Bondia, Patrick Day amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 27 –

✍🏻 Bondia, Patrick Day amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 27 – siku nne baada ya kupata jeraha la ubongo katika mapigano na Mpinzani wake Charles Conwell huko Chicago.

✍🏻 Mmarekani huyo alilazwa Coma tangu siku ya Jumamosi baada ya kutandikwa vibaya katika raundi ya 10 Mpinzani wake huyo… Alitolewa kwa Msaada wa Machela baada ya kuanguka chini na Kushindwa kuamka tena.

✍🏻 Promota wa pambano, Lou DiBella amethibitisha kifo hicho kuwa Bondia huyo alifariki akiwa “amezungukwa na familia yake, marafiki wa karibu na washiriki wa timu yake ya ndondi”.. R.I.P 🕯🕯🕯
@Harunlugoyah

El Clasico. kuhamishiwa Santiago Bernabeu

✍🏻 La Liga imeomba game ya El Clasico mnamo Oktoba 26 iondolewe kutoka uwanja wa Barcelona, Nou Camp kwenda Santiago Bernabeu, uwanja wa Real Madrid, Sababu ni juu ya hofu ya machafuko ya raia… Kumekuwa na siku za maandamano huko Barcelona baada ya viongozi tisa wa kujitenga wa Kikatalani kuhukumiwa kwenda jela siku ya Jumatatu na Maandamano yakiwa na Mabango yenye ujumbe zaidi yanatarajiwa jijini siku ya mechi ndani ya Uwanja.

✍🏻 La Liga imetuma ombi tu kwa Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF), lakini Ombi halijatumwa kwa Barcelona au Real Madrid…Vilabu vyote viwili vitapewa Taarifa na RFEF kutoa mapendekezo yao, na kamati ya mashindano ya Shirikisho kufanya uamuzi wake katika siku chache zijazo…Shirikisho la Soka la Kikatalani lilisimamisha mechi zote siku ya Jumatatu, ingawa uamuzi huo haukuathiri mechi za timu ya taifa ya Uhispania.

✍🏻 Watajaji hao tisa walitiwa hatiani kwa sababu ya kuasi msimamo wao katika kura ya maoni na walipewa kifungo cha miaka tisa hadi 13 na Mahakama Kuu ya Uhispania.. Kufuatia hukumu hiyo, Barcelona ilisema: “Gereza sio suluhisho… Mabingwa hao wa Uhispania waliongeza: “Sasa ni zaidi ya hapo zamani, klabu inawataka viongozi wote wa kisiasa kuongoza mchakato wa mazungumzo ili kusuluhisha mzozo huu, ambao unapaswa pia kuruhusu kutolewa kwa viongozi na raia wa kisiasa waliotiwa hatiani… FC Barcelona pia inaelezea msaada wake wote na mshikamano kwa familia za wale ambao wamenyimwa uhuru wao… 🙌🏻👏🏻
#elclassico2019⚽️🔥🔥🔥 #Elclassico #realmadrid #fcbarcelona
@harunlugoyah

Messi atwaa tuzo ya sits mfungaji bora ulaya

Mshambuliaji wa Fc Barcelona Lionel Messi amekabidhiwa tuzo ya ufungaji bora barani Ulaya aliyoshinda msimu uliopita

Messi alitwaa tuzo hiyo baada ya kupachika mabao 36 na kuwa kinara wa kufunga mabao katika ligi zote barani Ulaya

Hiyo ni mara ya sita Messi anatwaa tuzo hiyo akimshinda mpinzani wake Cristiano Ronaldo aliyetwaa tuzo nne

Simba yashindwa kutamba nyumbani

Mchezo wa Kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Aigle Noir umemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, ulishuhudia timu zote zikipata wakati mgumu kucheza katika mazingira yasiyoridhisha ya uwanja huo

Pamoja na kutengeneza nafasi kadhaa hasa kwenye kipindi cha pili, mambo yalikuwa magumu kwa safu ya ushambuliaji ya Simba iliyoongozwa na Wilker Da Silva raia wa Brazil ambaye alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa walinzi wa Aigle Noir

Simba imemaliza ziara yake mkoani Kigoma bila ya kupoteza mchezo ikishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Mashujaa

Mchezo huo pia umekamilisha mechi tatu za kirafiki ambazo Simba imecheza wakati huu ambao ligi imesimama

Simba inarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa uwanja wa Uhuru, Oktoba 23

Mchezo wa Yanga waahirishwa

Katika hatua nyingine, mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Pan Africans uliokuwa upigwe uwanja wa Uhuru leo, umeahirishwa baada ya uwanja huo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam

Makamu wa raisi TFF kuteuliwa

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao ameweka wazi mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo ambayo kwa kiasi kikubwa yanahusu mfumo wa uongozi kuelekea uchaguzi ujao.

Moja kati ya mambo yaliyoguswa ni nafasi ya Makamu wa Rais ambapo kuanzia sasa hatachaguliwa kwa kupigiwa kura bali atakuwa akiteuliwa na Rais.

Mabadiliko mengine yamegusa idadi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ambayo sasa itapungua kutoka 22 hadi 13, huku kanda nazo zikipunguzwa kutoka 13 hadi 6.

Vilevile katika mabadiliko hayo wajumbe wa mkutano mkuu watapungua kutoka 129 hadi 87, ikimaanisha kuwa kila mkoa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara utatoa wajumbe wawili, wajumbe 20 watatoka kwenye vilabu huku vyama washirika wakitoa wajumbe 15.

Taifa stars ..matumaini ya kufuzu CHANI. Bado yapo

Pamoja na kuwa nyuma kwa bao 1-0, kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano kusaka nafasi ya kucheza fainali za mashindano ya CHAN 2020 yanayohusisha wachezaji wa ndani

Kikosi cha Stars kiliwasili salama nchini Sudan jana kikitokea Rwanda ambako juzi walicheza mchezo wa kirafiki na kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya wenyeji wao Rwanda

Nahodha Msaidizi wa timu hiyo Erasto Nyoni amesema wachezaji wote wako katika hali nzuri, jana jioni walifanya mazoezi yao ya kwanza nchini Sudan

Kuhusu usalama, Nyoni amesema timu iko katika mazingira salama huku akiwataka mashabiki kuwaombea ili waweze kushinda keshokutwa

Tanzania inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili ili kukata tiketi ya kucheza fainali za CHAN ambazo zitafanyika mwakani nchini Cameroon

Kama itafanikiwa kufuzu, hiyo itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki fainali za michuano hiyo ikikata tiketi kwa mara ya kwanza mwaka 2006 wakati huo ikinolewa na Marcio Maximo raia wa Brazil

Awali mchezo huo ulitangazwa kuwa ungechezwa nchini Uganda kutokana na hofu ya usalama huko Sudan

Lakini wenyeji Sudan wamelihakikishia shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kuwa mchezo huo utachezwa nchini humo katika mazingira salama

Simba , yanga Leo. Viwanjani

Vigogo wa soka nchini Simba na Yanga leo wako viwanjani kucheza mechi za kirafiki

Simba bado iko mkoani Kigoma ambapo leo itashuka uwanja wa Lake Tanganyika kuikabili Aigle Noir kutoka Burundi

Mabingwa hao wa Tanzania Bara walitua Kigoma Jumapili na juzi Jumatatu kucheza na Mashujaa katika mchezo ambao walishinda kwa bao 1-0

Wakati Simba ikiwa Kigoma, Yanga itashuka kwenye uwanja wa Uhuru kuikabili Pan African

Huo ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Yanga ambayo inakabiliwa na mchezo mgumu wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc Oktoba 27

Juzi Yanga iliichapa Friends Rangers mabao 4-2 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam

Spurs yamrejesha Michel Vorm

Mlinda mlango Michel Vorm amerejeshwa kwenye kikosi cha Tottenham, baada ya kuachwa mwishoni mwa msimu uliopita, kufuatia mkataba wake na klabu hiyo kufikia kikomo.

Vorm amerudi klabuni hapo kwa mkataba maalum, na ananatarajiwa kuwa langoni mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi kuu ya England dhidi ya Watford.

Vorm raia wa Uholanzi, amepewa nafasi hiyo, kufuatia kuumia kwa mlinda mlango chaguo la kwanza Hugo Lloris, alipokua kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Brighton.

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amependekeza kurejeshwa kwa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 35, ili asaidiane na Paulo Gazzaniga ambaye alikua chaguo la pili baada ya Lloris.

“Sijaona tofauti kubwa kurejea hapa, klabu hii ni kama nyumbani na ninaahidi kupambana ili kusaidia kufikia malengo,” alisema Vorm baada ya kukamilisha usajili wake akiwa kama mchezaji huru. “Nilipigiwa simu ya kunitaka kurudi hapa, na mimi sikukataa kufanya hivyo kwa sababu ninahitaji kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hii.”

“Tunahitaji kushikamana kwa pamoja, kila mmoja atambue mchango wa mwingine ili kufikia lengo,” aliongeza Vorm, ambaye amesisitiza kuwa tayari kwa mapambano ya kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Spurs.

Vorm atavaa jezi namba 13, ambayo aliitumia wakati akiwa klabuni hapo, kabla ya kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita

Kwa mara ya kwanza Vorm alisajiliwa klabuni hapo mwaka 2014, na alifanikiwa kucheza michezo 47.

Cheche ataka magoli azam

Kocha Msaidizi wa Azam Fc Iddi Cheche amesema bado safu ya ushambuliaji ya kikosi chake haitumii nafasi ipasavyo

Azam Fc imeanza msimu kwa kishindo, ikishinda mechi zote tatu pamoja na kushinda mechi zote za kirafiki walizocheza karibuni

Waliifunga Green Warriors mabao 5-0 na baadaye juzi wakawafunga African Lyon 2-0, katika mechi hizo mbili za kirafiki walizocheza za kujiandaa kuwakabili mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba ifikapo Oktoba 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Cheche amesema anataka kuona safu yao ya ushambuliaji inatumia nafasi zote wanazozitengeneza ili kuwa salama katika kila mechi wanayocheza.

Cheche alisema Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu inaushindani zaidi ya msimu uliomalizika, kwa sababu idadi ya timu zinazotarajiwa kushuka daraja ni nyingi, hivyo kila klabu inataka kulikimbia janga hilo.

“Bado tunataka kuona timu inafunga zaidi, unapopata nafasi, unatakiwa uitumie vizuri, haya ni baadhi ya makosa ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi, huko mbele mambo yasije kuwa magumu, tunataka kufunga mabao zaidi ili kujihakikishia pointi tatu,” alisema Cheche.

Aliongeza kuwa amefurahi kuona wachezaji waliokuwa majeruhi wamepona, na wamerejea katika kikosi hicho kinachowania ubingwa wa Bara kwa mara ya pili.

“Tunaweza kucheza mechi nyingine ya kirafiki au la, tutaangalia hili na kufanya uamuzi, tunajua Simba ni moja ya timu ngumu, lazima tuwe imara kabla ya kuwakabili,” Cheche alisema.

Miaka 4 ya Klopp kutimia old trafford

#Part1 – Miaka 4 ya Klopp: Safari ya Kuirudishia Liverpool Hadhi Yake.
.
.
Jumapili hii, Klopp na vijana wake wanaelekea Old Trafford kuumana na Manchester United, mtanange kileleni mwa msimu na uongozi wa points 8 mbele ya Manchester City wanaoshika nafasi ya pili.

Mechi hii ya Jumapili inaangukia katika wiki ambayo Klopp anatimiza miaka 4 na Liverpool, katika kipindi hicho amefanya mabadiliko makubwa katika klabu hii.

Klopp alimrithi Brendan Rodgers na kuanza kazi rasmi mnamo 17 October 2015, mchezo wake wa kwanza uliisha kwa sare ya 0-0 dhidi ya Tottenham- kwenye kikosi ambacho kilijaa vijana wengi wasiokuwa na uzoefu wa kutosha.

Katika wachezaji 18 walioitwa kwenye mchezo huo – ni wanne tu ambao wamebaki katika klabu – Adam Lallana, Divock Origi, James Milner na Nathaniel Clyne. Tangu wakati huo, Klopp ameibadilisha Liverpool, kuiongoza kutwaa Champions League na kuifanya kuwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa uchampions wa nyumbani.

Kuelekea mchezo wa Jumapili, Klopp anaonyesha namna amefanya kazi kubwa kuifanya Liverpool kuwa klabu ya kuogopwa barani ulaya – hasa ukizingatia kikosi alichorithi kutoka kwa Brendan Rogers kilikuwa dhaifu kuliko kikosi alichorithi mpinzani wake wa Jumapili Ole Gunnar Solskjaer. Lakini alifanikiwa kuwapeleka fainali mbili katika msimu wa kwanza, na kuwawezesha kucheza Champions League katika kila msimu tangu wakati huo.

Klopp amefanikiwa kufanya usajili mzuri wa wachezaji wanaofit katika filosofia yake ya soka, wenye haiba nzuri yenye kutengeneza ushirikiano mzuri kwenye timu.

Kuna sababu nyingi Kwanini Liverpool wanafanikiwa – kuanzia kwenye uongozi wa juu mpaka kwenye benchi la ufundi – lakini ‘Klopp Man Manmanagement’ ni sababu kuu katika kuunda ngome ngumu ya Liverpool.

Msimu ambao Klopp alichukua mikoba ya Rogers, Liverpool walimaliza kwenye ligi katika nafasi ya 8, nyuma ya timu kama Soton na West Ham, timu ambazo hivi sasa zikisikia inakuja mechi na Liverpool zinajua vipigo vinakuja.

Kumekuwepo na matokeo ya kuwarudisha nyuma kama Fainali ya Europe League 2016, kuondokewa na baadhi ya wachezaji muhimu kama Coutinho – lakini chini ya uongozi wa Klopp, Liverpool imeendelea kuimarika.
•••••••••INAENDELEA••••

Design a site like this with WordPress.com
Get started