YANGA YAWASILI MWANZA

MSAFARA Wa WAKILISHI Pekee Wa TANZANIA Ktk Michuano Ya KIMATAIFA #YangFC Umewasili Jjn MWANZA Tayari Kwa Mchezo Muhimu Uliyopo Mbeleni.
_
>Tarehe 22 October Dhidi Ya Mbao FC Ukiwa Mchezo Wa Ligi Kuu TANZANIA Bara:
_
>Tarehe 27 October Dhidi Ya Pyramids FC Mchezo Wa KOMBE LA SHIRIKISHO Barani AFRICA.
_
>MICHEZO Yote Hiyo Itapigwa Ktk Uwanja Wa CCM Kirumba:
.
.
>KILA LA KHERI Yanga FC!!

Tetesi za usajili barani ulaya

Kiungo wa kati Manchester United na Serbia Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, anatafutwa na Inter Milan. (Sun)

Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 31, ameacha azma yake ya kuhamia Manchester United mwezi Januari kwasababu Wacroasia hawataki ahamie Manchester. (Mail)

La Liga imependekeza kwa shirikisho la soka la Uhispania kwamba shindano la El Clasico lililiyopangwa tarehe 26 Oktoba Barcelona lifanyike badala yake tarehe 7 Disemba . Tayari shirikisho hilo la mpira wa miguu limeomba kubadilisha gemu hiyo ifanyike Madrid kutokana na hofu ya ghasia za kiraia.(AS)

Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Haaland analengwa na Manchester City. Kijana huyo Mnorway mwenye umri wa miaka 19 ni mtoto wa kiungo wa kati wa Manchester City Alf-Inge Haaland. (Sun)

Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya klabu ya Lyon Moussa Dembele anataka kurejea katika soka ya England , huku akiripotiwa kusakwa na Everton na Manchester United. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 23- aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya Ufaransa ya walio chini ya umri wa miaka -21 awali alichezea klabu ya Fulham. (Football Insider)

Manchester United walimtaka na kumfuatilia mchezaji wa Juventus raia wa Poland na mlindalango wa zamani wa Arsenal goalkeeper Wojciech Szczesny, mwenye umri wa miaka 29, wakati wa msimu ujao wa soka kabla David de Gea kusaini mkataba mpya katika Old Trafford mwezi uliopita. (Goal)

Wolves wameweka dau kwa ajili ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Ivory Coast Franck Kessie mwenye umri wa miaka 22 kutoka AC Milan mwezi Januari . (La Gazzetta dello Sport via Calciomercato)

Tottenham na Manchester United ni miongoni mwa klabu kadhaa zilizowasiliana na Borussia Monchengladbach kuhusiana na namna wanavyoweza kumpata Mswiss anayecheza safu ya kati Denis Zakaria ambaye sasa ana umri wa miaka 22. (Bild – in German)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, “si mzuri vya kutosha ” kwa Bayern Munich, anasema mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Lothar Matthaus. (Sport 1, via Standard)

Tottenham watalenga kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Madrid Muhispania Isco,mwenye umri wa miaka 27, kama wataamua kumuuza Eriksen ifikapo mwezi Januari (El Desmarque – in Spanish)

Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, ambaye sasa ana umri wa miaka 31, mwishoni mwa msimu ikiwa atbakia kuwa mchezaji wa ziada. (Football Insider)

Mlindalango wa Liverpool Mhispania Adrian, mwenye umri wa miaka 32, anasema the Reds walimkanyaga mara mbili na kumuumiza mlindalango wa Brazil Alisson Becker,mwenye umri wa miaka 27. (Telegraph)

Watfordwamekataa ombi kutoka kwa Fluminense la kuendelea kubaki na Joao Pedro nchini Brazil hadi Juni -2020. Hornets wamekubali kusiani mkataba na kijana huyo mchanga mwenye umri wa miaka 18 tu anayecheza safu ya mashambulizi Januari 1 . (Watford Observer)

Winga wa Crystal Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, hutoa 10% ya mshahara wake kama msaada katika nchini Ivory Coast ambako ndio asili yake , ikiwa ni ni pamoja na kusaidia kituo cha yatima kinachoendeshwa na dada yake. (Mirror)

Liverpool ina matumaini ya kuipiku Chelsea kwa kusiani mkataba na mchezaji wa kimataifa wa vijana wadogo ya England kutoka Exeter anayecheza safu ya kati Ben Chrisene ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15. (Sun)

BBC

Neymar kua nje ya dimba kwa mwezi mmoja

Kiungo wa PSG, Neymar ametupwa nje kwa wiki nne baada ya kuumia nyama za paja akiwa na timu ya Taifa ya Brazil.

Neymar aliumia kwenye mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Nigeria

Hili ni pigo kubwa kwa PSG ambayo msimu huu ilikuwa imeshaanza kuweka matumaini makubwa kwake kwa kuwa alishaanza msimu vizuri.

Hata hivyo, daktari wa timu ya Taifa ya Brazil, Rodrigo Lasmar, amesema kuwa majeraha ya mchezaji huyo siyo makali sana.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, alipelekwa moja kwa moja kwa daktari wake wa timu yake ya PSG.

Juzi aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram, akiwa kitandani huku akiwa amefunga bandeji ngumu.

Mshambuliaji huyo alikosa michezo kadhaa ya mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu wa kulia.

Moringa kuikosa pyramids

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mshambuliaji David Molinga na beki Mustafa Suleyman wataanza kuitumikia timu hiyo kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho iwapo watafanikiwa kuitoa Pyramids Fc

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwakalebela amesema kulingana na kanuni za CAF za michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho haziwaruhusu kucheza hatua ya mtoano

“Napenda nitoe ufafanuzi kuhusu wachezaji wawili ambao watu wamekuwa wakiuliza kama wataweza kucheza mechi dhidi ya Pyramids Oktoba 27”

“Ni suala la kikanuni kwamba wachezaji Molinga na Mustafa wataruhusiwa kuitumikia Yanga kama tutatinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa au kombe la Shirikisho”

“Hivyo wachezaji hao tutaendelea kuwatumia kwenye ligi na kama tutatinga makundi wataweza kucheza,” amesema

Taarifa hiyo inakinzana na ile iliyotolewa wiki iliyopita na Afisa Habari Hassan Bumbuli ambaye alisema Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) lilikuwa limewahakikishia kuwa wachezaji hao wataruhusiwa kucheza na kinachosubiriwa ni kuwasili kwa vibali vyao

Ni wazi baada ya kufuatilia huko CAF, Yanga imejiridhisha haitaweza kuwatumia wachezaji hao kwa ajili ya mchezo dhidi ya Pyramids FC

Joto. Laongezeka niyonzima.kutejea jangwani

“mwenyekiti wa club ya yanga mshindo Msolla amesema watamsikiliza mwalim wao mwinyi zahera iwapo atahitaji huduma ya kiungo Mnyarwanda #haruna Niyonzima watamsajili kipindi cha dirisha dogo.

Msolla amesema moja ya viungo waliocheza kwa mapenzi yao na mafanikio makubwa yanga ni haruna niyonzima hivyo mwalim akimwitaji watamsajili.

JESHI SIMBA LAINGIA VITANI

JESHI la mabingwa watetezi Ligi Kuu Bara, Simba, ni kama halijaridhika na kile kilichovuna katika michezo minne iliyopita licha ya kukusanya pointi zote 12.

Sasa kikosi hicho kinataka kuonyesha kuwa bado kinataka kuweka historia ya kipekee katika soka la Tanzania na Afrika kwa ujumla, kutokana na inavyohaha kuhakikisha inafanya mambo makubwa zaidi.
Malengo makubwa ya Wekundu wa Msimbazi ni kutetea ubingwa ili kurejea katika michuano ya kimataifa, hivyo mkakati uliopo ni kuzivuruga timu zote za Bara kwa kutoa vichapo.
Licha ya mkakati huo, uongozi umekuwa mkali kuhakikisha kunakwepo na nidhamu lengo likiwa ni kuinua hadhi ya klabu hiyo kongwe.

Simba ilianza mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kuzinyamazisha timu sumbufu mbili za Mtibwa Sugar ambao waliichapa mabao 2-1, kisha kuwafunga Kagera Sugar 3-0 ugenini.
Katika mechi nyingine walizocheza, Simba waliwafunga JKT Tanzania mabao 3-1 na Biashara United 2-0.
Kama vile haitoshi Simba sasa wameamua kuelekeza nguvu zao katika mechi yao dhidi ya Azam FC inayotarajiwa kupigwa baadaye mwezi huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itachezwa Oktoba 23 mwaka huu.

JAMES KOTEI MAMBO MAGUMU HUKO KEIZER CHIEF’S●

James kotei ameshindwa kumshawishi kocha wa KEIZER CHIEF’S kiasi kwamba watabe hao wa south Africa wanafikiria kumtoa kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili mwezi January.
james kotei alijiunga na KEIZER CHIEF’S akitokea simba sc kama mchezaji huru mwezi jully.
je Simba watamrejesha kiungo huyo ambaye alikuwa kivutio hasa akifit moja kwa moja katika mifumo ya Patrick?
#sportskitaa

Uongozi yanga wafunguka kuhusu pyramids kuigomea.CCM kirumba

Uongozi wa Klabu ya Yanga umekanusha taarifa za wapinzani wao wa Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), Pyramids FC ya nchini Misri kugomea kutumia Uwanja wa CCM Kirumba wa mkoani Mwanza.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa Yanga utangaze kuuhamishia mchezo huo CCM Kirumba utakaopigwa Oktoba 27, mwaka huu saa kumi jioni. Yanga, awali ilikuwa ikitumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kuhamishia Mwanza.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amelifunulia gazeti hili kuwa taarifa zinazodai wapinzani wao Pyramids kupeleka malalamiko Caf ikipinga mabadiliko ya uwanja waliyofanya siyo kweli.

“Hakuna malalamiko yoyote yaliyopelekwa na Pyramids, hivyo mchezo utachezwa Mwanza kama tulivyopanga awali, tunawafahamu wanaozusha hizo taarifa ni wapinzani hapa nchini.

“Ifahamike kuwa kabla ya kuanza mashindano kila timu ilitakiwa kuwasilisha viwanja viwili ambavyo watavitumia, sisi tuliwasilisha CCM Kirumba na Uwanja wa Taifa ambayo ndiyo viwanja rasmi kwetu,” alisema Mwakalebela.

#BonyezaLikePageNewsUpdates

YANGA KUITUMIA MBAO KUWAMALIZA PYRAMIDS

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema watahakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC ili kujiweka kwenye nafasi nzuri kushinda mechi ya kwanza ya mchujo ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri.

Zahera amesema mara zote mechi dhidi ya Mbao inakuwa ngumu hasa katika uwanja wa CCM Kirumba lakini wamejipanga kupata alama tatu ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji kabla ya kukutana na Pyramids.

Kocha huyo Mkongomani amerejea nchini leo saa 10 alfajiri kutoka nchini Ufaransa alipokuwa na majukumu ya timu yake ya Taifa ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo. “Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mechi ya ligi dhidi ya Mbao ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kushinda mechi ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids. Kama tukiwafunga Mbao wachezaji watakuwa na molari ya kufanya vizuri pia dhidi ya Pyramids,” alisema Zahera.

Yanga itacheza mchezo huo Oktoba 22 na siku tano baadae itawakabili Pyramids katika uwanja huo huo wa CCM Kirumba.

@yangasc @mbaofc

#wapendasokaupdates

RASMI: EL CLASICO YAAHIRISHWA

Bodi ya ligi kuu ya Spain imefikia maamuzi ya kuahirisha mchezo Wa El Clasico baina ya Barcelona dhidi ya Real Madrid kutokana na machafuko ya kisiasa kwenye jimbo la Catalunya.

Mapema week hii mahakama kuu nchini Spain iliwahukumu viongozi Tisa wanaodai Uhuru Wa jimbo hilo kifungo cha miaka 13 mpaka 25 jela hali iliyoleta machafuko na wananchi wengi wakijitokeza katika maandamano mitaani.

Mechi baina ya Barcelona dhidi ya Real Madrid ilipangwa kuchezwa tarehe 26 na sasa imepigwa kalenda mpka mwezi Disemba sababu ikielezwa ni kukosekana kwa usalama

@realmadrid @fcbarcelona
@laliga
#wapendasokaupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started