Tarehe kama ya leo miaka 15 iliyopita, Lionel Messi alicheza mechi ya kwanza ndani ya Barcelona.

Tarehe kama ya leo miaka 15 iliyopita, Lionel Messi alicheza mechi ya kwanza ndani ya Barcelona.

Miaka 15 ya Maajabu ya Messi:

2003: Messi anacheza mechi ya kwanza ndani ya Barcelona akitokea benchi 1⃣

2005: Bao lake la kwanza kwa Barcelona ⚽. 1⃣

2007: El Clasico Hat-trick dhidi ya Real Madrid kwenye Champions League. ⚽⚽⚽

2007: Goli la maajabu dhidi ya Getafe, Bao Bora katika historia ya Barcelona.✅

2009: Bao la kichwa kwenye Fainali ya Ligi ya Mabingwa…dhidi ya Ronaldo (Man Utd), Bao analolikubali sana Messi katika maisha yake ya soka 🤩

2010: Messi anaipiga Arsenal mabao manne kwenye Champions League. ⚽⚽⚽⚽🙀

2012: anakuwa mfungaji bora wa mda wote Barcelona (bao 233) 📈

2015: Anashinda Ballon d’or ya 5, na kufikisha makombe manne ya Champions League. 🏆🏆🏆🏆

2018: anapewa unahodha Barcelona 🎩

2019: Ile Freekick dhidi ya Liverpool, Messi akisimama takriban yadi 30

*Leo Lionel Messi atakabidhiwa tuzo ya Golden Boot kwa mara ya 6 katika maisha yake ya soka

Inaendelea…

Ben mwalala . atoa.mbinu kwa.yanga kuiondosha pyramids

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Ben Mwalala ambaye kwa sasa ni kocha wa Bandari FC ya Kenya anasema Yanga inataka kuitoa Pyramids na kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika basi ihakikishe inapata matokeo mazuri nyumbani.

“Yanga wanatakiwa kutumia vizuri home advantage wapate ushindi. Lazima wapate matokeo mazuri nyumbani, wasipopata matokeo mazuri basi wamekwisha”-Ben Mwalala, kocha Bandari FC-Kenya.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Pyramids kwenye mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho. Mchezo huo utakaochezwa October 27, 2019 kwenye uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Oscar Mirambo ateuliwa kuwa mkurugenzi mpya TTF

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limemtangaza Oscar Mirambo kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi wa shirikisho hilo
. .
Mirambo ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) anachukua nafasi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Amy Ninje.
. .
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

WAMBURA ABADILISHIWA MAJUKUMU TFF

Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi (TPLB), Boniface Wambura amebadilishiwa majukumu na sasa atakuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Masoko

Wambura atasaidiwa na Clifford Ndimbo kwa upande wa Habari na Mawasiliano na Aaron Nyanda atamsaidia kwa upande wa Masoko.

Mabadiliko hayo yametangazwa mbele ya Waandishi wa Habari na Katibu mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidao baada ya maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji.
.

Kidao amesema wanataka kuiendesha Idara ya Habari kisasa kama teknolojia inavyotaka ndio maana wameanzisha TFF TV, Tovuti na wako mbioni kuanzisha Radio kwa njia ya mtandao (Online Radio).
. “Boniface Wambura amemaliza mkataba wake Bodi ya ligi na sasa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa TFF ili kuongeza ufanisi katika Idara ya Habari,” alisema Kidao.

@tanfootball @tplboard
@clifordmariondimbo @wilfredkidao

#wapendasokaupdates

Simba kulinda heshima ..nyumbani Leo

✍🏻 Baada ya kuichapa 1-0 Mashujaa FC, Hii Leo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania, klabu ya Simba SC itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na mabingwa wa Burundi 🇧🇮, klabu ya Aigle Noir.

✍🏻 Wakati huo huo, Baada ya kuwanyoosha 4-2 Friends Rangers, Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Kimataifa Barani Afrika, klabu ya Yanga SC hii leo itashuka katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kucheza mechi yao nyingine ya Kirafiki dhidi ya klabu ya PAN Africans… Game zoote kupigwa Saa 16:00.
#FriendMatch #YNGPAN #SSCANR

Real. madrid kuingia sokoni kunasa ng’olo kante

✍🏻 Klabu ya Real Madrid imejiandaa kutoa kitita cha pauni 86m pamoja na kiungo wa Kimataifa wa Colombia, James Rodriguez kama ofa yao kutaka kumsajili kiungo wa Kimataifa wa Ufaransa, N’Golo Kante anaekipiga katika klabu ya Chelsea… Kwa Mujibu wa Gazeti la Hispania, El Desmarque..
#chelseafc #realmadrid #TransfersNews

De Gea kuikosa livepool…mechi ijayo

✍🏻 Mlinda lango, David de Gea kuna mashaka ya kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo klabu yake ya Manchester United itakapokuwa na Kibarua dhidi ya Liverpool Jumapili, hii ni baada ya kutolewa kufuatia kupata majeraha kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Hispania 🇪🇸.
..
✍🏻 Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana kuumia misuli katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa EURO 2020 nchini Sweden 🇸🇪…. Nafasi yake alichukua Kepa Arrizabalaga wa Chelsea, Hispania walianza kufungwa huku goli lao la Kusawazisha likifungwa na Rodrigo dakika ya 90 na kutoka sare ya 1-1 na Hispania kupata nafasi ya kushiriki Michuano ya EURO 2020.
….
✍🏻 United ni ya 12 kwenye Msimamo wa Ligi ikiwa tayari na “rundo” la Majerahi katika Kikosi, hawajashinda kwenye michezo yao mitatu ya Iliyopita, Watakabiliana na Liverpool ambao hawajapoteza mchezo hata mmoja msimu huu..
#spain #ManchesterUnited #PremierLeague #EURO2020Qualifiers
@Harunlugoyah

Simba kumaliza..ziara..kigoma.leo..

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wanamaliza ziara yao mkoani Kigoma kwa kuwakabili Aigle Noir, mabingwa wa Burundi

Mchezo huo utapigwa saa kumi jioni katika uwanja wa Lake Tanganyika

Simba iliwasili Kigoma Jumapili iliyopita ambapo juzi Jumatatu ikacheza na Mashujaa Fc katika mchezo ambao walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0

Leo wanatupa karata nyingine dhidi ya mabingwa hao wa Burundi waliosafiri kutoka kwao kwa ajili ya mchezo huo

Katika kipindi hiki cha mapumziko ya michuano ya Kimataifa, Simba ilipanga kucheza mechi tatu a kirafiki, wakiwa wameshinda mechi mbili za awali dhidi ya Bandari Fc na Mashujaa

Baada ya mchezo huo Simba itarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 23

Italy 🇮🇹 wamefikia rekodi ya kushinda mechi tisa mfululizo

Italy 🇮🇹 wamefikia rekodi ya kushinda mechi tisa mfululizo katika mashindano yote, rekodi iliyowekwa tangu Mei 1938 mpaka Machi 1939, chini ya Vittorio Pozzo.

Italy 1-0 USA
Italy 2-0 Finland
Italy 6-0 Liechtenstein
Greece 0-3 Italy
Italy 2-1 Bosnia
Armenia 1-3 Italy
Finland 1-2 Italy
Italy 2-0 Greece

🏟 Mechi 9
✅ Ushindi ×9
⚽ Mabao 21

Design a site like this with WordPress.com
Get started