•
Jina kamili la uwanja huu ni First National Bank Stadium, au Soccer City pia hufahamika kwa jina la “The Calabash” uwanja huu upo kwenye mji mdogo wa Nascer uliopo Kwenye Manispaa ya Johannesburg Afrika Kusini
•
Uwanja huu hutumiwa na klabu ya Kaizer Chiefs kama uwanja wao wa nyumbani kwenye michezo ya ligi kuu ya Afrika Kusini PSL pia hutumika kwenye mechi za kimataifa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana pia hutumika kwenye michezo mbali mbali ya klabu bingwa barani Afrika
•
Uwanja huu unaongoza kwa ukubwa barani Afrika ukiwa na uwezo wa kuchukua jumla ya watazamaji Elfu tisini na nne mia saba thelathini na sita [94,736] , pia uliwahi kuweka rekodi ya kujaa zaidi ya idadi inayotakiwa, ilikuwa August 1 mwaka 2015 kwenye mchezo wa Soweto derby ambapo Kaizer Chiefs “Amakhosi” waliwakaribisha Orlando Pirates uwanja huu uliingiza jumla ya watazamaji 94,807
•
Uwanja huu ulifunguliwa rasmi mwaka 1989 na mwaka 2009 ulifanyiwa maboresho kwa kupanuliwa na kuongezwa ukubwa eneo la majukwaa ya watazamaji
•
Mwaka 1996 uwanja huu ulipewa heshima ya kuchezwa fainali ya Afcon ambapo Afrika Kusini walitwaa ubingwa baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Tunisia, pia mwaka 2013 ambapo fainali ilichezwa hapo FNB na Nigeria walipata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burkinafaso
•
Uwanja huu pia ulitumika kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 na fainali ya michuano hiyo ilipigwa kwenye uwanja huo
•
Uwanja huu pia utatumika February 29 mwaka huu kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Afrika Kusini PSL ambapo Orlando Pirates watakuwa wenyeji wa mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs
•
Kihistoria uwanja huu ulikuwa sehemu ya kwanza kabisa ya Hayati Nelson Mandela kufanya mkutano wake baada ya kutoka kifungini gerezani mwaka 1990
Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz











