Tottenham..yaanza mipango ya kunasa James Maddison wa Leicester City

– Mshambuliaji wa klabu ya Leicester City, James Maddison ndio Target namba moja ya klabu ya Tottenham, wakimuona Muingereza huyo kama mbadala sahihi wa nyota wao, Christian Eriksen Ambaye muda wake wa kuondoka klabuni hapo unahesabika.

– Maddison pia anawindwa na Manchester United, lakini Klabu hiyo ya London chini ya kocha wao Mauricio Pochettino wanaongoza mbio za kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22..
#tottenham #leicestercity #TransfersNews #SokaPlaceUpdates
@Harunlugoyah

Je.ndairagije kushinda mchezo wa tatu…mbele ya namungo fc

Kwenye muendelezo wa mechi za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara |
⚽Azam FC vs Namungo
🏟 Chamazi Complex
⏰ 1:00 usiku

Namungo amepata pointi 7 kwenye michezo minne aliyocheza mpaka sasa wakati Azam ikiwa na pointi 6 baada ya kucheza mechi 2.
Azam imecheza mechi mbili za ligi na kushinda zote, katika mechi 4 zilizopita kwenye mashindano yote, Azam imeshinda mechi mbili na kupoteza mechi mbili.

Azam FC ?? Namungo FC
Azam FC 2-0 Ndanda FC
Triangle 1-0 Azam FC
Azam FC 0-1 Triangle
KMC FC 0-1 Azam FC

Namungo ilikuwa na mwanzo mzuri wa ligi baada ya kukusanya pointi 7 kwenye uwanja wa nyumbani, imeshinda mechi mbili na sare moja kabla ya kupoteza mchezo wake wa ugenini dhidi ya KMC FC mchezo ambao ulichezwa uwanja wa Azam Complex.

Azam FC ?? Namungo
KMC FC 1-0 Namungo
Namungo FC 0-0 Mwadui
Namungo FC 2-0 Singida United
Namungo FC 2-1 Ndanda

Leo kwa mara nyingine Namungo watakuwa Azam Complex kucheza na wenyeji Azam FC, Namungo itatoboa?

#VPL
#AzamNamungo

Clop ajipanga kuivaa Leicester City kisawasawa

Premier League

Liverpool vs Leicester City
Anfield
11:00 jioni

Liverpool wanaongoza ligi kwa ushindi wa asilimia 💯 hawajapoteza mchezo katika mechi 7 walizocheza msimu huu lakini wanatambua ugumu wa kocha wao wa zamani Brendan Rodgers ambaye tangu alipoajiriwa na Leicester City amekuwa akifanya vizuri.

Liverpool bado wanakumbukumbu ya hofu waliyojazwa na Salzburg katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya ambapo waliruhusu wavu wao kutikiswa mara tatu kabla ya Mo Salah kufunga goli la ushindi.

Brendan Rogers wa Leicter City anarudi pale Anfield tangu aachane na Liverpool mnamo oktoba 2015, nani kuibuka na ushindi Klopp au Rogers? na beki Van Dijik ataweza kuuzima moto wa Vardy?

Tembelea http://www.mbet.co.tz usepe na mkwanja!! #Mbet #NyumbaYaMabingwa

Kocha mkuu mpya wa Timu ya Taifa ya Uganda atangaza kikosi

Kocha mkuu mpya wa Timu ya Taifa ya Uganda, Johnathan McKinstry ametaja majina ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Ethiopia October 13, 2019.

Kikosi cha Cranes kinaundwa na:
Makipa:
Denis Onyango (Mamelodi Sundowns, South Africa), Robert Odongkara (Horoya AC, Guinea)

Mabeki:
Bevis Mugabi (Motherwell, Scotland), Timothy Awany (FC Ashdod, Israel), Ronald Mukiibi Ddungu (FK Ostesunds, Sweden), Hassan Wasswa Mawanda (Jeddah FC, Saudi Arabia), Joseph Benson Ochaya (TP Mazembe), Isaac Muleme (Viktoria Žižkov), Nico Wakiro Wadada (Azam, Tanzania)

Viungo:
Michael Azira (Chicago Fire, USA), Allan Kyambadde (El Gouna, Egypt), Tadeo Lwanga (Tanta, Egypt), Khalid Aucho (El Meskir, Egypt), Abdu Lumala (Pyramids, Egypt), William Luwagga Kizito (Shakhter Karagandy, Kazakhstan), Milton Karisa (Oujda, Egypt), Moses Opondo (FC Odense, Denmark)

Washambuliaji:
Patrick Henry Kaddu (RS Berkhane, Morocco), Derrick Nsibambi (Smouha), Emmanuel Arnold Okwi (Al Ittihad, Egypt)

Katika kikosi hicho, HAKUNA mchezaji hata mmoja anayecheza ligi ya ndani (Uganda)

#UgandaNationalTeam.

Kocha mkuu tottenham ahaidi shangwe kwa mashabiki

Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettino amewaahidi mashabiki wa klabu hiyo kuwa kwasasa anawekeza nguvu zake kwa kiungo Delle Ali ili kuhakikisha anamrudisha kwenye ubora wake.
.
.
Pochettino amekiri kuwa Delle Ali yupo kwenye kipindi kigumu kwasasa na anatambua kuwa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi chake hivyo atahakikisha anapambania arudi kwenye ubora wake ili kuisaidia timu yake.
.
.
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Mkongwe Godfrey WALUSIMBI astafu kuichezea timu ya taifa uganda

✍🏿 Godfrey WALUSIMBI Amethibitisha Kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa ya Uganda 🇺🇬 “Uganda Cranes” akiwa na umri wa Miaka 30 huku Miaka 1️⃣0️⃣ akilitumikia taifa lake.

✍🏿 Walusimbi aliichezea Uganda Cranes kwa mara ya kwanza Septemba 2010 katika mchezo dhidi ya Angola akitokea benchi ilikuwa ni kuwania kufuzu kwa AFCON 2012… tangu hapo kaichezea Uganda mechi zaidi ya 100 na kuwa Mchezaji wa kwanza kufikisha idadi ya mechi hizo kwa Cranes… Legend 🙌👏
#UgandaCranes
@Harunlugoyah

Lampard amteua Jorginho kuwa nahidha msaidizi chelsea

Kocha Mkuu wa klabu ya Chelsea, Frank Lampard Amethibitisha kuwa kiungo wake wa Kimataifa wa Italia 🇮🇹, Jorginho ndio Nahodha mpya msaidizi wa klabu hiyo ya London.
..
– Lampard amesema kuwa nyota huyo wa zamani wa Napoli amekuwa ni Mchezaji mwenye ushawishi mkubwa wa timu kusonga mbele ndani na nje ya uwanja licha ya kujiunga hivi karibuni kutoka kucheza Soka lake nchini Italia.

– Msimu uliopita, Gary Cahill alichaguliwa kama nahodha wa klabu kila alipokuwa uwanjani chini ya kocha Maurizio Sarri, na Cesar Azpilicueta alitajwa kama nahodha Msaidizi – lakini sasa Azpilicueta amekuwa nahodha Mkuu wa klabu.
#PremierLeague #ChelseaFC
@Harunlugoyah

KIKOSI CHA TANZANIA U20 vs KENYA U20

1-Razack Shekimweli
2-Israel Mwenda
3-Gustapha Saimon
4-Dickson Job
5-Oscar Masai
6-Novatus Miroshi
7-Tepsi Evance
8-Kelvin Nashon
9-Andrew Simchimba
10-Kelvin John Mbappé
11-Abdul Seleman
:
SUBs
-Ally Salim (GK)
-Wilbol Maseke (GK)
-Kibwana Shomary
-Lusajo Mwaikenda
-Frank Kihole
-Ally Msengi
-Gadafi Said
-Said Luyaya
-Onesmo Mayaya
:
Mchezo wa fainali ya CECAFA U20 muda ni saa 9:30 Alasiri katika dimba la FUFA Technical Centre, Njeru Uganda.
Live:- Azam Extra.

@yossima_sports

Kahata apoteana simba hajui acheze namba gapi

Kiungo Francis Kahata alianza maisha yake vyema katika klabu ya Simba, akifunga moja ya mabao kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc ambao Simba ilishinda kwa mabao 4-2

Tangu mchezo huo, Kahata amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Patrick Aussems

Kupona kwa Ibrahim Ajib na kiwango kizuri kinachoonyeshwa na Miraji Athumani, kimebadili upepo kwa kiungo huyo

Hata hivyo Kahata, kiungo wa Kimataifa wa Kenya, bado anahitaji kujituma ili kumshawishi Aussems kuweza kumpa nafasi

Simba ina ‘utajiri’ mkubwa wa wachezaji mafundi kwenye nafasi anayocheza

Mzamiru Yassin, Sharaff Shiboub, Hassan Dilunga, Ibrahim Ajib na Miraji ni baadhi tu ambao wanafanya vizuri zaidi yake

Neema yaendelea kumiminika msimbazi

Kocha Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Patrick Aussems jana alichaguliwa kuwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi Septemba huku mshambuliaje wake, Miraji Athumani naye akishinda tuzo ya Mchezaji Bora

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo, alisema jana kuwa Aussems na Miraji wametwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wapinzani wao walioingia nao hatua ya fainali katika uchambuzi uliofanywa na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na shirikisho hilo.

Ndimbo alisema kuwa kwa mwezi huo uliopita, Simba ilicheza michezo mitatu na kushinda yote, ikiifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1, Kagera Sugar mabao 3-0 na Biashara United mabao 2-0, ambapo Miraji alikuwa na kiwango kizuri uwanjani kwa mwezi huo na kuchangia kwa asilimia kubwa mafanikio ya timu yake.

“Mbali na kucheza katika kiwango cha juu, Miraji alifunga mabao mawili katika mechi hizo tatu na vile vile alitoa pasi za mabao mawili,” alisema Ndimbo.

Aliongeza kuwa Miraji alimshinda mchezaji mwenzake kutoka Simba, Meddie Kagere, ambaye pia alitoa mchango mkubwa katika mafanikio ya Simba ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne na Ismail Kada wa Tanzania Prisons.

“Kada naye, kufuatia mapendekezo kutoka kwa makocha wanaohudhuria mechi katika viwanja mbalimbali, ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu, alionyesha kiwango kizuri na kutoa mchango katika michezo ambayo Prisons ilicheza, ikishinda miwili, sare moja, ambapo iliifunga Ruvu Shooting mabao 2-1, Mtibwa Sugar mabao 3-1 na kutoka sare ya magoli 2-2 dhidi ya Lipuli FC.

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Miraji atazawadiwa kikombe na zawadi ya Sh. milioni moja kutoka kwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo, Vodacom pamoja na kisimbusi kutoka Azam TV.

Kwa upande wa Aussems, yeye aliwashinda Mohammed Rishard wa Tanzania Prisons na Abdallah Baresi wa JKT Tanzania, baada ya Mbelgiji huyo kuwaongoza mabingwa watetezi kuweka pointi tisa kibindoni kutokana na mechi tatu walizocheza mfululizo.

Simba ndio vinara wa ligi hiyo baada ya kuwa na pointi 12, wakiwa wamecheza mechi nne wakati watani zao Yanga walioshuka dimbani mara mbili, wana pointi moja na wako katika nafasi ya 19

Nipashe

Design a site like this with WordPress.com
Get started