Urusi πŸ‡·πŸ‡Ί Taifa la tatu kufuzu EURO 2020

✍🏻 Timu ya taifa ya Urusi πŸ‡·πŸ‡Ί imekuwa timu ya tatu huku Timu ya taifa ya Poland πŸ‡΅πŸ‡± imekuwa timu ya Nne kufuzu kucheza Michuano ya EURO 2020.. Ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Cyprus πŸ‡¨πŸ‡Ύ uliwahakikishua Warusi kuwa nafasi ya kwanza katika kundi I, huku Poland nao wakimaliza kinara wa Kundi G baada ya Ushindi wao wa 2-0 mbele ya Macedonia πŸ‡²πŸ‡°!..

– Urusi waliomaliza robo fainali ya Kombe la Dunia waliongoza kupitia kwa Denis Cheryshev kabla ya Magomed Ozdoyev kuongezeka goli la pili mpaka Mapumziko, mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Artem Dzyuba, Aleksandr Golovin na la pili kutoka kwa Cheryshev yalitosha kuwafanya kuwa na pointi 21 Katika kundi lao… Poland waliomaliza na Pointi 19, walipata magoli yao kupitia kwa Frankowski na Arkadiusz Milik na Assist zote za Roberto Lewandowski yalitosha kuwapeleka EURO 2020!..
..
✍🏻 Ubelgiji Kinara wa Kundi I na Italia kinara wa Kundi J, pia ni Miongoni mwa Mataifa ambayo tayari yamefuzu kwa mashindano hayo ya msimu ujao wa kiangazi..
#EURO2020Qualifiers #EURO2020Q
@Harunlugoyah

Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ yatwaa kombe mataifa ya magharibi

✍🏻 Timu ya taifa ya Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ imeshinda Kombe la Mataifa ya Afrika Magharibi (WAFU) baada ya kuichapa timu ya taifa ya Ghana πŸ‡¬πŸ‡­, 3-1 kwa changamoto ya mikwaju ya Penati…. Fainali hiyo Kali kwenye dimba la Stade Lat-Dior iliisha bila kufungana katika muda wa dakika 90, lakini timu zote mbili zilipata bao katika kipindi cha pili cha muda wa ziada.
..
✍🏻 Akitokea Benchi kipindi cha pili, Youssouph Badji alifunga bao la kwanza kwa Senegal dakika ya 107 lakini, Joseph Esso dakika mbili baadaye aliisawazishia The Black Stars… Dakika 120 zilimalizika kwa sare ndipo Penati zikaamua Wenyeji Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ kuwa Mabingwa kwa Mara ya Kwanza mbele ya Mabingwa wa Kihistoria wa Michuano hii, Ghana πŸ‡¬πŸ‡­ ambao Wachezaji wake waliiga Mtindo wa Kupiga Penati wa Jorginho wa Chelsea, lakini ikawaponza πŸ˜†πŸ˜‚!..

✍🏻 Nahodha wa Ghana, Shafiu Mumuni alimaliza kama mfungaji bora wa mashindano na mabao yake Manne akiwa ndio Mchezaji wa kwanza katika historia ya Michuano hii kufunga hat-trick, wakati Jean Moustet wa Guinea alipewa tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mashindano..
#WAFU #WAFU2019Final #WAFUCupOfNations2019
@Harunlugoyah

πŸ‘‰πŸ» Fainali mbili kwenye Shindano Moja πŸ€”… Huko Afrika Magharibi (WAFU Cup of Nations). …

✍🏻 Jana ilipigwa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Magharibi (WAFU Nations Cup) na Senegal πŸ‡ΈπŸ‡³ ilishinda baada ya kuichapa timu ya taifa ya Ghana πŸ‡¬πŸ‡­, 3-1 kwa changamoto ya mikwaju ya Penati..

✍🏻 Juzi Ilipigwa fainali nyingine huko huko Afrika Magharibi inayoandaliwa pia na WAFU inayojulikana kama “Plate Cup/ Plate Competition” na fainali yake ni Plate Final, hiyo Bingwa ni Guinea πŸ‡¬πŸ‡³ baada ya kuwalaza Cape Verde πŸ‡¨πŸ‡» pia kwa mikwaju ya Penati 4-3..

✍🏻 Kabla ya kuanza kwa Michuano hii, Mataifa yote 16 Wanachama, wanaingia katika hatua ya Mchujo, Mataifa Nane yatakayoshinda mechi zao yataingia kushiriki WAFU Nations Cup hatua ya Robo fainali… Huku Mataifa Mengine Nane yatakayopoteza mechi zao ndio yanaangukia huko Plate Cup ambapo inaanzia hatua ya Robo fainali..
#PlateCupFinal #WAFUCupOfNations2019
@Harunlugoyah

✍🏽 SAUTI ZA MASHABIKI HURU WANAWAKE HUKO IRAN MATOKEO NI 14-0.

.

✍ Baada ya miaka 40 hatimae wanawake waliruhusiwa ingia uwanjani nchini IRAN.
.
✍ Furaha ilikuwa maradufu IRAN iliposhinda goli 14 – 0 dhidi ya COMBODIA pale Azadi Stadium, mjini Tehran, kuwania tiketi ya kufuzu World Cup 2022.
.
✍ Tiketi 3500 ziliuzwa na kuisha ndani ya lisaa moja, na ata nyongeza ya tiketi 1100 pia ziliisha. Japo wanawake wote walitengewa jukwaa lao pekee πŸ˜”, ila hiyo haikuzuia furaha, walishangilia kwa nguvu wakiwa wima mithiri ya “Yellow Wall” πŸŒ“ pale Signal Iduna Park.
.
✍ Ikiwa ni baada ya mwezi kupita tu tangu mshabiki wa kike kujichoma moto nje ya mahakama Tehran nchini IRAN ilipojua anawezaa pewa hukumu ya kifungo baada ya kuingia uwanjani akiwa amevalia nguo za kiume πŸ˜­πŸ˜”, hii moja kati ya matukio ya kusikitisha, FIFA waliingilia kati na kutishia kuwafungia IRAN.
.
✍ Binti aliejichoma moto Sahar Khodayar “Blue Girl” aliekuwa mshabiki wa timu ya Esteglal FC inayotumia rangu ya blue. Ni tukio linalosikitisha ila limeleta ukombozi. Japo haijafahamika kama uhuru huu ni wakudumu au la.
.
✍ Tukio hilo la wanawake wa Iran uwanjani wakishangilia, selfie 🀳🏻 za kutosha, passion, machozi ya furaha, uku wengine wakiwa na mabango ya “Blue Girl” kumuenzi shujaa, na ushindi mpana wa goli 14 ni tukio bora zaidi la wiki kwangu.
.
✍ Chukua hii… Uhuru ni chanzo cha furaha na michezo ni furaha so michezo yataka uhuru, hii ni hesabu rahisi tu si kama ile if X=Y and Z=Y so Z=X, Ohooo wanangu wa backbenches hapa nshaanza waacha πŸ˜πŸ˜‚
.
✍ Mkali wa Raggae na mpenzi wa soka Bob Marley aliwahi kusema “Football is Freedom”. Nasikia Bob Marley akicheza mpira alikuwa Midfielder General mpira ulimtii bila shuruti ⚽
.
✍ Oya wanangu wa vijiweni niwaache na mistari ya Bob Marley – Redemption Song….. “emanticipate yourself from mental slavery, none but ourselves can free our minds”. Muwe na Jumapili huru na yenye furaha.
.
✍ Imeandikwa na mpenda watoto wa kiarabu kutoka Iran πŸ˜‚πŸ˜€.
.
✍ Daniel Mtani Thomson
@danirito_thomson

John McGinn amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga Magoli Matatu yaani hat-trick katika Kipindi cha kwanza

1952 – John McGinn amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga Magoli Matatu yaani hat-trick katika Kipindi cha kwanza kwa timu ya taifa ya Scotland tangu mara ya mwisho Lawrie Reilly katika mechi ya Kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Marekani πŸ‡ΊπŸ‡Έ, April 1952… Miaka 67 na Siku 166 zilizopita..

– Mpaka kufika sasa, John McGinn ndio Mchezaji wa 33 tofauti kufunga hat-trick katika timu ya taifa ya Scotland… Hakuna Mchezaji aliyeifungia Hat-trick Scotland kati ya Mwaka 1970 mpaka 2014.. Kuna hat-trick tano tu tangu 2015 mpaka Sasa!..
#Scotland #EURO2020Qualifiers
@Harunlugoyah

πŸ‡°πŸ‡ͺ REKODI mpya kwenye ulimwengu wa MARATHON πŸ† πŸ‡°πŸ‡ͺ

Siku moja baada ya mafanikio ya kushangaza ya Eliud Kipchoge, binamu yake Brigid Kosgei mwenye miaka 25 anaandika rekodi mpya kwenye Chicago Marathon, kakimbia km 42 katika muda wa saa 2, dakika 14 na sekunde 4.

Anavunja rekodi iliyodumu zaidi ya miaka 16 ikishikiliwa na mwanamama Paula Radcliffe ambaye alikuwa wa kwanza kumpongeza baada ya kumaliza mbio hizo.

Paula Radcliff πŸ—£”Siku zote nilijua siku hii itafika.”

Design a site like this with WordPress.com
Get started