



Mechi namba 19: Coastal Union 2 v KMC 0- Klabu ya KMC imetozwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na timu yake kutoingia vyumbani wakati wa mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa Septemba 13, 2019 katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 24: Alliance FC 1 v Biashara United 1- Klabu ya Alliance imetozwa faini ya jumla ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kutokana na vurugu za washabiki wake pamoja na kufanya vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 20, 2019 Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Nayo klabu ya Biashara United imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kufanya vitendo vinavyoashiria imani ya ushirikiana wakati ikiingia uwanjani. Adhabu zote ni kwa mujibu wa Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Mechi namba 40: Kagera Sugar 0 v Simba 2- Mchezaji Zawadi Mauya wa Kagera Sugar amepewa Onyo kutokana na kitendo chake cha kumpiga mateke mchezaji wa Simba kwenye mechi hiyo iliyochezwa Septemba 26, 2019 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Adhabu dhidi yake ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Naye Mwamuzi wa mchezo huo Emmanuel Mwandembwa amepewa Onyo kwa kumuonesha Mauya kadi ya njano badala ya nyekundu kwa kitendo chake ambacho kilikuwa cha makusudi na kujirudia.
Mechi namba 41: Singida United 0 v Alliance FC 2- Klabu ya Alliance imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kumweka kwenye benchi la ufundi Meneja ambaye hakutambulishwa katika kikao cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) wakati wa mechi hiyo iliyofanyika Septemba 28, 2019 Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 44: Lipuli FC 2 v Tanzania Prisons 2- Klabu ya Tanzania Prisons imetozwa faini ya sh. 3,000,000 (milioni tatu) kutokana na basi lililobeba wachezaji wa timu hiyo kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 29, 2019 Uwanja wa Samora mjini Iringa. Adhabu imezingatia Kanuni ya 14(49) kuhusu Taratibu za Mchezo.

Romelu Lukaku sasa amefunga mabao kwenye timu ya taifa sawa na Thierry Henry …huku akiwa na pungufu ya michezo 40! 😲
Romelu Lukaku
Mechi 83
Mabao 51
Thierry Henry
Mechi 123
Mabao 51
Nani mkali? Namba zinaongea☝
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imezuia baadhi ya viwanja kutumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutokana na kuwa na upungufu katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la kuchezea (pitch) na uzio wa ndani unaotenganisha wachezaji na washabiki (fence).
.
.
Viwanja hivyo ni Kinesi Bull (Dar es Salaam), Bandari (Dar es Salaam), Jamhuri (Morogoro), Namfua (Singida), na Mkwakwani (Tanga). .
.
.
Klabu ambazo timu zao zinatumia viwanja hivyo zimepewa nafasi ya kufanya marekebisho kipindi hiki ambacho Ligi zimepisha mechi za kirafiki za FIFA au kuchagua viwanja mbadala vyenye sifa.Vilevile klabu zimekumbushwa kuwa kwa mujibu wa kanuni, zinapaswa kupeleka viwanjani gari ya wagonjwa badala ya gari yenye kitanda kwani kanuni ya 14(2) imetaja ambulance na si gari lolote.
.
.
“Wasimamizi wa mechi vituoni wanatakiwa kuhakikisha ambulance zinapokuwepo viwanjani kama ilivyoelekezwa kikanuni. Kama huduma ya ambulance haitokuwepo wanatakiwa kuzuia mechi kuchezwa”, imeeleza taarifa iliyotolewa na kamati hiyo. .
.
Powered by @upholstery_designsco

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya saa 72) imetoa adhabu mbalimbali kwa baadhi ya vilabu vya ligi daraja la kwanza ikiwemo kuwapeleka kwenye kamati ya nidhamu baadhi ya wachezaji na viongozi wanaotuhumiwa kuwapiga waamuzi katika mechi mbili tofauti.
Mechi namba 10B, Geita Gold FC 1-0 Rhino Rangers: Meneja wa Rhino Rangers, Ali Rhumba amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF akidaiwa kumpiga Mwamuzi Msaidizi Omari Mataka na kumjeruhi chini ya jicho katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 21, 2019 kwenye Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Nao wachezaji wa Rhino Rangers (Simon Joseph Kiula jezi no. 5 na Julius Elias Masunga jezi no. 26) wanapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa tuhuma za kuwarushia mawe waamuzi baada ya kumalizika mechi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Bodi ya Ligi, polisi waliokuwa uwanjani walijitahidi kupambana licha ya kupata upinzani kutoka kwa wanajeshi kadhaa waliombatana na Rhino Rangers.
Mechi namba 17B, Pamba SC 1-2 Geita Gold FC: Meneja wa Pamba SC, Jafari Juma amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF akidaiwa kumpiga ngumi mwamuzi, tukio lililosababisha askari polisi wamuweke chini ya ulinzi katika mechi hiyo iliyofanyika Septemba 28, 2019 kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Mechi namba 12B, Sahare All Stars 1-1 Green Warriors: Kipa wa Green Warriors, Shabani Dihile amepewa onyo kali kwa kutoa shutuma dhidi ya waamuzi kuwa walichezesha kwa maelekezo ya viongozi mechi hiyo iliyochezwa Septemba 22, 2019 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. .
.
Powered by @upholstery_designsco
Uongozi wa @yangasc umethitbisha kuwa mchezo wake wa Kombe la Shirikisho barani Afrika #CAFCC dhidi ya Pyramids FC kutoka Misri utapigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, Oktoba 27 mwaka huu. Sababu bado hazijawekwa bayana.
Je, nini maoni yako?
Powered by @upholstery_designsco

Timu ya Taifa @taifastars_ leo jioni imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Amahoro nchini Rwanda kujiandaa na mchezo wa Kirafiki dhidi ya Rwanda utakaochezwa Oktoba 14,2019 Kigali ambao ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wa marudiano kufuzu CHAN dhidi ya SUDAN Oktoba 18,2019..
#CHAN2020Qualifiers #FriendMatch



Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameshinda tuzo ya kocha bora wa mwezi Septemba
#wapendasokaupdates
#PL
#PLAwards

Mshambuliaji wa Arsenal Pierre Emerick Aubameyang ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba baada ya kucheza michezo minne na kufunga magoli 5
#wapendasokaupdates
#PL
#PLAwards

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha kuwa utawaongeza wachezaji sita wa timu ya vijana kwenye kikosi cha kwanza kuelekea michezo mitatu ya kirafiki ambayo Simba itacheza hivi karibuni
Taarifa iliyotolewa na uongozi imesema, uamuzi huo umechukuliwa baada ya timu kuwa na wachezaji wachache idadi kubwa ya wachezaji wakienda kutumikia timu za Taifa
Wachezaji hao watashiriki kwenye michezo yote mitatu ambayo itapigwa;
Jumamosi Oktoba 12, 2019 (vs Bandari FC – Kenya)
Jumatatu Oktoba 14, 2019 (vs Mashujaa FC) na
Jumatano Oktoba 16, 2019 (vs Aigle Noir – Burundi).