
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake haikuwa ikiangalia matokeo zaidi kwenye michezo ya kirafiki waliyocheza jijini Dar es salaam na mkoani Kigoma
Simba ilianza kwa kuichapa Bandari Fc bao 1-0 jijini Dar es salaam kisha kuelekea mkoani Kigoma ambako ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mashujaa Fc kisha kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Aigle Noir
“Matokeo yalikuwa jambo la mwisho kwenye mechi zetu za kirafiki,” amesema
“Muhimu tulihitaji kuwapa wachezaji muda wa kucheza wakati huu ambao ligi imesimama”
Hata hivyo Aussems amekiri mazingira ya uwanja wa Lake Tangayika hayakuwa mazuri kwa timu yake kuweza kufanya vizuri
Jana baada ya mchezo dhidi ya Aigle Noir, beki Yusufu Mlipili alisema uwanja wa Lake Tanganyika uliwapa wakati mgumu kucheza kama walivyozoea
“Tulishindwa kabisa kucheza, uwanja lilikuwa tatizo. Lakini tunashukuru hatupoteza mchezo”
Simba inarejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Oktoba 23

🇮🇱 Eran Zahavi – 11














