
Ligi ya Ufaransa (Ligue 1) ndio ligi ambayo imechezwa michezo mingi kwa kila timu hadi sasa, PSG wanaongoza ligi hiyo katika hali ambayo haimshangazi yeyote ambaye amekuwa akiifatilia ligi hii tangu ambapo Olympique Lyon ilitwaa mataji 7 mfululizo.
PSG wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi 2 wakiwa wamewazidi Nantes wanaofuatia kwenye nafasi ya pili huku Angers wakiwa kwenye nafasi ya 3 katika mfululizo wa yale ambayo hatukuyatarajia kuyaona mpaka wakati huu.
Ambacho hakikutarajiwa ni kuona PSG wakiwa wamefungwa mechi mbili hati kufikia wakati huu hali inayoashiria kuongezeka kwa ushindani kwenye ligi hii ambayo ilikuwa ikidharauliwa kwa jinsi ambavyo ilionekana kutawaliwa na klabu moja kwa muda mrefu.
Katika orodha ya mambo ambayo huwezi kuacha kujadili ni nafasi ya Olympique Lyon ambayo tayari wametangaza kuachana na kocha wao Sylvinho baada ya mlolongo wa matokeo mabaya ambayo yamewaacha wanaingia kwenye wiki ya kimataifa wakiwa nafasi ya 14 kwenye ligi baada ya kushinda mechi mbili pekee.
Msimu uliopita Lille wakichagizwa na nyota wao Nicolas Pepe ambaye walimuuza kwenda Arsenal, hakuna mengi yakiyobadilika hadi sasa kwa timu hiyo ambayo imetoa mtu aliyeongoza kwa ufungaji na kwa mara nyingine akiwa mwafrika anayetokea Nigeria Victor Osimhen ambaye hadi sasa amefunga mabao 7 akifuatiwa na Wissam Ben Yedder aliyehamia Monaco akitokea Sevilla, Habib Diallo (FC Metz) na Moussa Dembele (Lyon) wote wakiwa wamefunga mabao 6.
Burudani hii huwezi kupata sehemu yoyote isipokuwa kupitia kingโamuzi cha @StarTimesTz pekee. Ukiwa na kingโamuzi cha Antenna utalipia kifurushi cha UHURU Tsh. 18,000 tu na kingโamuzi cha Dish utalipia kifurushi cha SMART Tsh. 21,000 tu.
#StartimesPekee #MpiraPasiMpiraGoli