YANGA KUPIGA MBILI ZA KIRAFIKI KABLA YA KUIVAA MBAO

Timu ya Yanga imepanga kucheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kukutana na Mbao FC katika mtange wa ligi kuu bara utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba, Oktoba 20.

Yanga itacheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Friends Rangers, Oktoba 12 kabla ya kukutana na Pan African siku nne baadae.

Msemaji wa timu hiyo, Antonio Nugaz amesema mechi hizo ni kwa mujibu wa matakwa ya kocha wao mkuu Mwinyi Zahera ambaye amekwenda nchini Kongo kwa majukumu ya timu ya Taifa. “Tutakuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Friends Rangers na Pan Afrika kabla ya timu kwenda jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbao. Mwalimu ametaka mechi hizi ili kukiweka fiti kikosi chake,” alisema Nugaz.

Baada ya mchezo dhidi ya Mbao, Yanga itaanza maandalizi ya mchezo wa mchujo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri ambao utachezwa Oktoba 27, uwanja wa Taifa.

#wapendasokaupdates

Bodi ya ligi kufanya uchaguzi mdogo

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi katika Shirikisho la Tanzania , TFF Malangwe Mchungahela amesema kutakuwa na uchaguzi mdogo katika Bodi ya Ligi (TPLB) utakaofanyika Desemba 7 mwaka huu ili kujaza nafasi sita zilizo wazi.

Nafasi zilizo wazi ni wajumbe watatu kutoka vilabu vya ligi kuu, wajumbe wawili kutoka vilabu vya ligi daraja la kwanza na mjumbe mmoja kutoka ligi daraja la pili.

Akizungumza na wanahabari Mchungahela amesema mchakato wa kutangaza nafasi za wagombea umeanza leo huku zoezi la kuchukua fomu likianza Oktoba 12 mpaka Oktoba 16.

Amesema mgombea ni lazima awe Mwenyekiti/Rais wa klabu ya ligi kuu, ligi daraja la kwanza na ligi daraja la pili.

Pyramids wapinzani wa yanga ni balaa

Timu ilianzishwa miaka 11 iliyopita 2008 ikijulikana Kama Al Assiouty Sport. 2014 walipanda ligi kuu ya Misri,2018 ilinunuliwa na Mwenyekiti wa makampuni ya Saud Sport Authority na kubadilisha jina kutoka Al Assiouty Sport na kua Pyramids FC.

Juni mwaka huu mfanyabiashara toka Emirate Salem Al alifanikiwa kua mmiliki wa timu hii baada ya kununua hisa zote na kuwekeza pesa nyingi.

Kwa Sasa inafundishwa na Kocha Sebastian Desabre aliyewai kua kocha wa timu ya Taifa Uganda 2017-2019 raia wa ufaransa. Ni kocha mzoefu Africa amewai kufundisha vilabu vikubwa barani Africa Kama Esperance ya Tunisia ,Asec mimomasa ,Libolo ,waydad Casablanca Morroco na Ismaily.

Msimu uliopita kwa mara ya kwanza walishika nafasi ya Tatu katika ligi kuu ya Misri nyuma ya mabingwa Al Ahly na Zamaleck hivyo kupata tiketi ya kuwakilisha Misri michuano ya Confederation cup msimu huu.

Hatua ya awali walikutana na Etoile du Congo ya Congo na waliitoa kwa kujumla ya magoli 5-1 mechi ya kwanza Misri wakitoka 4-1 na marudiano Congo wakishinda 1 kwa bila.

Hatua inayofuata walikutana na CR Belouizdad ya Algeria na waliitoa kwa jumla ya magoli 2-1 mechi ya awali nchini Misri wakitoka 1-1 na mechi ya marudiano Pryamids fc wakishinda goli 1 kwa bila na kufuzu hatua ya Play off.

Takwimu zinaonyesha katika michuano hii ya CAF wameshinda mechi zote ugenini na moja nyumbani na kutoka sare moja nyumbani hivyo ni timu inayoweza kutoa matokeo ugenini.

Kocha wa zaman Al Ahly Hossam El Badry ndie Mwenyekiti wa klabu Msemaji wao pia ni Mchezaji wa zaman Misri.

Ikiwa hii ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano chini ya CAF, wanaowachezaji kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo John Attwa toka Ghana.

Pointi nne zaiondoa lipuli fc kileleni

Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Herman Haruna, amesema, walitamani kukaa kileleni mwa ligi bila kushuka lakini kupoteza pointi nne za michezo miwili waliyotoka sare kuliwagharimu

Lipuli ilianza msimu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kisha kuongoza ligi kwa muda kabla ya kuiachia nafasi hiyo kwa Kagera Sugar ambayo baadae nayo ikaikabidhi kwa Simba

Lipuli ililazimishwa sare kwenye michezo dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons

Inashika nafasi ya nne ikiwa imejikusanyia alama nane baada ya kushuka dimbani mara nne

Aussems kuitwngeneza simba mpya

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema michezo mitatu ya kirafiki wanayotarajia kucheza, ataitumua kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha kwanza

Aussems ambaye kikosi chake Jumamosi kitashuka uwanja wa Taifa kuikabili Bandari Fc, amesema mchezo huo ni sehemu ya mazoezi kwa vijana wake

“Tunawakosa wachezaji saba ambao wako timu za Taifa hivyo sio mchezo ambao tunaweza kuutumia kujiimarisha kimbinu,” amesema

“Ni mchezo wa mazoezi ambao nitautumia kuwapa wachezaji wengine nafasi ya kucheza”

Simba imeendelea kujifua uwanja wa Gymkhana hata hivyo mazoezi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara yamekuwa yakiathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Aussems amesema hilo linaweza kuwaathiri vijana wake Jumamosi kwani wamekosa muendelezo wa program za mazoezi kutokana na mvua hizo

Baada ya mchezo huo Simba itaelekea mkoani Kigoma, Oktoba 14 ikitarajiwa kucheza na Mashujaa Fc kisha kukamilisha ratiba yake kwa kucheza na Aigle Noir Oktoba 16 hukohuko Kigoma

Dante aendeleza mgomo yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umemshukia beki wake Andrew Vicent ‘Dante’ ambaye amekataa kurejea kambini akishinikiza alipwe fedha anazoidai klabu hiyo

Msemaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema pamoja na uongozi wa timu hiyo kuwa tayari kumlipa kwa awamu fedha anazodai zinazofikia Tsh Milioni 40, beki huyo amegoma kurejea kikosini

“Yanga tulikuwa tayari kumlipa kwa awamu tatu, Mil 15 mara mbili kisha kumalizia Mil 10”

“Yeye si mchezaji pekee anayeidai Yanga, wengine tumefanya nao makubaliano ya aina hiyo, wamekubali”

“Lakini Dante anaikosea Yanga kwa kuwa ameendelea kupokea mshahara bila ya kufanya kazi”

“Madai yake alipaswa kuyafanya huku akiwa kazini. Huo ndio utaratibu wa kazi mahali popote”

“Yeye kama hataki mpaka alipwe fedha zake kwa nini anaendelea kupokea mshahara wakati anajua hafanyi kazi?”

“Tayari wapo wanaohoji hatua hiyo kuwa pengine kuna mpango umejificha kama ule wa Beno, pengine dirisha dogo anataka kujiunga na timu nyingine. Sisi viongozi tunayajua ya ndani tu lakini ya huko nje nyie mashabiki mtakuwa mnayafahamu zaidi,” alisema Nugaz

Dante amegoma kujiunga kikosi Yanga akishinikiza alipwe huku mwenzie Juma Abdul ambaye alikuwa na madai, amekubali kurejea kikosini na anapokea malipo yake kwa awamu

Beki huyo kisiki hakujiunga kabisa na Yanga msimu huu akianza kwa kukosa maandalizi ya mwanzo wa msimu yaliyofanyika mkoani Morogoro

Yanga tunaifahamu pyramid vizuri

“Tunafahamu ni timu iliyoanzishwa mwaka 2008. Msimu uliopita ilimaliza nafasi ya tatu ligi kuu ya Misri na hivyo kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho,” amesema
.
.
“Pia tunafahamu katika mechi zao nne za kombe la Shirikisho mpaka kufika hatua hii, wameshinda mechi mbili ugenini, sare na ushindi nyumbani”
.
.
“Ni timu yenye utajiri mkubwa, mapema mwaka huu tunafahamu ilinunuliwa na matajiri kutoka Arabuni”
.
.
“Lakini hilo halitutishi Yanga kwa sababu tunafahamu hii ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano ya Kimataifa”
.
.
“Miaka ya hivi karibuni tumecheza Misri na vilabu vya Al Ahly na Zamalek na tulitoa ushindani mkali. Hivyo sisi hatuzihofii kabisa timu kutoka Misri”
.
.
“Kwa sababu tumeshamfahamu mpinzani wetu, tutaboresha ratiba yetu ya maandalizi ili kuhakikisha tunakuwa tayari kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumba ambao utapigwa Oktoba 27” ~ HASSAN BUMBULI (Msemaji Wa Yanga)

@yangasc @hbumbuli
#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started