Namungo fc. “Tupo tayari kuisambaratisha azam fc”

Kuelekea mchezo wetu dhidi ya Azam fc, maandalizi yamekamilika tupo tayari kwa mchezo huo. Wadau, mashabiki na wapenzi wa namungo fc tujitokeze kwa wingi azam complex kuipa hamasa timu yetu. Mchezo utapigwa 5.10.2019 mida ya 1.00 usiku.
@vodacomtanzania @metlgroup @crdbbankplc
#namungofc
#southernkillers

Zawadi za Rock City Marathon Zawakosha Washiriki

Ikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya kufanyika kwa mbio za Rock City Marathon jijini Mwanza, wadau mbalimbali wanaotarajia kushiriki katika mbiohizo wameonyesha kufurahishwa na zawadi zitakazo tolewa kwa washindi na washiriki ikiwemo medali na fedha taslimu zaidi ya Sh Mil 30.

Mbio hizo zilizojinyakulia umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi zinatarajiwa kufanyika Octoba 20 mwaka huu kwenye Viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall huku wadau mbalimbali wakiwemo viongozi waandamizi serikalini akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella wakitarajia kushiriki katika mbiohizo.

Mratibu wambio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Kasara Naftal amesema pamoja na medali washindi wa kwanza wa
mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Tsh. Mil 4 kila mmoja Tsh. Mil2/- kwa washindi wa pili na Tsh. Mil1/-kwa washindi wa tatu, huku washindi wa nne hadi kumi na tano nao pia wakiibuka na zawadi za medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Bw. Kasara amesema pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia Tsh. Mil2/- kila mmoja, Tsh. Mil1/- kwa washindi wa pili na Tsh. Laki7/- kwa washindi wa tatu huku pia washindi wa nne hadi wa kumi na tano wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

“Kuhusu mbio za kilomita tano ambazo zitahusisha washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali (corporates) tunatarajia zitaongozwa na Mkuuwa Wilaya ya Nyamagana Dk. Philis Nyimbi sambamba na washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani albino ambapo zawadi za fedha taslimu zitatolewa kwa washindi watatu wenye ualbino pekee.”

Bw. Kasara aliongeza kuwa kwa washindi wa mbio za kilomita mbili na nusu zitakazo husisha watoto wenye umri kati ya miaka 7 hadi 10 watapatiwa fedha taslimu.

Mbio hizo zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinatarajiwa kupambwa na maonesho ya wadau umbalimbali wakiwemo wadhamini wa mbiohizo kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants.

Vuguvugu la bale na zidane lapamba moto

Kumekua na mvutano mkubwa kati ya mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale na meneja Zinadine Zidane, kumaanisha kuwa kiungo huyo wa kimataifa wa Wales hana maisha marefu katika klabu hiyo.

Video imeibuka ikimuonyesha Gareth Bale akiwasili Bernabeu dakika nne baada ya mchezo kuanza kati ya Real Madrid na Club Brugge kwenye Champions league

Sheria za kilabu ya Real Madrid zinaamuru kwamba wachezaji wote wa timu ya kwanza lazima wahudhurie mechi na kuzitazama mwanzo mpaka mwisho wa mchezo (Full time) – hata kama hawajachaguliwa kuanza katika kikosi.

Bale, ambaye hivi sasa anaweza kuadhibiwa chini ya sheria kali za nidhamu pale Madrid, amevunja sheria hii kabla wakati alipoondoka kwenye mchezo dhidi ya Real Sociedad dakika ya 78 mwezi Januari.

Baadhi ya Faini zilizowekwa na Klabu ya Real Madrid kwa wachezaji wasio na nidhamu:
•Kuchelewa Dakika 5, £222 (Laki 627,475)
•Kutokuwepo Mazoezini, £2670 (Milioni 7.5)
•Matumizi mabaya ya simu £890 (Milioni 2.5)
•Kuondoka pasipo ruhusa, £890

Real Madrid kuwakaribisha Granada..bernabeu..nani kuongoza la liga

#LaLigaSantander
⚽Real Madrid vs Granada
🏟 Bernabeu
🕰 17:00

1st vs 2nd: Mtanange kati ya Real Madrid na Granada unakutanisha timu ambayo inaongoza msimamo wa La Liga (Real Madrid) wakati Granada ikishika nafasi ya pili.

Granada wamepoteza mechi 14 kati ya 15 walizocheza kwenye La Liga dhidi ya Real Madrid. Ushindi wao pekee dhidi ya Real Madrid ulikuwa mnamo Februari 2013 kwa bao la kujifunga la Cristiano Ronaldo Zidane anaitaji ushindi katika mchezo wa leo, kwani ni miongoni mwa makocha waliopo kwenye hatari ya kupoteza ajira zao

FC Bayern Munich kuivaa Hoffenheim .leo

FC Bayern Munich vs Hoffenheim .
.
Ni ngumu kutokuionea huruma Hoffenheim kuelekea kwenye mchezo wa leo kutokana na form waliyonayo Bayern hivi karibuni. Wamepanda kileleni mwa msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza msimu huu wikiendi iliyopita kwa ushindi wa 3-2 dhidi ya Paderborn.

Ushindi huo uliofuatiwa na kipigo kitakatifu walichowapa Spurs cha magoli 7-2 katika Champions League – mechi ambayo Serge Gnabry alifunga magoli 4, wakati kikosi cha Niko Kovac kilipotoa onyo zito kwa timu pinzani barani Ulaya.

Coutinho na Gnabry leo huenda wakaanza tena, ingawa Thomas Muller pia anataka kurejea kikosini. Leon Goretzka, Fiete Arp, Lucas Hernandez na David Alaba hawa wote hawatohusika na mchezo huu kutokana na majeruhi. Benjamin Pavard anatarajiwa kuziba nafasi upande wa kushoto wa ulinzi, Kimmich ataendelea na majukumu yake upande wa kulia.
.
.
Hoffenheim bado hawajapata mwendo mzuri msimu huu, wakishinda mechi 1, sare 2 na wamefungwa 3. Kulikuwa na ishara nzuri katika mchezo dhidi ya Borussia Mönchengladbach wiki iliyopita, lakini Bado waliangukia pua kwa kipigo cha magoli 3-0. Kuendelea kutokuwepo kwa mshambuliaji wao Andrej Kramaric kumezidisha matatizo – vijana wa kocha Alfred Schreuder wamefunga magoli 4 tu kwenye ligi msimu huu – na leo pia watamkosa Mcroatia huyo pia.
.
.
Takwimu
.
• Lewandowski ndio mchezaji wa kwanza katika Bundesliga kufunga idadi ya magoli zaidi 9 baada ya mechi 6 tu za ligi – akifunga goli katika kila mechi. Anahitaji kuendelea kufunga katika mechi mbili zijazo ili kuifikia rekodi ya kufunga mechi 8 za mwanzo mfululizo iliyowekwa na Pierre-Emerick Aubameyang.
.
•Bayern hawajawahi kupoteza mchezo wa nyumbani dhidi ya Hoffenheim, wakishinda 9 kati ya 11 katika dimba la Allianz Arena. The Bavaria wamefunga jumla ya magoli 35 na kuruhusu 9 tu katika mechi hizo.
.
.
Mchezo huu utakuwa live kuanzia majira ya 10:30 jioni, na kwa kipekee kabisa utaonyeshwa on @startimestz

Wachezaji watano wa Eritrea wametoweka nchini Uganda CECAFA U20

Wachezaji watano wa timu ya taifa ya Eritrea wametoweka nchini Uganda katikati ya mashindano ya Kombe la Cecafa U20.

Uongozi wa soka nchini Uganda unasema kuwa wachezaji hao hadi sasa hawajarudi kambini na haifahamiki wako wapi.

Kipa wa Eritrea U20 Girmay Hanibal ni mmoja kati ya watano ambao wameondoka. Wengine wanne ni Simon Asmelash, Deyben Gbtsawi Hintseab, Hermon Fessehaye Yohannes na Mewael Tesfai Yosief. Ripoti zinaonyesha usalama umeongezeka kuzunguka hoteli ili kuepusha wachezaji zaidi kukimbia.

Hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa Eritrea kutoweka wakati wa mashindano mnamo 2009, timu nzima ya taifa haikurudi nyumbani baada ya mashindano nchini Kenya. Kocha tu na ofisa mmoja ndio waliopatikana

Kikundi cha haki za binadamu Amnesty International kinasema kwamba kulazimishwa kwa raia kujiunga na jeshi na unyanyasaji wa haki ni sababu zinazopelekea maelfu kukimbia Eritrea.

RATIBA YA SOKA LEO JUMAMOSI

#TanzaniaFDL A
16:00 Maji Maji vs Mbeya Kwanza
16:00 Mlale vs Iringa United
16:00 Reha Fc vs African Lyon
16:00 Friends Rangers vs Ashanti United
16:00 Dodoma Fc vs Ihefu Fc
16:00 Njombe Fc vs Boma Fc
:
#VodacomPremierLeague
19:00 Azam FC vs Namungo FC
:
#EnglandPremierLeague
14:30 Brighton vs Tottenham
17:00 Burnley vs Everton
17:00 Liverpool vs Leicester City
17:00 Norwich City vs Aston Villa
17:00 Watford vs Sheffield United
19:30 West Ham United vs Crystal Palace
:
#EnglandChampionship
14:30 Fulham vs Charlton Athletic
17:00 Bristol City vs Reading
17:00 Derby County vs Luton Town
17:00 Huddersfield Town vs Hull City
17:00 Millwall vs Leeds United
17:00 Nottingham Forest vs Brentford
17:00 Preston North End vs Barnsley
17:00 Queens Park Rangers vs Blackburn
17:00 Sheffield vs Wigan Athletic
17:00 Swansea City vs Stoke City
17:00 West Bromwich vs Cardiff City
:
#TanzaniaFDL B
16:00 Rhino vs Mawenzi Market
16:00 Mashujaa vs Sahare All Star
16:00 Arusha Fc vs Green Worriors
16:00 Stend United vs Transit Camp
16:00 Geita Gold vs Gwambina
:
#SpainLaLigaSantander
14:00 Leganes vs Levante
17:00 Real Madrid vs Granada
19:30 Valencia vs D. Alaves
22:00 Osasuna vs Villarreal
:
#ItalySerieA
16:00 SPAL vs Parma
19:00 Verona vs Sampdoria
21:45 Genoa vs Milan
:
#GermanyBundesliga
16:30 B.Leverkusen vs RasenBallsport Leipzig
16:30 Bayern München vs Hoffenheim
16:30 Freiburg vs B.Dortmund
16:30 SC Paderborn vs Mainz 05
19:30 Schalke 04 vs 1. FC Köln
:
#FranceLigue 1
18:30 PSG vs Angers
21:00 Dijon vs Strasbourg
21:00 Nantes vs Nice
21:00 Toulouse vs Bordeaux
21:00 Montpellier vs Monaco
21:00 Brest vs Metz
:
#AlgeriaLigue1
18:00 NC Magra vs MC Alger
19:45 MC Oran vs USM Alger
20:45 ASO Chlef vs USM Bel Abbes
21:00 US Biskra vs CS Constantine
:
#EgyptPremierLeague
16:00 Aswan FC vs Al Ahly
18:30 El Entag El Harby vs Al Mokawloon Al Arab
18:30 Wadi Degla FC vs Ismaily SC
21:00 Al Masry vs Al-Ittihad Al-Sakandary
:
#BelgiumFirstDivisionA
19:00 Eupen vs Mechelen
21:00 Waasland-Beveren vs Oostende
21:00 Zulte Waregem vs Cercle Brugge
21:30 Kortrijk vs St.Truide

Imeandaliwa na @officialchristz wa @sokaplace_

MATOKEO YA SOKA JANA IJUMAA :

#EnglandChampionship
FT Birmingham City 2 – 1 Middlesbrough

#SpainLaLigaSantander
FT Real Betis 1 – 1 Eibar
:
#GermanyBundesliga
FT Hertha BSC 3 – 1 Fortuna Düsseldorf
:
#FranceLigue1
FT Amiens 3 – 1 Marseille
:
#BelgiumFirstDivisionA
FT Sporting Charleroi 1 – 2 Anderlecht
:
#ScotlandChampionship
FT Alloa Athletic 1 – 0 Dundee United
:
#EgyptPremierLeague
FT Smouha SC 2 – 1 ENPPI
:
KAMATA RATIBA YA SOKA LEO.
:
#AlgeriaLigue1
18:00 NC Magra vs MC Alger
19:45 MC Oran vs USM Alger
20:45 ASO Chlef vs USM Bel Abbes
21:00 US Biskra vs CS Constantine
:
#EgyptPremierLeague
16:00 Aswan FC vs Al Ahly
18:30 El Entag El Harby vs Al Mokawloon Al Arab
18:30 Wadi Degla FC vs Ismaily SC 21:00 Al Masry vs Al-Ittihad Al-Sakandary
:
#KenyaPremierLeague
13:00 SoNy Sugar vs AFC Leopards 14:00 Chemelil Sugar vs Kariobangi Sharks
14:00 Posta Rangers vs Kisumu All Stars
14:00 Western Stima vs Ulinzi Stars 14:00 Mathare United vs Wazito FC 16:15 KCB vs Nzoia Sugar FC

Imeandaliwa na @officialchristz
Wa @sokaplace_

MATOKEO YA SOKA JANA IJUMAA :

#EnglandChampionship
FT Birmingham City 2 – 1 Middlesbrough

#SpainLaLigaSantander
FT Real Betis 1 – 1 Eibar
:
#GermanyBundesliga
FT Hertha BSC 3 – 1 Fortuna Düsseldorf
:
#FranceLigue1
FT Amiens 3 – 1 Marseille
:
#BelgiumFirstDivisionA
FT Sporting Charleroi 1 – 2 Anderlecht
:
#ScotlandChampionship
FT Alloa Athletic 1 – 0 Dundee United
:
#EgyptPremierLeague
FT Smouha SC 2 – 1 ENPPI
:
KAMATA RATIBA YA SOKA LEO.
:
#AlgeriaLigue1
18:00 NC Magra vs MC Alger
19:45 MC Oran vs USM Alger
20:45 ASO Chlef vs USM Bel Abbes
21:00 US Biskra vs CS Constantine
:
#EgyptPremierLeague
16:00 Aswan FC vs Al Ahly
18:30 El Entag El Harby vs Al Mokawloon Al Arab
18:30 Wadi Degla FC vs Ismaily SC 21:00 Al Masry vs Al-Ittihad Al-Sakandary
:
#KenyaPremierLeague
13:00 SoNy Sugar vs AFC Leopards 14:00 Chemelil Sugar vs Kariobangi Sharks
14:00 Posta Rangers vs Kisumu All Stars
14:00 Western Stima vs Ulinzi Stars 14:00 Mathare United vs Wazito FC 16:15 KCB vs Nzoia Sugar FC

Imeandaliwa na @officialchristz
Wa @sokaplace_

Design a site like this with WordPress.com
Get started