Uchaguzi mwenyekiti simba bado

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kuwa bado Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo haujakutana kujadili suala la Mwenyekiti mpya baada ya Swedi Mkwabi kuachia ngazi hivi karibuni

Mkwabi alijiuzulu nafasi yake mwezi uliopita akitoa sababu ya kuhitaji muda zaidi kusimamia shughuli zake binafsi

Kulingana na Katiba ya Simba, mchakato wa kujaza nafasi yake unapaswa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu

Simba yapanda viwango CUF

Pamoja na kutolewa mapema michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba imeendelea kuziburuza timu za Tanzania na Afrika Mashariki kwenye viwango vya soka barani Afrika baada ya kupanda kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 20 hadi ya 16

Ni Gor Mahia pekee iliyoingia top 30 miongoni mwa timu kutoka ukanda wa Afrika Mashabiki ikiwa inashika nafasi ya 19

Hata hivyo viwango hivyo vitabadilika baada ya michuano ya mwaka huu ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Massimiliano Allegri kumrithiOle Gunnar manchester united

Kocha wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri amewaambia Manchester United kama watamwitaji kuchukua mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari lakini inabidi wafanye haraka kumtimua kocha huyo.

Allegri kwa sasa hana kazi tangu alipoachana na Juventus msimu uliopita baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka mitano na kuipa mafanikio ya kutawala soka la nchini Italia.

Kwa sasa, Manchester United wapo nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kucheza michezo nane, wameshinda miwili, sare tatu na kufungwa mara tatu.

Allegri mwenye umri wa miaka 52 anafukuzia kwa ukaribu nafasi hiyo, kilisema chanzo kutoka katika kituo cha Gazzetta dello Sport cha nchini Italia.

Lakini, anachokitaka kocha huyo Manchester United wafanye uamuzi wa haraka kumfukuza Solskjaer ambaye alisaini mkataba wa miaka mitatu Machi, mwaka huu.

Tetesi za usajili balani ulaya

Manchester United wameafikiana makubaliano ya maongezi ya kumsajili mwezi Januari mshambuliaji wa Croatia na klabu ya Juventus Mario Mandzukic, 33. (Tuttosport, via Mirror)

Lyon wameshindwa mipango yao ya kumsajili kocha wa zamani wa Chelsea na Manchester United Jose Mourinho. Kocha huyo mwenye mika 56 raia wa Ureno anataka kurejea kwenye ligi ya Primia ya England. (Mirror)

Klabu ya Fenerbahce ya Uturuki inaaminika kuanza mazungumzo na Arsenal juu ya kumsajili kwa mkopo mwezi Januari kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim, via Sun)

Ozil ana wasi wasi kuwa hatacheza tena katika klabu ya Arsenal. (Mirror)

Mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 30, hana furaha baada ya kupunguziwa muda wa kucheza katika klabu yake ya Bayern Munich na amekiri kuwa anaweza kusaka timu ya kuhamia mwezia Januari. (Kicker, via Mail)

Mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 32, na beki wa Brazil Thiago Silva, 35, wanaweza kuondoka bure kutoka klabu ya Paris St-Germain mwishoni mwa msimu. (ESPN)

Kiungo wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 31, ambaye alikuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Manchester United msimu uliopita, amesema kuwa huenda akaihama klabu yake ili kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. (Mail)

Leeds wanapanga kumsajili kocha wa Rangers ya Uskochi Steven Gerrard endapo kocha wao Marcelo Bielsaataihama klabu. (Football Insider)

Manchester United wanapanga kumsajili kiungo Francisco Sebastian Cordova, ambaye anachezea klabu ya America ya Ligi Kuu nchini Mexico. Kiungo huyo mwenye miaka 22 ambaye ameichezea timu ya taifa lake kwa mara ya kwanza juma lililopita pia anatakiwa na Sevilla na Benfica. (Mail)

Mcezaji mmoja mwandamizi wa Manchester United aliandaa mlo katika moja ya mgahawa kwa kikosi kizima lakini ni wachezaji watano tu ndio waliokwenda.. (ESPN)

Juventus na Napoli wanamnyemelea mshambuliaji kinda wa klabu ya Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway striker Erling Haaland, 19, ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa vilabu vya Nottingham Forest, Leeds na Manchester City Alf-Inge Haaland. (Corriere dello Sport – in Italian)

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger anaamini Bayern Munich “walimlaghai” mshambuliaji wa Ujerumani Serge Gnabry, 24, ili kuihama Arsenal mwaka 2016. (Goal.com)

Mlinzi wa England Harry Maguire, 26, anaamini usajili wake wa pauni milioni 80 ulikuwa ni “dili nzuri” baina ya vilabu vya Manchester United na Leicester. (Leicester Mercury)

BBC

Iran 🇮🇷 yatoa kipigo bila huruma 14-0

Timu ya taifa ya Iran 🇮🇷 iliichapa Cambodia 🇰🇭 kipigo bila huruma cha Magoli 14-0 katika mchezo wao wa kufuzu Kombe la Dunia 2022 Jana siku ambayo wanawake waliruhusiwa rasmi kutazama mechi kwa mara ya kwanza katika miaka takribani 40.

– Magoli Manne kutoka kwa Karim Ansarifard, hat-trick kutoka Sardar Azmoun na Magoli Mawili kutoka kwa Mehdi Taremi na Mohammad Mohebi yalitosha kuwapa ushindi huo mbele ya Cambodia, ingawa matokeo hayatakuwa na umuhimu mkubwa sana, jambo la kihistoria ilikuwa ni mahudhurio ndani ya uwanja..

– Wakati wanawake wachache walitazama mchezo wa soka kwa wanaume hapo awali, walikuwa wakiteuliwa na viongozi; Lakini hii ilikuwa mara ya kwanza wanawake kuruhusiwa kununua tiketi kwa uuzaji wa jumla…Karibu tiketi 3,500 ziliuzwa kwa sehemu maalum ya wanawake kwenye mchezo huo, ambapo sehemu yao ya kukaa ilijaa saa tu kabla ya mechi kuanza..
#WorldCupAFCQualification #Iran
@Harunlugoyah

Mabingwa wa.dunia ufaransa kuwakabiri Iceland leo

Iceland wameshinda michezo yote mitatu wakiwa nyumbani katika Kundi H lakini wanakabiliwa na timu bora zaidi ya Ufaransa ambao wameshinda mechi 5 kati ya 6 za mwisho, wakifunga mabao 19.

Iceland wataitaji ushindi na kwa faida ya uwanja wa nyumbani wana tishio la kuwaumiza France ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye majeraha kwenye timu 🚑: Laporte, B. Mendy, Dembele, Martial, Mbappe, F. Mendy, Sakho, Pogba, Thauvin, Lloris, Dubois, Umtiti

Endelea kufuatilia mechi hizi kupitia StarTimes. Pia waweza angalia kupitia App 📱 cheki link kwenye bio ya @startimestz

Mabingwa wa euro ureno kutafuta upenyo wa.kishiriki EURO 2020 leo

#EuroQualifiers2020 ndani ya @StarTimesTz
🇵🇹 Portugal 🆚 Luxembourg 🇱🇺
⌚21:45
🏟 Jose Alavalade
📺 ST Sports Focus

Mabingwa watetezi wa kombe la Euro, timu ya Portugal wanashika nafasi ya pili kwenye Kundi B. Wako alama tano nyuma ya Ukraine inayonolewa na kocha Andrey Shevchenko.

Luxembourg wamejikusanyia pointi 4 licha ya kuwa katika kundi ngumu. Waliipiga Lithuania 2-1 nyumbani na kutoka sare 1-1. Lakini, timu ya Portugal inatarajiwa kupata ushindi vizuri kutokana na ubora wa kikosi kilichopo

Mechi hii utaipata kupitia @StarTimesTz channeli ya Sport Focus, pia waweza angalia kupitia App ya Startimes 📱 cheki link kwenye bio ya @startimestz

#MpagoniSoka
#StartimesPekee

Czech Rep 🆚 England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 nani kuondoka mbabe

#EuroQualifiersOnStartimes
🇨🇿 Czech Rep 🆚 England 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿
⌚ 3:45 usiku
🏟 Eden Arena
📺 ST World Football

England ilishinda 5-0 walipokutana dhidi ya Czech pale Wembley mapema mwaka huu-lakini unatarajiwa kuwa mpambano mgumu watakapo cheza ugenini leo dhidi ya Czech pale Prague

England walipocheza na Czech nyumbani, Raheem Sterling alifunga hat-trick, wakishinda 5-0, ingawa timu ya Czech baada ya kipigo hicho imeshinda mechi tatu kati ya nne zilizopita

Ushindi utaiwezesha England iongoze kwa tofauti ya alama sita kwenye kundi A

Mechi hii utaipata kupitia #StarTimes channeli ya World Football, pia waweza angalia kupitia App 📱 cheki link kwenye bio ya @StarTimesTz

#MpagoniSoka
#StartimesPekee

Design a site like this with WordPress.com
Get started