.

Manchester United kwa timu iliyopo sasa hivi (wachezaji) ni sawa na vilabu vingine vya kawaida pale England (ndani ya uwanja) ukiacha ukubwa wa jina la timu nje ya uwanja.

Leo hii Rashford angekuwa Everton anaweza kumaliza ligi akiwa na magoli 17 hadi 20 lakini kuwa pale Manchester United anashindwa kufanya hivyo kwa sababu ya presha timu.

Manchester United inahitaji kuvumilia kwa kipindi fulani kipite, hawawezi kufanikiwa kirahisi kwa kubadilisha makocha na wachezaji. Ni sawa na moto unawaka chini halafu mtu anakuja kuufunika juu halafu hataki moshi utoke juu.

Leo usiku ni Manchester United vs Arsenal, ukitembelea @mbet.co.tz United wana 2.27 wakati Gunners wana 2.99 kwenye mkeka wako wa umempa nani?

#Mbet #NyumbaYaMabingwa

Uganda yatangaza kocha mpya timu ya taifa

OFFICIAL | Shirikisho la Soka nchini Uganda “FUFA”, Limethibitisha na kumtangaza, Johnathan McKinstry kuwa kocha mkuu wa timu yao ya taifa ya Uganda Cranes πŸ‡ΊπŸ‡¬. Kocha huyo kijana kabisa mwenye umri wa miaka 34 Raia wa Ireland Kaskazini πŸ‡¬πŸ‡§ Amesaini Mkataba wa miaka Mitatu kuiongoza Uganda Cranes.

– Mwaka 2013, McKinstry aliteuliwa kama kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Sierra Leone πŸ‡ΈπŸ‡± ambapo aliwaongoza kufika katika nafasi yao bora zaidi ya juu kabisa ya FIFA Ranking… Mwaka 2015 aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Rwanda πŸ‡·πŸ‡Ό, akiwaongoza Amavubi kwenye Fainali ya Kombe la CECAFA 2015 wakipoteza mbele ya Uganda na Aliisaidia kufika Robo ya Mashindano ya CHAN 2016 wakiwa wenyeji wakipoteza mbele ya Waliokuwa Mabingwa DR Congo πŸ‡¨πŸ‡©, na Pia amekuwa kocha mkuu wa vilabu, Kauno Ε½algiris ya Lithuania πŸ‡±πŸ‡Ή na Kabla ya Sasa katoka kuwa kocha mkuu wa klabu ya Saif FC ya huko Bangladeshi πŸ‡§πŸ‡©.

– Mnamo Desemba 2017 McKinstry aliorodheshwa Shirikisho la Soka nchini Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬ kuwania nafasi ya meneja wa timu yao ya taifa lakini alikosa, na mnamo Aprili 2018 alikuwa mmoja wa waombaji 77 wa timu ya taifa ya Cameroon πŸ‡¨πŸ‡² Pia alikosa, Ilithibitishwa pia na maafisa wa Chama cha Soka cha Zambia mnamo Juni 2018 kwamba McKinstry alikuwa ni mmojawapo katika orodha ya mwisho ya wagombeaji wawili waliowamia kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Zambia πŸ‡ΏπŸ‡² “Chipolopolo” Pia alikosa.. Mwaka huu kafanikiwa kupata Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬ ambako mwanzo aliwahi kukosa πŸ™ŒπŸ»πŸ‘πŸ»πŸ‘πŸ».
#transfersUpdates #UgandaCranes
@Harunlugoyah

Design a site like this with WordPress.com
Get started