Timu ya taifa @Taifastars_ imewasili salama nchini Sudan tayari kwa mchezo wa Marudiano kufuzu CHAN dhidi ya wenyeji Sudan Ijumaa Oktoba 18,2019… Game kupigwa Saa 19:00..
#CHAN2020Qualifiers

Tetesi za usajili ulaya ..jumanne octoba 15

Meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri angependelea mchezaji wa zamani wa safu ya ulinzi Manchester United Patrice Evra – ambaye alimfunza katika Turin -kujiunga na makocha wasaidizi katika Old Trafford ikiwa atateuliwa kuwa meneja wa timu hiyo. (Daily Mail)
Mmiliki mwenza wa Manchester United Kevin Glazer,ambaye ni mmoja wa ndugu sita wanaoendesha klabu hiyo anatarahia kuuza asilimia 13% ya hisa zake katika Red Devils. (The Sun)
Kocha wa zamani wa Chelsea boss Maurizio Sarri anamtaka difenda wa zamani wa Chelsea Emerson Palmieri, mwenye umri wa miaka 25, na kiungo wa kati wa Mfaransa N’Golo Kante, mwenye umri wa miaka 28, kuondoka Stamford Bridge kuelekea Juventus. (Daily Express)
Milan wanaangalia uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Arsenal mwezi Januari Mmisri Mohamed Elneny, mwenye umri wa miaka 27, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni katika Besiktas. (Gazzetta – in Italian)
Meneja wa Arsenal Unai Emery hatalazimika kuvunja kipengele katika mkataba aliosaini mwaka 2018 mwishoni mwa msimu. (The Athletic, via Express)
Meneja wa zamani wa Tottenham Harry Redknapp anasema Mauricio Pochettino atakuwa “mjinga ” kuondoka katika klabu yake kwa ajili ya kujiunga na Manchester United, ambayo anaamini “inaweza kuchukua miaka ” kuijenga upya . (Mirror)
Manchester United wanamatumaini kuwa Juventus itakubali pauni milioni £9m kwa ajili ya Mshambuliaji wa Mcroasia Mario Mandzukic mwenye umri wa miaka 33 . (Goal.com)
Chelsea ni moja kati ya klabu zinazopokea mashindano zinazomfukuzia kiungo wa kati Charlie Allen mwenye umri wa miaka 15-ambaye amefanikiwa kujiunga na timu yake ya kwanza katika championi Ligi ya Ireland Kaskazini ya Linfield. (Daily Express)
Victor Lindelof, mwenye umri wa miaka 25, anadai kuwa hakujali mazungumzo ya uhamisho yanayomuhusisha na Barcelona katikia msimu waujao ,na mlinzi wakikosi cha Sweden . (goal.com)
Manchester United wanajiandaa kumuunga mkono meneja Ole Gunnar Solskjaer katika msimu wa uhamisho wa wachezaji ifikapo mwezi Januari lakini wanaonya kuwa hawatalipa malipo ya ziada kwa wachezaji eti tu kwasababu ya kunusuru msimu wao kimchezo . (ESPN)
Paris St-Germain wamethibitisha kwamba mshambuliaji Mbrazil Neymar, mwenye umri wa miaka 27, ataondolewa katika kikosi hicho kwa wiki nne kutokana na jeraha la mkono . (Mirror)
Meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini ameongeza mkataba wake kama kocha wa Italy hadi mwaka 2022 baada ya kuheshimu kipengele katika mkataba wake , kwa kusaini kufuzu kwa Euro 2020 . (Mail)
Meneja wa klabu ya Bournemouth Carl Fletcher anafanya mazungumzo yatakayo muwezesha kuwa meneja wa Leyton Orient . (Bournemouth Echo)
Arsene Wenger atafichua kiwango chake cha taaluma katika Arsenal mwaka ujao wakati wasifu wake utakapotangazwa . (London Evening Standard)
BBC
Niyonzima afunguka baada ya kukutana na bin kleb

Kiungo wa zamani wa Yanga Haruna Niyonzima jana alikutana na Abdallah Bin Kleb, ambaye ndiye aliyekamilisha usajili wake wa kujiunga na Yanga mwaka 2012
Bin Kleb alisafiri nchini Rwanda na kikosi cha timu ya Taifa yeye akiwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya uhamasishaji
Baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, wawili hao walikutana
“Leo nimekutana na baba yangu boss wangu mtu aliyenifanya Watanzania wote wa kanijua”
“Nakumbuka ilikuwa 2012 aliponifuata nyumbani kwetu na leo tumekutana tena”
“Nakuombea maisha marefu Abdallah (bin-kleb) wewe ni zaidi ya ndugu yangu,uliishi na mimi vizuri na ulikuwa mtu mwema kwangu”
“Allah azidi kukulinda na kukuepusha na kila jambo baya,” ulisomeka ujumbe washukrani aliotoa Niyonzima
Niyonzima amekuwa akihusishwa kutaka kurejea Yanga, timu aliyoitumikia kwa mafanikio zaidi nchini Tanzania
Edwin van der Sar amekiri anania ya kuwa mkurugenzi wa michezo wa Manchester United

Edwin van der Sar amekiri anania ya kuwa mkurugenzi wa michezo wa Manchester United
Golikipa uyo namba 1 wa zamani wa Manchester United kwa sasa ni mtendaji mkuu uko Ajax na amesimamia ongezeko kubwa la vipaji ndani ya Academy
Van der Sar alikaa miaka sita pale Old Trafford, akishinda mataji manne ya Ligi Kuu na kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa mara tatu (Akishinda mara 1)
Man United iko katika mpango wa kumtangaza Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo baada ya klabu hiyo kushindwa kufanya vyema katika madirisha ya usajili wa wachezaji.
Barcelona Ivan Rakitic alazimika kuondoka uwanja wa ndege wa Barcelona kwa mguu

Nyota wa Barcelona Ivan Rakitic amelazimika kuondoka uwanja wa ndege wa Barcelona kwa miguu kufuatia maandamano yanayoendelea katika jimbo la Catalonia.
Maelfu ya waandamanaji wanaendelea kumiminika katika mitaa ya Barcelona, kupinga hukumu iliyotolewa Jumatatu na mahakama kuu ya Hispania dhidi ya viongozi wa Kikatalani walioshinikiza jimbo la Catalonia kujitenga na Uhispania.
Inaripotiwa kwamba waandamanaji hao wana mpango wa kutumia mechi ya El Clasico itakayochezwa pale Camp Nou tarehe 26 mwezi huu kama sehemu ya kupinga hukumu hiyo, kwani itakuwa mechi inayofuataliwa ulimwenguni kote.
Je malengo ya ndairagije stars ..kutimia

Kwa kila kocha anayepewa nafasi ya kuifundisha timu ya taifa malengo yake yako wazi, ni kuhakikisha timu ya taifa husika inafanya vizuri kwenye mashindano inayoshiriki.
Malengo aliyopewa Ndayiragije ni kuisaidia Tanzania kufuzu kwenda fainali za CHAN kwa hiyo kama nchi haijatolewa hakuna mjadala wa kuanza kumtathmini.
Siwezi kusema Etienne Ndayiragije amefeli, kwa sababu alipewa timu na jukumu lake ni kuivusha timu kwenda kwenye fainali za CHAN ambapo timu bado haijatoka kwenye mashindano.
Kuna wadau anasema anashinda kwa penati, haijalishi. Kwenye soka matokeo ya ushindi wa penati ni matokeo, watu wameshangilia sana kubeba ubingwa wa kombe la dunia kwa penati, watu wamebeba Champions League kwa penati, watu wameshinda kwa faida ya goli la ugenini. Kinachoangaliwa ni timu kupata matokeo.
Mpaka sasa hivi amefanikiwa kuivusha Tanzania na kuipeleka kushiriki hatua ya makundi ya kutafuta kufuzu fainali za kombe la dunia, aliwatoa Kenya kwenye harakati za kufuzu CHAN na bado anamchezo mmoja dhidi ya Sudan wa raundi ya mwisho ya kufuzu CHAN.
Tusubiri mechi dhidi ya Sudan iishe ndio tutakuwa na wakati mzuri wa kumfanyia tathmini kwamba anafaa kuendelea au hafai lakini kwa sasa bado anafanya vizuri na timu bado ipo kwenye mashindano.
Mechi ya kwanza dhidi ya Sudan alipoteza kwa kufungwa goli moja nyumbani lakini haimaanishi katoka kwenye mashindano bado ana mechi nyingine ya marudiano nani anajua nini kitatokea? Hebu tumpe muda kocha afanye kazi baada ya mchezo wa Sudan tufanye tathmini.
Akifanikiwa kufuzu CHAN atakwenda na timu yake kwenye mashindano mpaka mwisho kieleweke kama ilivyokuwa kwa Amunike.
Amunike alikuja akapewa jukumu la kuipeleka Stars kwenye fainali za AFCON, aliweza kuiongoza nchi ikafuzu akaendanayo kwenye mashindano hakufanya vizuri akarudi akaondoka.
Kwangu mimi bado sina sababu ya kumlaumu kocha Ndayiragije hadi pale ambapo atakapomaliza kibarua chake cha kuhakikisha nchi inafuzu fainali za CHAN.

Golikipa bora wa Dunia, Alisson Becker anatarajiwa kurejea uwanjani

Golikipa bora wa Dunia, Alisson Becker anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya kupona majeraha ya bega na atakuwepo Jumapili kwenye mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool.
Kwa upande wa Man United, wachezaji Luke shaw, Anthony Martial, Paul Pogba na Aaron Bissaka wanatarajiwa kuwepo kwenye mchezo huo utakaopigwa pale Old Trafford 🏟

SARRI APANGA KUIBOMOA CHELSEA

Meneja wa Juventus, Maurizio Sarri amepanga kuibomoa timu yake ya zamani ya Chelsea kwa kusajili wachezaji wawili muhimu kwa vijana hao wa Stamford Bridge.
Sarri anataka kumsajili mlinzi wa kushoto aliye kwenye kiwango bora Emerson Palmieri,mwenye umri wa miaka 25, na kiungo mkabaji N’Golo Kante, 28.
Raia huyo wa Italia ambaye msimu uliopita alikuwa Chelsea anaendele kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya michuano mbalimbali na kama watafainikiwa kunasa saini ya nyota hao atakuwa ameidhoofisha Chelsea.
#wapendasokaupdates