
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC hautakuwa rahisi, anaamini Azam ni moja ya timu bora Tanzania.
Simba na Azam Fc zitacheza Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ikiwa ni mara ya pili msimu huu baada ya kukutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii na Simba kushinda 4-2.
Aussems amesema anawaheshimu Azam Fc kwani wana timu nzuri kwa sasa lakini malengo ya kikosi chake ni kushinda mchezo huo
“Niliwaona Azam FC tangu msimu uliopita ni miongoni mwa timu nzuri za Tanzania, katika mpira hakuna mchezo rahisi, lakini tunajiandaa kupata matokeo mazuri tukijua ni wapinzani wa aina gani”
Simba ilitumia vyema mapumziko wa kalenda ya Fifa katika kujiimarisha kwa michezo mitatu ya kirafiki ambapo walishinda miwili na kupata sare moja.












