Takwimu za kundi A ligi daraja la kwanza baada ya kila timu kucheza michezo 13 •

Dodoma fc nafasi ya kwanza na Ihefu nafasi ya 2 wote wamecheza michezo 13 wamefanana kila kitu wote wana alama 27 pia wote wana goal difference ya goli 9 hapa atakaye poteza mchezo wowote ujao atakuwa amemtengeneza mazingira mazuri mpinzani wake

Mbeyakwanza wako nafasi ya 3 mechi 13 alama 25 bado wako kwenye hatua nzuri kikubwa hawataki kupoteza tena mchezo wowote kuanzia sasa, walifanya baadhi ya sajili muhimu ukiwepo usajili wa mkongwe Dany Mrwanda ambaye tangu asajiliwe amecheza mechi 3 na kufunga goli 3 🙌

“Wanalizombe” Majimaji fc nafasi ya 4 hali sio shwali alama 22 michezo 13 katika harakati za kuwania kupanda daraja bado hawako kwenye nafasi nzuri sana, wao ni wazoefu na wakongwe ukilinganisha na baadhi ya timu ambazo zinafanya vizuri kwenye kundi lao kama Ihefu fc

African Lyon alama 21 michezo 13 nafasi ya 5 bado jitihada zinahitajika

Friends Rangers michezo 13 alama 18 nafasi ya 6 Mambo bado

Njombe mji nafasi ya 7 mambo bado magumu hawajawa na mwenendo mzuri tangu washuke daraja michezo 13 alama 17 wajipange msimu ujao

Boma fc walianza vizuri lakini kadri siku zinavyozidi kwenda moto unakata nafasi ya 8 hivi sasa michezo 13 alama 16

Cosmopolitan alama 13 baada ya kucheza michezo 13 Wana wastani wa kupata alama 1 kwenye kila mchezo nafasi ya 9

Iringa United hali mbaya ya kiuchumi ina waathiri wako nafasi ya 10 hivi Sasa michezo 13 alama 10 wameshinda mchezo mmoja pekee

Maafande wa Jkt Mlale hali sio hali nafasi ya 11 michezo 13 alama 8

Pan African nafasi ya 13 nao wanahitaji nguvu ya ziada michezo 13 alama 7 wana buruza mkia

Mpaka sasa kwenye kundi hili Dodoma fc na Ihefu fc kila timu inaweza kumaliza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na kupanda moja kwa moja bila kucheza play off

Mbeya Kwanza pia wako kwenye nafasi nzuri endapo watashunda michezo yao yote ikiyobaki

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Takwimu za kundi B ligi daraja la kwanza baada ya kila timu kucheza michezo 13


Gwambina fc nafasi ya kwanza michezo 13 alama 25 mwendo mzuri maandalizi mazuri na uwekezaji, hakika wanastahili kuwa hapa awalisajili baadhi ya wachezaji wakongwe waliocheza ligi kuu kwa muda mrefu akiwepo Jacob Masawe, Kelvin Kongwe Sabato wa Mtibwa Sugar ingawa baadae aliondoka akajiunga na Kagera Sugar

Wachimba madini Geita Gold nafasi ya pili michezo 13 alama 22 wakiwa sawa na Arusha fc ambao pia wana alama 22 wakiwa nafasi ya 3, unaweza sema hawa ndio wapinzani sahihi wa Gwambina fc kwenye kundi hili

Gipco fc nafasi ya 4 na Rhino Rangers nafasi ya 5 wote wana alama 19 baada ya kucheza michezo 13

Mashujaa fc 😅 nafasi ya 6 michezo 13 alama 18

Mawenzi Market ya Morogoro nafasi ya 7 michezo 13 alama 17

Stand United “Chama la Wana” hali sio shwali sana alama 16 baada ya kushuka dimbani mara 13 nafasi ya 8… wapande au waendee kusubiri huku FDL😂

Transit Camp nafasi ya 9 michezo 13 alama 14

Nafasi ya 10 ni Sahare All Stars ya Tanga walianza vizuri lakini mambo yanazidi kuwa magumu michezo 13 alama 13 wako sawa na Pamba fc iliyokuwa ikifundishwa na Fred Felix Minziro wote wana wastani wa kupata alama 1 kwenye kila mchezo

Green Warriors 😅 Kumbe zilikuwa mbwembwe tuu wanaburuza mkia kundi B wakiwa na alama 11 baada ya kucheza michezo 13

Gwambina fc, Geita Gold na Gipco fc na Rhino Rangers wako Kwenye mazingira mazuri ya kupanda daraja msimu ujao

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

NDANDA KUCHELE INARUDI KWA HALI MPYA KATIKA HARAKATI ZA KUTOKA MSTARI WA KUSHUKA DARAJA

LEO 05/02/2020
NDANDA VS MBAO FC
saa 10:00 jioni kiingilio
Tsh 3000 NANGWANDA SIJAONA

Klabu ya NDANDA kuchele baada ya kuanza msimu wa Vpl 19/2020 kwa kusuasua,sasa wanamtwara wameungana pamoja kuiunga mkono kwa hali na Mali kuhakikisha wanaiondoa Timu katika ENEO hatari LA kushuka DARAJA Wanamtwara wamehamasika kuiunga mkono Klabu yao kwakile wanachosema TIMU YETU MKOA WETU UWANJA WETU POINT 3 ZETU
KUONGEZWA KWA vitalis mayanga katika safu ya ushambuliaji imeongeza hamasa kwa mashabiki wa NDANDA kuipenda Timu yao kwakua wanaamini Tatizo LA ufungaji limepatiwa MATIBABU YAKE
KAULI YA wanamtwara wanasema NDANDA HAISHUKI DARAJA NA ITAMALIZA NAFASI 10 ZA JUUU VPL

UTAMU WA DAKIKA 90 SIMBA DHIDI YA POLISI TANZANIA.

Prepared by @stevenjema_268

What a Match?? Mchezo wenye Hadhi Ya Premier, Kwa Viwango Vya Timu zote mbili hivi Karibuni (Current performance) nilitegemea kuuona mchezo kama uliionekana.
.
.
Mwalimu Sven na 4-2-3-1 yake bado Anashida kubwa sana Kwenye kipindi cha mpito kutoka kushambulia kwenda kulinda (Transition From Offence to Defence) Na kiufundi mfumo huu Kwenye Kulinda unakuwa na umbo La 4-5-1 lakini ukiangalia Simba inakuwa na 3-3-4.
.
Simba wanaposhambulia wanakuwa wanakuwa na 3-1-5-1 ili kuwapa nafasi viungo wa chini ku-win Second Balls na ndo maana tunaona Mkude na Fraga wanafunga sana Chini ya Sven, Hii inaacha mashimo mengi kwa wapinzan ,, Angalia Jinsi Polisi Tanzania walipokuwa wakipata mpira walikuwa na Option nyingi sana za kutengeneza mashambulizi.
.
Malale Hamsini!! What a game plan?? Japo amepoteza Huyu bwana anajua kufundisha Soka safii, Timu inatengeneza mashambulizi kutoka nyuma kwa pasi fupifupi za haraka, Footwork Nzuri sanaa ,, inaonekana Timu iliandaliwa haswaa kabla ya Mchezo.
.
Mwalimu Malale alijua Simba wana mawinga Ambao sio natural Wingers Hivyo hawawezi kuongeza Width pembeni , Akaja na Plan ya kuwazuia Simba eneo La kati ambalo ndio Hatari sana, Akamwanzisha Pato Ngonyani Ambae sio Typical Midfielder Amkabie Hassan Maulid,, Na first Half Simba wakazidiwa sana eneo La Kati na kuifanya timu ishindwe kuwa na Plan B kwasababu Pembeni hawana watu wa Kuongeza Width.
.
Pacha ya Tairone Na Kennedy Juma ilikuwa na makosa mengi sanafikili ni kwasababu hawajacheza wote muda mwingi.
.
Marcel Kaheza Na Jimmy Shoji wamecheza kwa kiwango cha juu sana , wanakimbia Wide na kuja chini kukaba,, Shamte ameteswa haswaa na Jimmy Shoji na ndo upende ambao ulikuwa na Hatari sana 🔥🔥.
.
Utulivu wa Safu ya ulinzi ya Mwalimu Malale hamsini ni wa hatari mnoo, Japo wamepoteza lakini Mohamed Khasim na Iddy Moby, Lucian, walikuwa na Nidhamu ya hali ya juu sana ya ukabaji.
.
Kama ningepata nafasi ya kumshauri Malale Hamsini baada ya First Half, Ngemshauri Acheze Dakika 15 za mwanzo then abaki nyuma awasubiri waje afanye Counter Pressing

Prepared by @stevenjema_268
Powered by @sports_lady_tz

ITIKADI ZETU ZIMETAFUNA DHAMIRI ZETU

NaJunior wa Pastor

Tabia ni urithi hasa kwa nchi zetu za kiafrika , si ajabu kusikia tabia za Wagogo , wasukuma ,wazaramo japo hujawahi kuishi nao na hata ukipokea mtu wa kabila hilo utaamini fika tabia zake ni zile ulizozisikia awali.

Nchini kwetu wapenzi wa soka ni wachache ukilinganisha na wapenzi wa simba na yanga , watu wengi walianza kupenda timu kabla ya mpira na hata katika siasa kuna ukawa na wale wa chama tawala hii ni kutokana na nchi yetu kuishi kwa itikadi zaidi na zikawa tabia na utamaduni wetu.

Ni rahisi kusikia Simba au Yanga kapewa ushindi au kaonewa lakini ni ngumu kusikia Majimaji kaonewa wakati akicheza na Ndanda , hii inatokana na watu kutazama na kupenda timu kuliko mpira wenyewe.

Haki inapotea kwa sababu ya itikadi tafsiri za sheria zinapotoshwa kwa sababu ya itikadi , likitokea Simba Yanga wanalibeba kama kesi ya mauaji hata Simba nao vile vile , sauti zinakuwa tofauti hata kwa viongozi , na waamuzi nao wamesahau majukumu yao kwa sababu ya itikadi .

Dhamiri haipati hatia kuharibu soka kwa kuvunja sheria ili timu ifaidike , hata katika yale ya waziwazi , kuna siku Yanga walishangilia goli la kupitia mkono wa Tambwe lakini kuna siku simba wanafurahia magoli ya offside hii ndio Tanzania bana.

Ushindani unapotea na soka linadidimia zaidi , kwa sababu dhamiri zetu haziko hai , tambua ukimaliza kupewa ushindi zamu yako ikiisha utakumbuka ubaya ukihamia kwako Maisha yanavyoendelea.

itikadi zimetafuna dhamiri zetu wakati yanatokea hatuutazami dhamana na nafasi zetu tunatazama timu , huwezi kuishi katika neema na nafasi ile ile milele na zama zikipita zimepita maandalizi yakubadili taswira ni kipindi cha Neema.

Itikadi zimetafuna dhamira za viongozi wetu , unaisahau vipi Yanga uikumbuke Mbao na Mwadui tatizo sio kiti tatizo ni itikadi , tunapaswa kuupenda mpira ili haki itakapokosekana ukweli usemwe kwa pamoja hata katika kamati tunazotegemea zidai haki kuna itikadi ndani yake.

Leo ataumia simba kesho Yanga lakini tukumbuke wakati hawa wakisikika kudai haki kuna wengine kule chini kuonewa ni Maisha yao miaka yote , mpira hauwezi kuwa bora mbele ya Itikadi zinazofanya timu kuwa bora kuliko mpira milele.

Lionel Messi amemshukia mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Eric Abidal

Nyota wa Barcelona Lionel Messi amemshukia mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Eric Abidal (ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Barcelona) kufuatia kauli yake kuwa wachezaji wa Barca walikua hawajitumi chini ya kocha Ernesto Valverde.

Messi amesema kama kauli hiyo ya Abidal ni kweli basi bosi huyo anapaswa kutaja majina ya wachezaji hao ambao walikua hawajitumi vinginevyo atakua anawakosea heshima wachezaji wote wa klabu hiyo.

#wapendasokaupdates

Tetesi za soka ulaya Leo jumatano 05.02.2020

Jack Grealish (kulia) alichezea timu ya Jamuhuri ya Ireland kwa vijana wa U 17,U 18 na U 21 kabla ya kuchaguz kuiwakilisha England

Manchester United wanajiandaa kutoa dau nono ili kumsajili kiungo wa England na Aston Villa Jack Grealish, 24, mwishoni mwa msimu. (Mirror)United wanamtaka Grealish kutokana na uwezekano mkubwa kwa chaguo lao la awali James Maddison, 23, kukaribia kusaini mkataba mpya na Leicester City. (Mirror) Klabu ya Chelsea inajipanga kumpa kocha Frank Lampard kitita cha pauni milioni 150 ili kumsajili mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembele, 23. (Evening Standard) Paul Pogba,26, amewaambia wachezaji wenzake wa Man United kuwa bado anataka kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. (Manchester Evening News)

Pogba bado ana nia ya kukiacha kikosi cha Man U

Juventus wanatathmini juu ya kumsajili winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24, ambaye pia anawindwa na Bayern Munich. (Calcio Mercato, via Inside Futbol)Kocha wa Man City Pep Guardiola anataka kusajili walinzi wa kati wawili hatua ambayo inazidi kuweka wingu jeusi kwa mustakabali wa beki wa England John Stones, 25. (Times, subscription required)Wakala wa winga Gareth Bale, 30, amekanusha kuwa Tottenham ilituma ofa ya usajili kwa klabu ya Real Madrid kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Talksport)Manchester United wanatarajia kipa wao raia wa Argentina Sergio Romero, 32, kuihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu sambamba na kipa wao namba tatu Lee Grant, 37. (Sun)Arsenal wanataka kumsajili kiungo wa Feyenoord na Uturuki Orkun Kokcu, 19.

Moussa Dembele ameifungia magoli kumi Lyon msimu huu wa ligi

Kocha Manuel Pellegrini amedai kuwa kiwango kibovu cha kipa Roberto kimechangia yeye kutimuliwa kazi na klabu ya West Ham. (Evening Standard)Mshambuliaji wa Leicester City na Algeria Islam Slimani, 31, “valikuwa karibu” ajiunge na klabu ya Inter Milan kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari. (Calcio Mercato, via Leicester Mercury)

Source link

Design a site like this with WordPress.com
Get started