Mtibwa yapata ushindi wakwanza ligi kuu

Juzi timu ya Mtibwa Sugar ilipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kuwachapa wenyeji, Ndanda FC 1-0 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mtibwa Sugar, mabingwa wa Ligi Kuu misimu miwili mfululizo 1999 na 2000 wamefikisha pointi tano baada ya kucheza mechi sita, nyingine tano wakifungwa tatu na kutoa sare mbili.

Bao pekee la Mtibwa Sugar lilifungwa na beki wake wa kati Dickson Daud Mbekya dakika ya 35, akimalizia pasi ya beki wa kulia, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’

Kwa miaka ya hivi karibuni Mtibwa Sugar imekuwa ikianza ligi kwa kasi lakini hali ilikuw tofauti msimu huu

Wamelazimika kusubiri mpaka raundi ya sita kupata ushindi wao wa kwanza msimu huu

Sio dalili nzuri kwao, kocha Zubery Katwila ana kazi ya kufanya kuhakikisha timu hiyo haiingia katika hatari kupigania kutoshuka daraja

Yanga yapunguza viingilio pyramids

Baada ya kupokea malalamiko, ushauri na mapendekezo mbalimbali, uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa utapitia upya viingilio vilivyowekwa kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa play-off kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids

Hivi karibuni Yanga ilitangaza viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa Jumapili, Oktoba 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba

VIP ni Tsh 50,000/-, Royal ni Tsh 70,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-

Hata hivyo wadau mbalimbali wamehofia kiingilio cha Mzunguuko kuwekwa Tsh 10,000/- itakuwa kikwazo kwa mashabiki wengi kushuhudia mchezo huo

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wanafanyia kazi malalamiko, ushauri na mapemdekezo waliyopewa na wadau ili kuhakikisha mashabiki wengi wanajitokeza uwanja wa CCM Kirumba kushuhudia mchezo huo

Mwakalebela yuko jijini Mwanza akiongoza safu ya viongozi wa timu hiyo walioweka kambi kuhakikisha mwarabu hatoki salama Tanzania OKtoba 27

Idadi ya Mataifa 16 yatakayoshiriki Michuano ya CHAN 2020 huko Cameroon 🇨🇲

✍🏻 Idadi ya Mataifa 16 yatakayoshiriki Michuano ya CHAN 2020 huko Cameroon 🇨🇲 yamejulikana… Michuano hii kuanza kupigwa January 2020..

👉🏻 Wenyeji Ni Cameroon 🇨🇲 wakishiriki kwa mara ya nne Michuano hii, wakati Bingwa mtetezi wa Michuano hii ni Morocco 🇲🇦 ambaye Pia anashiriki kwa mara ya Nne.. Wakati huo huo, Timu ya taifa ya Togo 🇹🇬 wao kwa mara ya kwanza kabisa katika historia wanashiriki Michuano hii..

👉🏻 Tanzania 🇹🇿, waliokuwa wa kwanza kabisa Kufuzu kushiriki Michuano hii, wanaenda katika Michuano hii kwa mara ya pili katika historia Sambamba na Namibia 🇳🇦 nao ni Mara ya pili… Tunisia 🇹🇳, Guinea 🇬🇳, Niger 🇳🇪, Burkina Faso 🇧🇫 na Congo 🇨🇬, Mataifa hayo yotee yanashiriki kwa mara yao ya tatu katika historia yao.

✍🏻 Zambia 🇿🇲, Rwanda 🇷🇼 na Mali 🇲🇱, Mataifa yoote haya yanashiriki kwa mara ya Nne ukijumihisha Mwenyeji na Bingwa Mtetezi… Mataifa ya Zimbabwe 🇿🇼, Uganda 🇺🇬 na DR Congo 🇨🇩, Ndio Nchi ambazo zimeshiriki mara nyingi zaidiii kati ya Nchi zote zilizofuzi Michuano, Mwakanj inakuwa ni mara yao ya tano (5).
#TotalCHAN2020 #CHAN2020Qualifiers
@Harunlugoyah

Chelsea itabakia kuwa Klabu pekee kuanza msimu wa Ligi na kushinda game zooote

Ole Gunnar Solskjær akiiongoza Manchester United inakatisha mfululizo wa Ushindi kwa Liverpool, game hii Liverpool waliitaji ushindi Ili kuifikia rekodi ya Man City..

– Wakati huo huo, Chelsea itabakia kuwa Klabu pekee kuanza msimu wa Ligi na kushinda game zooote Tisa za Mwanzo mfululizo… Jose Mourinho akiweka rekodi hiyo 🙌.
#PremierLeague #PLUpdates
@Harunlugoyah

FULL-TIME: CHAN 2020 Qualifier Final Round 2nd Leg

Ivory Coast 🇨🇮 1-0 Niger 🇳🇪 (Agg 1-2).
Libya 🇱🇾 1-2 Tunisia 🇹🇳 (Agg 1-3).
Mali 🇲🇱 2-0 Mauritania 🇲🇷 (Agg 2-0).
Burkina Faso 🇧🇫 0-0 Ghana 🇬🇭 (Agg 1-0).
DR Congo 🇨🇩 4-1 Central Africa Republic 🇨🇫 (Agg 6-1).
Congo 🇨🇬 1-0 Equatorial Guinea 🇬🇶 (Agg 3-2).
Lesotho 🇱🇸 0-0 Zimbabwe 🇿🇼 (Agg 1-3).
Guinea 🇬🇳 1-0 Senegal 🇸🇳
(Agg 1-1).
(Penalty 3-1, Guinea anasonga CHAN).
….
✍Yametimia Mataifa 16 Sasa baada ya Mataifa Nane yaliyosalia kukamilisha mataifa 16 yatakayoshiriki Michuano ya CHAN 2020 huko Cameroom kukamilika hii Leo…
#CHAN2020Qualifiers #TotalCHAN2020

Manchester united….kibaruani na livepool

14 – Ndugu zetu, Manchester United Leo wana kibarua mbele ya Liverpool ikiwa kinara katika Msimamo wa Premier League huku wao wakiwa nafasi ya 14; Katika nafasi hiyo, Man United ipo nafasi ya chiniii mno inapokutana na Liverpool katika game ya yao msimu wa Ligi.

– Mara yao ya kwanza kuwa nafasi ya chini afu wanaenda kukabiliana na Liverpool katika game ya Ligi ilikuwa ni Machi 18,1990 walipokuwa nafasi ya 16… Kwa kuongezea tu, Game hiyo Manchester United ilikufa 2-1 hapo hapo Old Trafford, Magoli mawili ya John Barnes.

1996 – Hii ni mara ya kwanza Liverpool kukumbana na Manchester United wakati ikiwa kinara katika Msimamo wa Premier League tangu mara ya mwisho Oktoba 1996 – Kwa Kuongezea tu, Man United ilishinda 1-0 kwa goli Pekee la Legend, David Beckham..
#PremierLeague #MUNLIV
@Harunlugoyah

TAREHE NA MWEZI KAMA WA LEO, MNAMO MWAKA 2013.. Ilipigwa Mechi ya Watani wa Jadi

📅 TAREHE NA MWEZI KAMA WA LEO, MNAMO MWAKA 2013.. Ilipigwa Mechi ya Watani wa Jadi Nchini Simba SC dhidi ya Yanga SC, Game ambayo ni miongoni mwa mechi isiyosahaulika katika historia ya Miamba hawa.
.
– Ilikuwa ni Dakika ya 15 tu, Mrisho Ngassa aliyekuwa kipenzi cha Wananchi, anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya kuiwahi krosi ya Mshambuliaji hatari wa Burundi 🇧🇮, Didier Kavumbagu…Yanga waliaanza mchezo kwa pasi za uhakika huku wakiwapa Simba taabu mno hasa eneo la kiungo likiongozwa nao Niyonzima, Domayo & Chuji.. Ilikuwa ni Dakika ya 36 ya mchezo, Mshambuliaji wa Uganda 🇺🇬, Hamis Kiiza “Diego” anaifungia Yanga SC bao la pili baada ya beki Wa Simba, Haruna Shamte “Terminator” kujichanganya mpira wa kurusha wa Mbuyu Twite ulioguswa na Didier Kavumbagu kwa kichwa.
.
– Mda mchache kabla ya Mapumziko Show game ilianza kwa Wananchi wakiamini game imeisha hii, Walikalia mpira na madoido kibao 😂😂, huku wale wa Simba wakianza kutoka uwanjani, MNAMO dakika ya 45, Yule yule Kiiza Diego anaifungia Yanga bao la tatu baada ya Kavumbagu kugongeana vizuri na kiungo wa Rwanda 🇷🇼, Haruna Niyonzima..
👉 HALF-TIME: Yanga SC 3-0 Simba SC
[Kiiza ⚽⚽, Ngassa ⚽].
.
– Simba wanaonekana kupoteana huku Yanga wakishambulia na kupoteza nafasi nyingi za Magoli… Ilikuwa dakika ya 53, Mshambuliaji, Betram Mwombeki anaipatia Simba SC bao la kwanza baada ya pasi ya Mshambuliaji wa Burundi 🇧🇮, Amis Tambwe…Simba wanaonekana kubadilika kipindi cha pili baada ya kuwatoa Humud na Haruna Chanongo kisha kuwaingiza chipukizi, William Gallas na Said Ndemla ambaye alikuja kuubonda mwingi Mno… Mnamo dakika ya 57, Simba wanafumania nyavu za Yanga kwa mara ya pili goli likifungwa nae Joseph Owino baada ya kuunganisha vizuri mpira wa kona wa Ramadhan Singano “Messi” wakati mabeki wa Yanga wakiwa wamezubaa.. Dakika ya 64, Ngassa anawatoka Mabeki Owino na Kaze, anabaki yeye na kipa, lakini anakosa goli la waziii baada ya kipa kuokoa…. Dakika ya 84, Beki wa Kimataifa wa Burundi 🇧🇮, Gilbert Kaze anawainua wana Simba waliokata tamaa kwa kufunga goli kwa Kichwa akiungamisha krosi ya faulo ya Nahodha, Masoud Nassor “Chollo”..

FULL-TIME 💓 3⃣ – 3⃣ 💛
#SimbaSC #YangaSC
@Harunlugoyah

Tairone akumbwa na tikio.lisiloelezeka

Juzi beki Tairone Da Silva alikumbwa na tukio lisilo la kawaida baada ya kuanguka akiwa kwenye mazoezi ya kikosi cha Simba uwanja wa Uhuru

Tukio hilo lilipelekea sintofahamu ya muda mfupi kabla ya kupewa huduma ya kwanza

Daktari wa Simba Dk Yassin Gembe amesema tukio hilo lilisababishwa na joto kali

Dk Gembe amefafanua kuwa Tairone alipata na kizunguzungu kutokana na jua kali lililokuwa likiwaka wakati wachezaji wakiendelea na mazoezi

Tairone alirejea kwenye hali ya kawaida baadae na kuendelea na mazoezi

Design a site like this with WordPress.com
Get started