
Baada ya FIFA kutaja timu ya Wachezaji Bora wa mwaka ‘FIFA The Best’ wiki kadhaa zilizopita.
•
Gazeti maarufu la Uhispania Marca kama kawaida yake liliamua kuandaa toleo la 3 la kikosi cha wachezaji wabovu zaidi ‘The Worst X1’ ambapo wasomaji wake walipiga kura kuchagua kikosi hicho.
•
Ila malalamiko yameanza kujitokeza baada ya beki wa Arsenal, Mustafi kunukuliwa akisema 🗣”Mimi sio beki wa pili mbaya zaidi ulimwenguni. Ninaweza pia kukabiliana na ukosoaji mgumu. Lakini ukosoaji umezidi na hauna maana. Nimekuwa mlengwa katika hili. Wakati fulani, watu hata walinilaumu tukifugwa na wakati huo nilikuwa sijacheza hata.”😀
•
Katika kikosi icho wachezaji watatu wa Manchester United wapo kwenye Kikosi Kibovu cha mwaka.
•
Nani kaonewa? Nani kakosekana?












