
SIWAFUNDISHI KAZI,ILA NAWAKUMBUSHA.
Na Octa Ayubu Jr
Nimejaribu kufuatilia kwa ukaribu uteuzi wa kikosi Cha timu ya taifa kwa makocha wote waliopita ndani ya miaka 10,Ni nadra Sana kuyakosa majina mawili Kelvin Patrick Yondan na Erasto Edward Nyoni.Hawa ni miongoni mwa wachezaji wakongwe ndani ya timu ya taifa.
Sahau kuhusu Juma kaseja aliyepumzishwa kwa kipindi kirefu kabla hajapitiwa na neema ya Ettiene Ndayragije na kurejeshwa.wahenga walishasema “Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha” lakini wakaongeza “Usipoziba ufa utajenga ukuta”. Erasto nyoni,Naweza kuthubutu kutamka sioni mchezaji anayekuja kuziba pengo lake kwa urahisi,kwasababu huyu ni mchezaji pekee anayeweza kumpa mwalimu option ya matumizi yake katika namba 5 tofauti.Ni mchezaji gani atakuja kukifanya anachokifanya nyoni? Makocha wanaliona hili? ile ngongoro iliyopo fainali ya Cecafa ina mbadala wa nyoni?
Yondan sio mchezaji wa nafasi nyingi Kama ilivyo kwa nyoni.Lakini tuliza akili,fikiri Ni nani wa kurithi mikoba yake? Tena sio kwa kucheza vizuri mechi moja tu,bali mchezaji atakayedumu kwenye kiwango Bora kwa muda mrefu Kama alivyofanya nyondani.
Sidhani kama Tff na makocha wanaoiongoza Tanzania walijaribu kuomba kadi zao wakaangalia umri wao,badala yake wanachoangalia ni mwendelezo wa ubora wao bila kufikilia Mwisho wao na Tutaziba vipi mapengo yao.
Nilianza kuiona sura ya kelvin Yondan kwenye miguu ya Yusuph mlipili bahati mbaya kwake Ni kuingia jeshini kipindi Cha Vita,huku mshare wa Saa ukifuta ndugu na kadi yake ya kliniki.Ndio ameingia Simba kipindi ambacho Simba inahitaji mafanikio hivyo kulazimika kuwa fiti muda wote na kama unapata majeraha urudi kwenye ubora mapema Jambo ambalo limekuwa gumu kwake huku umri wake ukiwa sio rafiki.
Kuna mechi nyingi za kirafiki tunacheza,lakini kwa bahati mbaya zaidi nazo Yondani na Nyoni wanacheza.hizi ndizo zilikuwa mechi za kutengeneza mbadala wao kama alivyoaminiwa Kelvin John.Lakini kitendo cha kuendelea kuwatumia Nyoni na Yondani Kuna Wakati tutawakumbuka,lakini tutakuwa tumekwishaumia
Hawajachelewa,Nyoni na Yondan bado wanacheza katika ubora lakini umri wao hauna tofauti na Gari la mkaa mda wowote litaingia gereji.Hawa mda wowote wanaweza kutangaza kustaafu tukabaki kutazamana Nani alaumiwe.
Tff kwa kushirikiana na Benchi la ufundi wanatakiwa kushauriana ni jinsi gani Tanzania itapata mbadala wa Hawa malegend wawili.Kuna mahali nilisema tusahau kuhusu kaseja kwa sababu katika nafasi yake kuna mwanga unaonekana kupitia kwenye mikono ya Aishi manula,mwanga wa nyoni ukizimwa na pumzi ya zahera Alipoamua kumpoteza Pato ngonyani na huku miguu ya Yondani ikimezwa na majeruhi ya Salim mbonde. ©Sokaplace Tanzania
Tags @tanfootball @taifastars_