
– Mkenya Eliud Kipchoge ameweka jina lake katika vitabu vya historia , akimaliza kilomita 42 za mbio za marathon kwa saa moja dakika 59 na sekunde 40 katika shindano la Ineos siku ya Jumamosi nchini Austria Vienna… Hatahivyo muda huo bora uliowekwa na bingwa huyo hautatambulika kama rekodi ya dunia.
…
– Kulingana Shirika la Riadha duniani IAAF , kwa mbio yoyote kufikia sheria zake na hivyobasi kutambulika kama rekodi ya dunia kuna masharti yanayopaswa kufuatwa kulingana na chombo cha habari cha AFP.
1️⃣ Kwanza mbio hizo lazima ziwe zimeandaliwa na shirika la riadha duniani IAAF ama shirikisho la raidha la nchini ambapo riadha hizo zinaandaliwa.
2️⃣ Wanariadha wanaodhibiti kasi hawawezi kuingia katika mbio hizo kwa zamu na kutoka.
3⃣ Lazima wanariadha wafanyiwe vipimo vya matumizi ya dawa za kusisimua mwili.
4⃣ Vinywaji vinapaswa kutoka kwa vituo rasmi na sio kupewa mwanariadha na wasimamizi wake.
5️⃣ Ni Sharti kuwepo zaidi ya washindani watatu katika mbio hizo.
6️⃣ Mwanariadha hafai kudhibitiwa kasi na gari lililopo mbele yake.
7️⃣ Njia itakayotumika ni sharti ifanyiwe ukaguzi na kupimwa na maafisa wa IAAF.
…
– Siku ya Jumamosi, Kipchoge alipewa vinywaji kila baada ya kilomita 5 na hivyobasi kukiuka sheria hizo za shirikisho la riadha duniani…. Kulingana na AFP , barabara hiyo ilikuwa imeandaliwa hali ya kwamba ingemchukua Kipchoge sekunde 4.5 zaidi kulingana na uchanganuzi wa wataalam wa michezo katika chuo kikuu cha Vienna.
Kwa jumla aliweza kushuka mita 26 na kupanda mita 12 , walisema wataalam hao.
Mbio hizo za Viena hazikuwa mashindano bali zililenga kuwapa motisha mamilioni ya watu duniani. Na Kipchoge amefanikiwa.
..
– Mkimbiaji huyo mwenye umri wa miaka 34 tayari anashikilia rekodi ya dunia miongoni mwa wanaume katika umbali huo akiwa na muda wa saa mbili dakika moja na sekunde 39, ambao aliweka katika mbio za Berlin tarehe 16 mwezi Septemba 2018.
#ELiud159 #NoHumanIsLimited #EliudKipchoge #IneosChallenge

















