




GoalKeeper:
Kimenyi Yves (Rayon Sports)
Defenders:
Omborenga Fitina (APR)
Imanishimwe Emmanuel (APR)
Rugwiro Herve (Rayon Sports)
Manzi Thierry(APR)
Medifielders:
Imran Nshimiyimana(Rayon Sports)
Niyonzima Olivier Seif(APR)
Nsabimana Eric (AS Kigali)
Niyonzima Haruna(As Kigali)
Strickers:
Kagere Meddie(Simba)
Tuyisenge Jacques(Petro Atletico)
.
.
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Klabu ya Fc Barcelona inatarajia kuingia sokoni mwisho mwa msimu huu kuwania saini ya mrithi wa Luis Suarez ambaye umri wake umemtupa mkono
.
.
Kwa mujibu wa Daily Express Barca wanatarajia kufanya usajili wa mmoja wa washambuliaji wakubwa katika Ligi Kuu England au Ufaransa
.
.
Kwenye Orodha ya wachezaji hao ni pamoja na Kylian Mbappe, Harry Kane au Roberto Firmino.
.
.
Unafikiri kwa namna Barcelona ilivyo nani anaweza kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wao?

– Mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Mbao FC dhidi ya Yanga SC sasa itapigwa Oktoba 22 badala ya Oktoba 24 iliyokuwa imepangwa awali katika dimba lilelile la CCM Kirumba jijini Mwanza.
…
– Baada ya mchezo huo Yanga itakuwa na kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids ya Misri kwenye uwanja huo huo Oktoba 27, 2019.
#VPLUpdates🇹🇿 #VPL

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Brescia, MARIO BALOTELLI anaripotiwa kuongezewa mshahara mara 3 ikiwa atafikisha mabao 15 ya Serie A msimu huu.
Balotelli mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na klabu hiyo ya nyumbani alikozaliwa mwanzoni mwa msimu huu baada ya klabu ya Brescia kupanda daraja msimu huu.
Inaaminika kuwa Balotelli analipwa karibia £ 870,000 kwa mwaka baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu.. Hivyo kama Balotelli atafikisha mabao 15 ataanza kulipwa £ 2.6M (Bilioni 7.5) kwa mwaka.

Klabu ya Sporting Lisbon (Ureno) inafikiria kubadili jina la uwanja wake na kuupa jina la nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo, kulingana na taarifa ya Rais wa klabu hiyo Frederico Varandas.
Uwanja wa nyumbani wa Sporting uitwao Estadio Jose Alvalade, ulipewa jina la mwanzilishi wa klabu hiyo Jose Alvalade tangu 1956 lakini ripoti zinasema Sporting inafikiri kubadili jina na kuupa jina la mchezaji waliyemlea katika Academy yao na na baadaye kucheza katika kikosi cha kwanza kabla hajaondoka kwenda Manchester United (2003)
Uwanja wa Estadio Jose Alvalade wenye uwezo wa kubeba mashabiki 50,000 unaweza kubadilishwa jina lake na kuitwa “Cristiano Ronaldo Arena au CR7 Arena”
•
“Cristiano yupo na atazidi kuwa moja ya alama kubwa ya historia ya kilabu yetu”-Rais wa Sporting Lisbon.

Pyramids FC si timu kongwe kwenye mashindano ya vilabu vya Afrika lakini uwekezaji wake ndio unaifanya ionekane timu kubwa na tishio.
Kwa miaka ya hivi karibuni Yanga imecheza hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup mara mbili. Je, Yanga inaweza kuingia kama timu kubwa na ikawasaidia au kuwaathiri?
Amri Kiemba anasema Pyramids inaweza kuwa ni timu ndogo kihistoria lakini ikawa na ushindani mkubwa kutokana na ligi inapotoka.
•
“Naiangalia mechi hiyo kwa gape la ligi ya Tanzania na Misri naona bado ni timu ngumu haijalishi tunacheza na timu gani. Tusiangalie historia ya timu tu…tuangalie pia historia ya ligi wanayocheza. Mechi haitakuwa rahisi.”
•
“Mara nyingi timu za Tanzania zimekuwa na uwezo wa kupata matokeo hata kwa timu za Afrika ya Kaskazini (kwenye mechi za nyumbani) shida imekuwa mechi inapokuwa ugenini.”
•
“Tumeshindwa pia kupata magoli ya kutosha hapa nyumbani ili yazisaidie timu zetu ugenini. Ukishinda goli 1-0 nyumbani kwa timu za Kaskazini mwa Afrika unakuwa kama tayari umeshatoka.”

Wachezaji wa Yanga sasa hivi wanahitaji watu ambao watakuwa nyuma yao kwa sababu presha imekuwa kubwa kwa wachezaji inaonekana usajili umefanyika lakini watu hawapati kile ambacho walikuwa wanahisi hata nusu walikuwa wanakipata msimu uliopita ambapo hawakuwa na wachezaji kama ilivyo sasa.
Mashabiki walishaaminishwa wachezaji wameshasajiliwa kwa hiyo tatizo lile la msimu uliopita litaisha na wataanzia pale walipoishia msimu uliopita lakini inaonekana wanaanza upya.
Kwa hiyo kuitoa timu Dar kuipeleka sehemu nyingine kwenye mazingira tofauti inaweza kusaidia kwa sababu haiwezekani watu wa Mwanza wakaichoka timu haraka. Mechi hii itakuwa na mwitikio na itawasaidia wachezaji na kumrahisishia mwalimu kufanya kazi yake.
Jambo ambalo nina wasiwasi nalo ni kama mwalimu alishirikishwa kwenye maamuzi ya kuipeleka mechi Mwanza…isijekuwa viongozi wameamua halafu wakapeleka taarifa kwa benchi la ufundi.

AFCON 2021: Gambia, Chad, Sudani Kusini na Sao Tome zatinga hatua ya makundi kufuzu fainali za AFCON.
Gambia na Chad zote zimefuzu baada ya kushinda kwa mikwaju ya Penati, wakati Sudani Kusini na Sao Tome Principe wamepita kwa ushindi wa matokeo ya jumla (Aggregate)
Gambia inachukua nafasi kwenye Kundi D ambapo watakutana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gabon na Angola.
Sudani Kusini itacheza kwenye Kundi B na Burkina Faso, Uganda na Malawi.
Sao Tome atakuwa kwenye Kundi C la kufuzu fainali za AFCON 2021 akiwa na Ghana, Afrika Kusini na Sudan.
Mzunguko wa kwanza wa mechi za makundi utaanza kuchezwa mwezi Novemba.

Timu ya Soka ya Tanzania ‘ Taifa Stars’ leo itakuwa na kibarua kigumu ugenini kuwakabili wenyeji Rwanda ‘ Amavubi’ kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali Rwanda
Mchezo huo utaanza Saa 1 Usiku na utakuwa mubashara @azamtvtz .
@tanfootball @taifastars_ @clifordmariondimbo .
#wapendasokaupdates