KUZIONA YANGA, PYRAMIDS CCM KIRUMBA BUKU KUMI

Uongozi wa klabu ya Yanga leo umetangaza viingilio katika mchezo wa mchujo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri utakaofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Oktoba 27.

Viingilio hivyo vimepangwa vya aina tatu ambapo mzunguko itakuwa shilingi 10,000 VIP shilingi 50,000 na Royal itakuwa shilingi 70,000.

Katika mchezo Yanga itapaswa kupata ushindi ili kujitengenezea nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano itakayoganyika nchini Misri.

@yangasc @tanfootball @caf_online
#wapendasokaupdates
#CafCC

STARS YAPINDUA MEZA KIBABE SUDAN, ILEEE CAMEROON

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imefuzu kushiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazo fanyika nchini Cameroon baada ya kuifunga Sudan ugenini mabao 2-1.

Wenyeji Sudan walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 30 kupitia kwa l Mahmoud baada ya kazi nzuri iliyofanywa na winga wao wa kushoto.

Erasto Nyoni aliisawazishia Stars bao hilo kwa mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja kufuatia Ditram Nchimbi kufanyiwa madhambi nje kidogo ya 18.

Nchimbi aliifungia Stars bao la pili na ushindi dakika ya 79 baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Shaban Chilunda baada ya kupokea pasi akiwa ndani ya 18.

Stars imetinga hatua hiyo kwa faida ya bao la ugenini kufuatia kulala kwa bao moja katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Taifa.

@tanfootball @taifastars_ @clifordmariondimbo @wallacekaria @wilfredkidao
#wapendasokaupdates

Beki wa klabu ya Liverpool, Joel Matip amesaini mkataba mpya

✍🏻 Beki wa klabu ya Liverpool, Joel Matip amesaini mkataba mpya wa muda mrefu ambao utamuweka kwenye klabu hiyo hadi msimu wa joto 2024… Beki huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao mawili katika mechi tisa kwenye mashindano yote katika klabu yake msimu huu, Jumla akiwa na magoli Manne katika mechi zake 82 kwa Majogoo hao.

✍🏻 Matip alijiunga na Liverpool akitokea Schalke ya Ujerumani, mnamo mwaka 2016 na kuisaidia Klabu hiyo ya kocha Jurgen Klopp kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2018-19… Kakosa mechi mbili zilizopita lakini anatarajiwa kurejea Jumapili hii Wakati Liverpool ipo Ugenini kumenyana na Manchester United katika Muendelezo wa Premier league..
#TransfersNews #Liverpool
@Harunlugoyah

Mambo yaliyojitokeza katika mchezo wa tanzania vs sudan

Mambo kadhaa niliyoyaona kwenye mchezo wa Sudan,dhidi ya Tanzania, kuwania kufuzu michuano ya CHAN, ya mwaka 2020.
.
.
Kipindi cha kwanza Taifa Stars ndani ya dakika 15 za kwanza walishambulia kwa kasi sana kutafuta bao la mapema lakini hakuwa bora kwenye utulivu pale wanapofika kwenye goli la Sudan, Nchimbi, alikosa sapoti ya kutosha eneo la ushambuliaji.
.
.
Viungo wetu muda mwingi walikuwa wanashindwa kujiamini walikuwa wanapoteza mpira mingi eneo la kiungo pasi hazifiki, mpira mirefu ilikuwa haina faida kubwa kwetu kwa sababu ya aina ya vimo vyetu.
.
.
Bakari Nondo, moja ya walinzi wa kati siku zote ukicheza na Erasto Nyoni, utakuwa bora alikuwa anakaba mpira ya hewani ilikuwa ikiishia kichwani mwake tuendelee kumjenga. .
.
Salum Kimenya, sijajua leo Ettiene ametumia kigezo gani na benchi lake kumpamga eneo la beki wa pembeni majukumu ya ulinzi ilikuwa shida kwake majukumu ya kushambulia pia ni mtihani kwake. .
.
Kipindi cha pili nafikiri Ettiene, aliwaambia wachezaji wake wasicheze mpira mirefu wacheze mpira wa chini kupiga pasi fupi fupi ndo silaha kubwa ya wachezaji wenye maumbo marefu.
.
.
Mabadiliko ya kuwatoa Iddi Nado, na Miraji Athumani, yalikuwa na faida kubwa kwa sababu hawakuwa na mchezo mzuri kutokana na aina ya wachezaji wa Sudan, matumizi makubwa ya nguvu.
.
.
Kuingia kwa Chilunda, Lyanga, kulikuwa na faida kwa Stars, ni wachezaji wenye nguvu ya kupambana na wachezaji wa Sudan, hii mechi imenikumbusha mechi ya ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mwaka 2014/15 Chelsea dhidi ya Paris Saint German, Jose Mourinho anawatumia washambuliaji wake wote wa tatu Toress, Demba Ba, na Etoo, kupindua meza Ufaransa. .
.
Sudan, wana wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira sana eneo la kati kujiamini sana wakajikuta kupoteza mchezo hili Taifa naliona mbali sana.
.
.
@Azizi_mtambo_15

Mulinga atabiriwa kuwa mshambuliaji tishio VPL

– Nyota wa zamani wa Yanga SC, Edbily Lunyamila amesema mshambuliaji David Molinga akiendelea na kasi ya kuzifumania nyavu katika mechi za ligi anaamini atabadili upepo… Lunyamila alisema anaamini Molinga ni mfungaji mzuri anachomshauri ni kuongeza juhudi ya kufanya mazoezi ya kumfanya mwili wake kuwa mwepesi akiamini atafunga mabao mengi.
..
🗣 “Nimemfuatilia katika mechi za kirafiki anazocheza namuona anajua kucheza na nyavu, naamini atabadili upepo katika ligi tofauti na alivyopokelewa na mashabiki wakati anafika, Kocha Mwinyi Zahera akimbadilisha kidogo, atafunga na watu watashangaa, pia yeye mwenyewe aongeze bidii ya mazoezi atafika mbali badala ya kumchukulia poa atabadili upepo na kuwa mfalme,”alisema.

– Molinga amefunga mabao mawili ya Ligi Kuu Bara, aliyofunga dhidi ya Polisi Tanzania, Yanga ikitoka sare ya mabao 3-3, manne amefunga kwenye mechi za kirafiki, hivyo ana jumla ya mabao sita..
#VPLUpdates🇹🇿 #YangaSC

Mtoto wa Etoo atemwa timu.ya taifa

✍🏻 Mtoto wa Samuel Eto’o anaekipiga katika klabu ya Real Mallorca ya Hispania na pia nahodha wa timu hiyo, Etienne Eto’o kakatwa katika kikosi cha mwisho cha Wachezaji wa timu ya taifa ya Cameroon 🇨🇲 chini ya umri wa miaka 17 ambacho kitashiriki Fainali za Kombe La Dunia 17 huko nchini Brazil 🇧🇷…. Nyota mwingine aliyekatwa katika Kikosi hicho ni, Daniel Barel anaekipiga katika klabu ya AS Roma ya Italia 🇮🇹.. 🙌
#U17FIFAWC #FIFAU17WorldCup

Pyramids yabadilisha beki yanga

Akiwa na uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza kitakachoivaa Pyramids FC ya nchini Misri, kocha msaidizi wa Yanga Mzambia, Noel Mwandila ameanza kumuandaa beki wa kati Mrundi, Moustafa Selemani.

Beki huyo pamoja na mshambuliaji Mkongomani, David Molinga waliikosa michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukosa leseni ya Caf kabla ya juzi kuhakikishiwa kucheza mechi na Pyramids baada ya kujibiwa barua yao.

Yanga inatarajiwa kucheza na Pyramids Oktoba 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mkoani Mwanza kabla ya kurudiana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano na kuthibitishwa na Mwandila ni kuwa amemuandaa beki huyo kwa ajili ya kuja kuziba nafasi ya beki wa kati au kulia ambayo yameonekana kuwa tatizo ndani ya kikosi hicho.

Yanga kwenye mechi yake ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Afrika walilazimika kumtumia beki Ally Ally ambaye anacheza beki wa kati kuitumikia nafasi hiyo kutokana na Paul Godfrey ‘Boxer’ lakini pia watamkosa beki Lamine Moro ambaye ana kadi nyekundu.

“Ni kweli kocha Mwandila amekuwa akimuandaa Mustapha kuja kucheza dhidi ya Pyramids kutokana na yeye kuwa na uwezo wa kucheza nafasi hizo vizuri.

“Tulimkosa kwenye mechi zile za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu alikosa leseni ya kucheza lakini sasa tuna uhakika wa kumuanzisha kwenye mechi hiyo na Waarabu na ndiyo maana kocha ameanza kumuandaa kucheza nafasi hizo kwa sababu ana uhakika wa kumtumia,” kilisema chanzo hicho.

Mustapha licha ya kusajiliwa kama beki wa kati akitokea Burundi lakini amekuwa akipangwa kama beki wa kulia ndani ya kikosi hicho na tayari ameshacheza kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting kufuatia kuumwa kwa Boxer.

Mzee akilimali achafua hali ya hewa.yanga

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, mzee Ibrahim Akilimali ameibuka na kusema kuwa haoni dalili za Yanga ikiitoa Pyramids ya Misri katika mchezo wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika kutokana na uongozi wa timu hiyo kugoma kuwapa timu wazee kuishughulikia.
Mzee Akilimali ametoa kauli hiyo kufuatia Yanga kupangwa na timu hiyo katika hatua ya mtoano ambapo inatarajia kucheza mchezo wa kwanza Oktoba 27, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Mzee Akilimali alisema kuwa wazee wa timu hiyo wamekuwa wakiiomba kwa ajili ya kuiweka sawa kabla ya kucheza na Waarabu hao wa Misri lakini wamekuwa wakipigwa chenga na uongozi wa timu hiyo bila kuwapa majibu ya maana.
“Niwe mkweli kwamba sioni dalili za Yanga ikiwaondoa Waarabu hasa kwa timu ambayo tupo nayo kwa sababu ukiangalia wachezaji wetu wote wamefungwa hawana uwezo wa kushindana kabisa, wanahitaji kufunguliwa lakini uongozi bado unatuwekea ngumu kila tunavyowaambia.
“Sisi tunataka watu ili tufanye mambo yetu na tuweze kufuzu makundi lakini wao hawana mpango wowote wa kutupa zaidi ya kutukimbia, wamepeleka mechi Mwanza lakini haiwezi kusaidia chochote maana kama unasajili wachezaji halafu kwao bado wanagombea tuzo kubwa ila hapa wanaonekana weupe, ndiyo wajue kama wamefungwa,” alisema mzee Akilimali.

Design a site like this with WordPress.com
Get started