Pamoja na ubora wao, Manchester City hawajaonekana kama timu isiyofungika katika kipindi cha hivi karibuni, wakipoteza mechi zao mbili kati ya 4 zilizopita, na utakumbuka walikuwa na hawa viumbe wa Palace ambao waliwapa kipigo pekee kwenye ligi katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad msimu uliopita shukrani kwa goli la Andros
Townsend.
Rekodi hii na mwanzo mzuri wa ligi msimu huu chini Roy Hodgson – unawapa matumaini Palace kutopoteza leo.
.
Hata hivyo, City wameshinda pointi 30 kati ya 33 walizotakiwa kushinda hivi karibuni, na ndio ilikuwa timu ya mwisho kuifunga Palace katika dimba la Selhurst katika EPL, ushindi wa 3-1 mnamo mwezi April.
.
Crystal Palace leo wanamkaribisha tena nahodha wao Luka Milivojevic, ambaye alisimamishwa kwenye mchezo vs West Ham.
Mamadou Sakho hatocheza kutokana na maumivu, Connor Wickham pia atakosekana..
.
Manchester City leo wanafurahia kurejea kwa Kevin De Bruyne, John Stones na Benjamin Mendy baada ya kupona majeruhi.
Sergio Aguero alihusika kwenye ajali ya gari wiki iliyopita lakini yupo kucheza. Aymeric Laporte na Leroy Sane bado wataendelea kuwa chumba cha wagonjwa. .
.
Takwimu
β’Crystal Palace wamebeba pointi 4 katika mechi zao 3 zilizopita za ligi dhidi ya Manchester City.
Hata hivyo, The Eagles π¦
hawajashinda mechi hata moja kati ya 4 zilizochezwa nyumbani kwao dhidi ya vijana wa Pep Guardiola- sare 1 na kufungwa 3.
.
β’ Wakati Palace wakiwa na clean sheets 3 kati ya mechi 4 walizocheza nyumbani msimu huu – Manchester City ndio timu yenye safu kali ya ushambuliaji – wamefunga magoli 27, magoli 7 zaidi ya timu yoyote mpaka kufikia weekend hii. .
.
Wazee mikeka, katika #NyumbaYaMabingwa @mbet.co.tz mikeka inasoma kwamba wenyeji Palace wapewa pointi 10.92 na City wamepewa pointi 1.25. Kazi kwako!!!