Jose Mourinho amesema kuwa ana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Roma

Meneja wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa ana mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Roma Cengiz Under majira ya joto (Daily Mail)


Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki mwenye umri wa miaka 22 amesema uhamisho wake utategemea klabu ambayo itashiriki Champions League msimu ujao.

Barcelona na Real Madrid wameingilia dili ya manchester juu ya usajili wa nyota wa Aston Villa Jack Grealish

Barcelona na Real Madrid wameingilia kati dili ya manchester juu ya usajili wa nyota wa Aston Villa Jack Grealish,


Grealish mwenye umri wa miaka 24, yupo kwenye mpango wa Manchester United katika dilisha kubwa
..

United wanakabiliwa na ushindani kutoka uhispania , kwenye vilabu hivyo vyenye uhakika wa kucheza ligi ya mabingwa ulaya (Uefa Champions League)

YIKPE NI STRAIKA BUTU?

.

. Achana na huyo Bernard Morrison hapo, mpira anaujua.. Ana kasi, anakaa kwenye nafasi sahihi, anawafungua wapinzani na kufunga.. Kiwango chake hakina mjadala.. .
. Nataka tumzungumzie huyu Yikpe Gislain. Straika ngongoti kutoka Ivory Coast.. Nini kilimkumba kwenye mchezo dhidi ya Lipuli?
.
. Kwanza mapokeo yake ya mpira siyo mazuri. Akiupokea mpira unakwenda hapa na kule. Kontroo chumba kizima. Mbali na hapo hawezi kukokota mpira wala kupiga Chenga.
.
. Pili anakaa kwenye nafasi vizuri, anawakimbia mabeki vizuri lakini umaliziaji wake ni mbovu. Dhidi ya Lipuli aliwavunja mashabiki wa Yanga moyo aliposhindwa kufunga akiwa peke yake ndani ya sita… Akapiga juu mawinguni.
.
. Akatengenezewa nafasi ya Pili, mapokeo yake mabaya ya mpira yakaua shambulizi. Anatengenezewa nyingine mbili tena akaharibu. Baadaye kocha wa Yanga akaamua kumpumzisha.. Unafikiri hilo ni tatizo kubwa? Hapana.
.
. Tatizo kubwa zaidi ni kwamba hadi Yikpe anatoka Uwanjani jana hakuwa amefanya shambulizi lolote kali la kichwa.. Hakuwa ameshinda mpira wowote wa juu ulioelekezwa kwake.. Hili ndio tatizo.. Unakuwaje straika mrefu halafu hupigi mipira ya vichwa? (Najua tayari amefunga magoli ya vichwa, lakini kwa kimo chake bado haitoshi)
.
. Yaani Yanga jana imepata goli la kichwa kupitia kwa Balama Mapinduzi.. Kipenseli… Kimo cha Balama na kile cha Yikpe nibMbingu na ardhi.. Yikpe anakwama wapi? .
. Nafasi alizopata Yikpe jana ingekuwa ni David Molinga asingetoka bila goli.. Bahati mbaya Molinga aliingia wakati Lipuli wameushika mchezo.. .
. Yikpe anakwama wapi? Hebu tumjadili kwa pamoja..

Uchambuzi wa Azam 1-1 Tanzania Prisons na gift macha

Azam 1-1 Tanzania Prisons.. Mechi bora… Mechi Kali.. Azam imeendelea kuponzwa na ufanisi mdogo wa washambuliaji wake… Waamuzi wa leo Jonesia Rukyaa na Grace Wamara leo walikuwa bora.. Waliamua sahihi kwa karibu kila jambo.. .
. Yanga 2-1 Lipuli .. Mechi bora pia.. Mechi Kali pia.. Yanga ilikuwa bora kipindi cha kwanza.. Krosi mbili mujarabu za Juma Abdul zikazaa magoli mawili.. .
.Yule Yikpe alikuwa ovyo.. Nafasi tatu za magoli yeye kashindwa kufunga hata moja.. Amewaibia wenzie nguvu.. .
. Lipuli walikuwa bora kipindi cha pili.. Kasi nzuri.. Walitengeneza nafasi za kutosha, kama wangekuwa na utulivu wangepata angalau alama moja.. .
.Metacha Mnata leo ametudanganya kwenye ile faulo.. Amepanga ukuta halafu akakaa nyuma ya ukuta tena.. Hii sijui amesomea wapi…David Mwasa ameitendea haki ile fursa. .
.Kenneth Masumbuko leo alikuwa na siku nzuri mchezoni.. Kama ilivyokuwa kwa Bernard Morrison.. Tatizo Morrison leo ametuangusha, hajatembea juu ya mpira..

KonaYaKiufundi Yanga dhidi ya Lipuli Fc

#
.
1. Gem plan ya Lipuli Fc ilikuwa nzuri,kucheza kwa kujihami na kushambulia kwa kuwasapraizi Yanga,maana yake waliiheshimu Yanga,tatizo likawa kuiishi plani yao,kipindi cha kwanza walicheza hovyo sana,ungeweza kudhani hawahitaji alama…..
.
2,Yanga walionekana wazi kuhitaji alama tatu toka dakika ya kwanza,hawakuwa na sababu ya kubaki chini,wakati mpinzani anakubali kufikika,gem plani yao ilikuwa kushambulia lakini zaidi kupitia kwenye flanks,ni wazi mshambuliaji wao ana matatizo ya one Vs One, au One Vs two(yaani akibaki na beki mmoja au wawili hana ujanja wa kumfikia kipa), kupunguza,ni mtu anaehitaji kulishwa zaidi,kama wangepita kati ni dhahiri wangepoteza mipira mingi sana,walipitia pembeni kupitia kwa Abdul na wakafaidika.
.
3. Lipuli na 4:4:2 yao walikuwa wanasafiri bila kujua wanakokwenda,hasa kipindi cha kwanza,walikuwa na lateral mobility nyingi,walidhani namna ya kuwawini Yanga ni kuufungua zaidi uwanja na kuswich mipira kutoka eneo moja kwenda lingine,sawa inawezekana ilikuwa plani nzuri lakini wakiupoteza mpira wanachelewa sana kutengeneza team compaction( kuubana uwanja) na kujikuta wanaacha mianya mingi ambayo ilikuwa faida kwa Yanga….
.
4.Juma Abdul Jafari 🙌 upande wake na mguu wake wa kulia ndio ulioasist magoli yote mawili,ilikuwa ni taiming mbovu ya Dida na mabeki wake,krosi ya kwanza inamaliziwa vyema na Balama,na kisha ya pili inaamua mchezo baada ya Morrison kuzisalimia nyavu…
.
5.Goli la walilopata Lipuli linakuja kuupooza mchezo,Yanga wanaongeza kujihami zaidi lakini lipuli wanashindwa kutumia advantage ya kupata goli kuongeza presha kwa Yanga,mwisho wa siku wanatoka bila alama….
.
6.Papy leo alitulia sana kwenye eneo lake,sehemu ya kugonga alifanya hivyo na kuiweka yanga salama zaidi,Papy ni mchezaji mzuri lakini sio box midfielder,ni box to box midfielder,na ndio maana anajitahidi sana kutulia chini lakini huwa hawezi,anapenda zaidi kuwepo kila mpira ulipo….
.
🎯Kwa ujumla mechi ilikuwa nzuri,na aliyekuja na mbinu nzuri na kuweza kuziishi ndie amepata matokeo..
.
NB: Kona hii leo inampa 👊 Juma Abdul kwa kuwa kwenye kiwango bora zaidi….
.
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo

Dondoo za michezo na Dominick Salamba ⛹


.
💥Yanga yapanda mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, ni baada ya kuifunga Lipuli Fc 2-1 taifa, Azam Fc na Tanzania Prison hakuna mbabe..
.
💥Luis Mikisson ruksa kuitumikia Simba SC,ITC yake yawasili…
.
💥Goli la Mahmoud Trezguet alilowafunga Licester City na kuipeleka Aston Villa fainali ya Carabao Cup, limetangazwa kama goli bora la mwezi januari huko Villa Pack, Aston Villa…
.
💥Ratiba ya robo fainali klabu bingwa na kombe la shirikisho Afrika imetoka,timu timu za kaskazini mwa Afrika zatawala……
.
💥Spurs yaitandika 3-2 Southamton kwenye FA Cup,sasa kukutana na Norwich City..
.
💥Christiano Ronaldo amefikisha mwaka wa 35 hapo jana…
.
💥Simba SC yatembelea kituo cha kulea watoto yatima na kutoa misaada mbalimbali,kituo hicho cha Wali Ul Asr kipo kibaha mkoani Pwani….
.
#bakinasisi__ #njookwetu #TupoNawePaleUlipo

Allan okello kesho atacheza mchezo wa ligi kuu ya Algeria

Kwa mara ya kwanza kabisa nyota wa kimataifa wa Uganda Allan okello kesho atacheza mchezo wa ligi kuu ya Algeria akiitumikia klabu yake ya Paradou Athletic Club dhidi ya US biskra tangu asajiliwe akitokea KCCA umya Uganda

Paradou mpaka sasa wamecheza jumla ya michezo 15 wakiwa wamekusanya alama 18 wakiwa nafasi ya 12 katika timu 16 zinazoshiri ligi kuu ya Algeria Ligue 1

Powered by @sports_lady_tz

MAAJABU HAYATOISHA TANZANIA

Baada ya yale maajabu 7 ya dunia ya kale, wanasema ajabu la 8 liko Tanzania, ambalo ni Ngorongoro Crater.

Lakini nadhani hata ajabu la 9 pia linaweza kupatikana hapa hapa Tanzania; siyo kwenye utalii, bali michezo hususani soka na hasa VPL.

Maajabu haya siyo kwa vipaji vya wachezaji, bali vituko vya waamuzi. Kila siku mpya, waamuzi wetu wanakuja na maajabu mapya.

Unaweza ukajiuliza, sheria wanazotumia ni zile zile za FIFA au wana sheria zao ambazo hata TFF hawazijui…maana na wao hawakubaliani nao kabisa.

Na ndiyo sababu Rais Wallace Karia, ameagiza wadau wanaohusika na masuala ya uamuzi kukutana ili kuangalia namna ya kuboresha utendaji…hata waziri pia katoa tamko.

MAAJABU YA JANA
Ili kuamua kwamba hili ni bao au siyo bao, mwamuzi huongozwa na sheria namba 10 katika zile 17 za FIFA.

Sheria hii inasema ili lihesabike kuwa ni bao, lazima mpira WOTE uvuke mstari wa golini, katikati ya nguzo mbili na chini ya mwamba.
Endapo mwamuzi atapuliza filimbi kuashiria ni bao ilhali mpira haukuvuka mstari, basi mpira unatakiwa uanzishwe tena kwa kudundwa.

Hili la ‘mpira wote kuvuka mstari’, pia utalikuta kwenye sheria namba 9. Hii ni sheria inayohusu mpira kuwa mchezoni au la.

Inasema kwamba mpira utahesabika uko nje ya mchezo endapo WOTE utavuka mstari, aidha wa golini au pembeni.

Hapo kwenye ‘mstari wa golini’, ndipo inapomaanisha ni BAO.

KWENYE TUKIO

Mwamuzi msaidizi aliashiria kona, akiwa na maana aliuona mpira WOTE umevuka mstari. Ina maana aliona umevuka lakini siyo katikati ya nguzo mbili na chini ya mwamba?

Maana ili tumeona sheria namba 10 ikisema ili liwe bao lazima mpira uvuke mstari wa golini katikati ya nguzo mbili na chini ya mwamba.

Hapa ndo kwenye shida, mpira ulivuka mstari au haukuvuka?

Na kama haukuvuka, kwanini iwe kona?

Na kama ulivuka, ulivukia katikati ya nguzo mbili na chini ya mwamba au siyo?

Kama ni katikati ya nguzo mbili na chini ya mwamba, kwanini lisiwe bao?

Uliendelea kuwaza sana utajikuta ndiyo umeshaanza kufanya utalii wa ndani kwenye mbuga za VPL, ukishuhudia maajabu ya 9 ya dunia.

Maajabu hayatoisha Tanzania!

Cc @zakazakazi
Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Unamkumbuka huyu jamaa kwenye upara..!?

Basi huyu jamaa ni kiungo wa kazi wa mapira pale Afrika Kusini

Jina la kamili anaitwa Samuel Tiyani Mabunda ila wenyewe wa South hususani mashabiki wa klabu ya Mamelod Sundowns wanapenda kumuita “Mabunda”

Mabunda alizaliwa April 17, 1988 kwa sasa anachezea klabu ya Mamelod Sundowns “Masandawana” au The Brazilians na ana umri wa miaka 31 kwa sasa

Mabunda alikuwa moja kati ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Afrika Kusini Bafana Bafana kilichofanya vema kwenye michuano ya Afcon mwaka jana nchini Misri kwenye eneo la kiungo akiwa na wachezaji wengine kama Thembankosi Lorchi , Lebogang Manyama na Themba Zwane pia Thapelo Morena

Mabunda alizaliwa kwenye mji wa Polokwane uliopo kwenye jimbo la Limpopo Gauteng Afrika Kusini

Mabunda alianza kucheza soka la ushindani rasmi mwaka 2009 ambao alianza kuchezea klabu ya Arcadia Sherphers ya hapo hapo Afrika Kusini mpaka mwaka 2010

2010 alijiunga na Black Leopards ambayo aliichezea misimu mitatu aliicheza michezo 58 na kufanikiwa kuifungia goli 5

Baadae mwaka 2013 alijiunga rasmi na Mamelod Sundowns alicheza msimu mmoja akatolewa kwa mkopo kwenye klabu ya Free State United mpaka mwaka 2015 ambapo alirejea rasmi Mamelod Sundowns klabu ambayo anaitumikia mpaka sasa akiwa amecheza jumla ya michuano 71 akifunga goli moja

Mabunda alianza kuitumikia timu ya taifa ya Afrika Kusini Bafana Bafana mwaka 2016

Jamaa alikuwa mstari wa mbele sana kutoa burudani ya nyimbo za hamasa kwa vijana wa Bafana Bafana wakati wa michuano ya Afcon mwaka jana

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Yaya Mohammed na Burekemu wafanya vema mwezi January ligi kuu ya Ghana

Yaya Mohammed na Burekemu wafanya vema mwezi January ligi kuu ya Ghana #NascoPremierLeague

Mshambuliaji wa zamani kwa klabu ya Azam fc anayechezea klabu ya Aduana Star’s ya Ghana Yaya Mohammed amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi January kwenye ligi kuu ya Ghana

Pia kocha Berekum Chelsea’s wa klabu ya Asare Baedioko naye amechaguliwa kuwa kocha Bora wa mwezi January wa ligi hiyo

Tuzo hizo zilitangazwa Jana usiku

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Design a site like this with WordPress.com
Get started