Klabu Ya Pamba SC yavunja mkataba na kocha wake mkuu

#Repost From @pambasportsclubofficiall

Uongozi wa Klabu Ya Pamba SC Tumefika Makubaliano ya Kuvunja Mkataba na aliyekua Kocha Wetu Muhibu Kanu kwa makubaliano ya Pande zote Mbili Baada ya Ombi lake la Kuvunja Mkataba kukubaliwa na Kamati tendaji Ya Klabu.

Kocha Muhibu Aliomba Kuondoka kwenye Klabu kutokana na Sababu zilizo Nje ya Uwezo wake na Uongozi Leo hii Umefika makubaliano ya Kuachana na Kocha huyo na mchakato wa kumpata Kocha Mpya Ukiwa tayari Umeanza.

Hata Hivyo Uongozi wa Klabu ya Pamba SC umeamua Kuvunja Benchi lake la Ufundi na Kuacha majukumu ya Kuongoza katika Mazoezi Chini ya Kocha wa Makipa Hassan Shehata.

Pamba SC inamtakia Kila lakheri Kocha Muhibu Kanu na tunamshukuru kwa mchango wake Wote ndani ya Klabu yetu.

WACHEZAJI WA SIMBA WAKOMALIA KUTAKA KULIPWA FEDHA ZAO ZA USAJILI

Story za vijiweni: WACHEZAJI WA SIMBA WAKOMALIA KUTAKA KULIPWA FEDHA ZAO ZA USAJILI
:
Sakata la baadhi ya nyota wa Simba ambao hawajalipwa hela zao za usajili limeshika kasi sana.
:
๐Ÿ‘‰ Kuna tetesi nyingi sana vijiweni. Inadaiwa kuwa Chama ameshinikiza kulipwa stahiki zake. Wengine ni Gadiel, Kahata, Nyoni na Mkude. Tetesi hizi zina ukweli kwa kiasi fulani kutokana na tabia ya vilabu vyetu hivi. :
๐Ÿ‘‰ Kuhusu hao wanne sina taarifa zaidi lakini taarifa za Kahata kutokulipwa nazifahamu kidogo. Wale waliosaidia dili Kahata kukamilika hawajamaliziwa chao achilia mbali hela ya Kahata.
:
๐Ÿ‘‰ Kuna jamaa aliahidiwa kiasi cha takribani dola 700 katika dili hilo (Tsh milion 1. 6) ila mpaka sasa amepewa kama $300. Jamaa mwingine ambaye alifanikisha kwa kiasi kikubwa dili hilo ameshakuja Tanzania kama mara 3 kufuatilia stahiki zake, lakini hola.
:
๐Ÿ‘‰ Taarifa za vijiweni zinasema aliyepaswa kutoa fedha hizo ni Magori. Baadhi ya wahusika wanasema Magori alikuwa anawasumbua sana kulipa.
:
๐Ÿ‘‰ Baadhi aliwaambia atawalipa kwa awamu jambo ambalo halikuwa kwenye mkataba.
:
๐Ÿ‘‰ Anyway najua jambo hili ni dogo tu na litamalizika soon ila huu ni uswahili ambao ulitafuna sana soka letu. Ujio wa Masingiza utabadilisha hali ya hewa.
:
๐Ÿ‘‰ Ukiangalia kwa Makini utagundua ndio Maana Bwana Heri siku hizi hata uwanja anafuatilia mwenyewe. Maji ya kunywa ya saidia fundi siku hizi Bwana Heri analipa mwenyewe hata ujinga na mtu ๐Ÿคจ

Cc @privaldinho

Kagere apumzishwa timu.ya taifa

Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Rwanda ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Oktoba 14

Kagere ameendelea kujifua na Simba ambapo mpaka jana hakuwa amepokea wito kutoka shirikisho la Soka nchini Rwanda

Timu hiyo huenda ikatumia wachezaji wake wanaocheza ligi za ndani kama ilivyofanya Tanzania

Kagere amesema anafahamu mchezo huo ni wa kirafiki hivyo hakuna cha kupoteza hata kama hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo

“Timu yangu ya Rwanda itacheza na Tanzania, najua lakini kwa upande wangu sifahamu kama nitakuwa miongoni mwa kikosi hicho kwa kuwa bado sijaitwa, ngoja tusubiri, nikiitwa sawa, nisipoitwa pia haina shida,” amesema Kagere

“Sina wasiwasi sababu mchezo wenyewe ni wa kirafiki, hakuna cha kupoteza, inawezekana kocha ameamua kuwapa nafasi zaidi wachezaji wanaocheza ligi ya ndani”

David De Gea amesemaย  kikosi cha manchesternunitedi kinanipa tabu

Mlinda lango wa Manchester United, David De Gea amesema kikosi chao kinapitia katika hali ngumu hususan mwanzoni mwa msimu huu na kutaka juhudi za makusudi zichukuliwe kuinusuru timu hiyo.

De Gea alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika mechi ya Ligi Kuu England Jumapili dhidi ya Newcastle United ambapo Mashetani Wekundu hao walipokea kichapo cha bao 1-0.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Sky Sports, De Gea alisema, Man United haipo vizuri ila watahakikisha wanapambana kurudi kwenye ubora wao.

“Sielewi kwanini iko hivi, tuna wakati mgumu kwasasa, kama nilivyosema na siwezi kuzungumza kitu, kwa pamoja tumekabiliana na hili na mambo yatakawa sawa,” alisema De Gea.

Man United haijashinda mechi zake tatu za mwisho za ligi, jambo ambalo limetoa hofu kwa wakongwe, waliowahi kukipiga humo akiwamo Michael Owen, Robin van Persie, Garry Neville na Alan Shearer.

Timu hiyo iko juu ya mstari wa kuteremka daraja kwa tofauti ya alama mbili tu licha ya kushika nafasi ya 12

Agrey Morris arwjea kikosini Azam fc ..

Beki mahiri wa Azam Fc Agrey Morris, huenda akaanza kucheza katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba, unaotarajiwa kupigwa Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, baada ya jana kuanza mazoezi mepesi.

Agrey alikosekana uwanjani kwa muda mrefu baada ya kuumia, akiwa Misri na timu ya Taifa, Taifa Stars, walipokuwa wakicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri, ikiwa ni maandalizi ya michuano ya Afcon iliyofanyika nchini humo na Algeria kutwaa ubingwa.

Afisa Habari wa Azam, Jafar Iddy, amesema kuwa kikosi chao kilianza mazoezi jana baada ya kupewa mapumziko ya siku mbili, ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Simba.

“Wachezaji wameanza mazoezi lakini pia nahodha wetu Morris aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, kwa sasa ameanza mazoezi mepesi baada ya hali yake kuimarika, hivyo huenda akacheza mchezo wetu dhidi ya Simba,” alisema.

Alisema kwa sasa wachezaji wao wote wanaendelea na mazoezi licha ya kuwa ligi imesimama kwa muda kupisha mchezo wa kirafiki wa Taifa Stars dhidi ya Rwanda.

Iddy alisema kwa sasa wachezaji wote wapo fiti huku kila mmoja akiwa na morali ya juu kuhakikisha wanaipatia timu yao matokeo mazuri.

Kurejea dimbani kwa Morris kunatarajiwa kuongeza uhondo kati yake na safu ya ushambuliaji ya Simba, inayoongozwa na Meddie Kagere.

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kushuka dimbani mara tatu na kushinda michezo yote, ikiwa haijapoteza hata mmoja.

Kanu akerwa wachezaji wa nigeria kubembeleza timu ya taifa

Nyota wa zamani wa Arsenal na Nigeria Nwankwo Kanu, ameitaka Shirikisho la Soka la nchi hiyo (NFF) kutowalazimisha wachezaji ambao wana asili ya taifa hilo.

Shirikisho hilo hivi karibu limejaribu kuwashawishi nyota wa kimataifa wa England, Tammy Abraham na Fikayo Tomori, ambao wana asili ya Nigeria.

“Nadhani hatupaswi kufanya hivyo, Nigeria ni kubwa zaidi ya wachezaji, huwezi kuomba mchezaji kucheza, tuna kila aina ya vipaji hii sio sahihi,” alisema Kanu.

“Mchezaji ana maamuzi yake kucheza, soka lipo hivyo (Super Eagles) tuna uwezo wa kushinda bila hata hao wachezaji”

Tammy Abraham amekuwa na msimu mzuri kwenye klabu ya Chelsea akiifungia timu hiyo mabao saba msimu huu

Pamoja na kuwa na asili ya Nigeria, Abraham amesema angependa kuichezea Uingereza, nchi aliyozaliwa na kukulia

Guardiola “kazi ipo.kuliziba pego lililopo mbele.yangu”

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema “pengo ni kubwa” lakini bado anaamini timu yake inaweza kuifikia Liverpool katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la ligi kuu England.

Pigo la Wolves 2-0 dhidi ya City ina maana sasa klabu hiyo ipo nyuma kwa pointi nane nyuma ya Liverpool.

Ni tofauti kubwa iliyowahi kuwepo baada ya mechi nane katika ligi kuu ya England – Timu ya awali iliowahi kuwa katika nafasi hiyo ni Chelsea mnamo 2014, ilioishia kushinda taji.

Ninawafahamu hawa jamaa,” anasema Guardiola. “Bado wanajikakamua na bado wanaweza kushinda.”

Kushindwa huko kuna maanisha kuwa City inakabiliwa na mwanzo mbaya kuwa kushuhudiwa tangu kampeni ya 2013-14 chini yake Manuel Pellegrini, wakati waliposogea na kushinda taji.

Liverpool ilizuia rekodi yake ya 100% Jumamosi kutokana na jeraha alilopata James Milner lililompatia penalti dhidi ya Leicester.

“Pengo ni kubwa, hilo najua,” anasema Guardiola. “Kwa wakati mwingi, [Liverpool] haikushuka kwa pointi. Ni vyema kutofikiria timu moja iko pointi nane mbele. Ni oktoba tu hii. bado kuna mechi nyingi.”

Pengo kubwa iliokuwa nayo City ambalo ilibidi kuliziba dhidi ya Liverpool msimu uliopita ilikuwa ni la pointi 10, licha ya kwamba hilo lilikuwa ni baad aya mechi 19 na ikisalia na mechi moja na timu hizo zililazimika kucheza mara moja . Timu hizo mbili zinakutana kw amara ya kwanza Anfield Novemba 10.

City inapania kuwa timu ya kwanza kushinda mataji matatu ya ligi tangu Manchester United kati ya 2007-09. Wakati wa mwisho walikuwa timu ya kwanza kulishikilia taji hilo tangu wakati huo. Chelsea ndio timu nyingine iliowahi kushinda mataji kwa mtawalia katika enzi ya Premier League.

“Timu nyingi zilizoshinda siku za nyuma, mwaka uliofuata hazikushinda,” anasema Guardiola.

City imeshindwa kushinda mechi mbili za ufunguzi nyumbani kwa mara ya kwanza tangu 2014. Tayari timu hiyo imeshukwa kwa pointi tano nyumbani pointimbili zaidi ya msimu mzima uliopita.

Mwaka uliotangulia, walipoweka rekodi ka kufika pointi 100 walishuka kwa pointi 7 uwanjani Etihad katika kampeni nzima.

Kabla ya mechi dhid ya Wolves, City ilikuwa ndio timu kati ya ‘sita kubwa’ ‘ambayo Wolves ilishindwa kuifunga tagu kuanza kwa msimu, ikiwa imezifunga nyingine kwenye ligi na kuwahi kuiondoa Liverpool kutoka kwenye kombe la FA.

“Ilikuwa ni siku mbaya,” anasema Guardiola. ” Nilihisi siku ya leo itakuwa ndio siku ambayo hatutakuwa na mapato. Tumekabiliana na timu nyingi zenye ulinzi mkali na kwa namna moja au nyingine tumepata njia ya kulishughulikia hilo, lakini leo tulikuwa na shida.”

Mkude afanya yake ..rungu la.simba kumshukia

Uongozi wa klabu ya Simba utaweka wazi hatma ya kiungo wake Jonas Mkude ambaye anatuhumiwa kwa makosa ya utovu wa Nidhamu

Inaelezwa suala la Mkude tayari limeshajadiliwa na Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo ambapo mwenyewe alipewa nafasi ya kujitetea

Hata hivyo uongozi wa Simba umeona sio vyema kutoka hukumu wakati huu ambao kiungo huyo fundi anakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa

“Suala la Mkude limesimama kwa muda kwa sababu ya kuitwa katika kikosi cha Stars, hukumu yake ilikuwa itolewe leo (jana) Jumatatu, lakini ameshajieleza na sisi viongozi wa timu, pia tulitoa taarifa kwa upande wetu, ” alibainisha mmoja wa viongozi aliyekuwa kwenye Kamati iliyokuwa ikijadili suala hilo

Mkude anakabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa ambapo Oktoba 14 Stars itacheza na Rwanda ukiwa ni mchezo wa kirafiki ambao uko kwenye kalenda ya FIFA

Oktoba 18 Stars itarudiana na Sudan katika mchezo wa kusaka tiketi ya michuano ya CHAN kwa wachezaji wa ndani

Mchezo huo utapigwa nchini Uganda

Mkude alifikishwa kwenye kamati ya Nidhamu ya klabu ya Simba baada ya ‘kukacha’ safari kanda ya ziwa bila ya kutoa taarifa kwa uongozi wa timu hiyo

Yanga yawapa wachezaji mapumziko..zahera atimkia kongo

Kocha Mkuu wa Yanga SC Mwinyi Zahera anatarajiwa kurejea nchini Oktoba 19 mwaka huu kutoka kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya DR Congo ambayo inakabiliwa na jukumu la mechi mbili za kirafiki.

Afisa Habari wa timu hiyo Hassan Bumbuli amesema mara baada ya kocha huyo kurejea, kikosi kitaanza rasmi kambi kujiandaa na mechi mbili za ligi kuu zitakazochezwa jijini Mwanza dhidi ya Mbao FC na dhidi ya Alliance FC.

Bumbuli amesema baada ya mechi ya jana dhidi ya Coastal Union, kikosi hicho kimepewa mapumziko ya siku tatu kabla ya kuanza mazoezi ya kawaida huku kikimsubiri kocha wake Mwinyi Zahera.

Katika hatua nyingine, Bumbuli ametaja wachezaji tisa wa timu hiyo ambao ni majeruhi wa sasa akiwemo Kelvin Yondani.

Design a site like this with WordPress.com
Get started