
– Wasafi Media Imethibitisha kuwa hivi karibuni watafungua kituo cha Kukuzia vipaji vya Soka Nchini (Academy)… Kituo hicho kinatarajia kujengwa Mkoani Morogoro..👏👏👏
#Updates #SokaPlaceUpdates

– Wasafi Media Imethibitisha kuwa hivi karibuni watafungua kituo cha Kukuzia vipaji vya Soka Nchini (Academy)… Kituo hicho kinatarajia kujengwa Mkoani Morogoro..👏👏👏
#Updates #SokaPlaceUpdates

Uongozi wa klabu ya Yanga umetimiza ahadi yake ya kupunguza bei ya viingilio vya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Jumapili Oktoba 27 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema baada ya kupokea malalamiko, mapendekezo, maoni na ushauri kutoka kwa wadau, wamepunguza bei hizo za viingilio
Hii hapa bei mpya za viingilio;
Royal – Tsh 50,000/-
VIP – Tsh 20,000/-
Mzunguuko – Tsh 7,000/-
Aidha Mwakalebela amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Oktoba 27 kuiunga mkono timu yao ili kuhakikisha wanashinda mchezo wa kwanza dhidi ya Pyramids Fc
Amewataka wadau wote kukata tiketi halali ili pamoja na kupata burudani, waweze kuichangia timu yao kupitia viingilio hivyo
“Baada ya makato yote, Yanga tutapata asilimia 42 ya mapato yote yatakayopatikana. Hivyo tunawaomba mashabiki na wadau wote kukata tiketi halali na kuingia uwanjani kwa utaratibu rasmi uliowekwa.”

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), katika kikao chake cha Oktoba 19 2019 pamoja na mambo mengine, imeongeza muda wa kuchukua na kurudisha fomu za uchaguzi mdogo wa Bodi ya Ligi (TPLB)


Klabu ya Azam FC imethibitisha kumrejesha aliyewahi kuwa kocha wao Mkuu, Aristic? Cioaba kuwa kocha wao mpya kwa mara nyingine tena
Kocha huyo raia wa Romania alijiunga na Azam FC January 2017 na kumtimka Mei 2018 na kujiunga na Klabu ya Sohar FC ya ligi Kuu nchini Oman
Nafasi yake ilichukuliwa na Mdachi, Hans Van Der Pluijm ambaye baadae nae akaondolewa na Etienne Ndayiragije kukabidhiwa mikoba mwanzoni mwa msimu
Cioaba amechukua nafasi Ndayiragije ambaye yupo mbioni kutangazwa kuwa kocha wa kudumu wa Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’
#EnglandPremierLeague
22:00 Sheffield United vs Arsenal
:
#ItalySerie A
21:45 Brescia vs Fiorentina
:
#NetherlandsEersteDivisie
21:00 Jong AZ Alkmaar vs NEC Nijmegen
21:00 Jong Ajax vs Jong FC Utrecht
21:00 Jong PSV vs FC Eindhoven
21:00 NAC Breda vs De Graafschap
:
#EgyptPremierLeague
18:30 El Entag El Harby vs Pyramids FC
21:00 Al Masry vs FC Masry
:

⚽️ Gabriel Jesus, ni Mchezaji wa Saba kufunga Magoli 5️⃣0️⃣➕ katika Klabu ambayo ipo chini ya kocha Mkuu, Pep Guardiola..
…
– Guardiola kafundisha vilabu vitatu vikubwa barani Ulaya, na kuwaongoza Wachezaji zaidi ya wawili katika timu moja kufikisha Magoli 5️⃣0️⃣➕ chini yake… Wachezaji Wengine Sita ni pamoja na.
– Lionel Messi – Magoli 2️⃣1️⃣1️⃣ (FC Barcelona).
– Sergio Agüero – Magoli 1️⃣0️⃣3⃣ (Man City).
– Thomas Müller – Magoli 7️⃣9️⃣ (Bayern Munich).
– Raheem Sterling – Magoli 6️⃣7️⃣ (Man City).
– Robert Lewandowski – Magoli 6️⃣7️⃣ (Bayern Munich)
– Pedro – Magoli 5️⃣8⃣ (FC Barcelona).
#Updates #PepGuardiola
@Harunlugoyah

Kiungo Jonas Mkude na Clatous Chama jana walikuwepo uwanja wa Uhuru kwenye mazoezi ya kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba
Chama alishiriki mazoezi hayo kikamilifu wakati Mkude aliyerejea juzi kutoka Sudan alikoisaidia Stars kufuzu fainali za CHAN, hakufanya mazoezi
Kurejea kikosini kwa nyota hao kunaaminisha uongozi wa Simba umamaliza sintofahamu iliyokuwa ikiwakabili
Leo kiraka Erasto Nyoni na Gadiel Michael nao wanatarajiwa kujumuika kwenye mazoezi hayo yakiwa ni maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa

Pamoja na kutopewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool jana, Manchester United nusura iwe timu ya kwanza kuifunga Liverpool msimu huu kama sio bao la Adam Lallana alilofunga dakika ya 85 kuinusuru Liverpool na kipigo
Marcus Rashford iliitanguliza United kwa kuifungia bao kwenye dakika ya 36 akimalizia krosi murua ya Daniel James
Bao hilo liliibua sintofahamu pale uamuzi wa VAR ‘ulipopotezea’ madhambi aliyofanyiwa Divoc Origi na Lindelof kabla ya mpira kumfikia James
Mkufunzi wa Man Utd Ole Gunnar Olskjaer alibadili mfumo wa uchezaji wa kikosi chake kwa kutumia walinzi watatu nyuma, mabadiliko ambayo yalichangia kuweza kuidhibiti Liverpool ambayo haikuwa imepoteza alama hata moja msimu huu
Liverpool ilimiliki mchezo kwenye dakika 15 za mwisho na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Lallana
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amelalamikia maamuzi ya VAR kuwa hayakuwatendea haki kwa kulikubali bao la United
Aidha ameponda mfumo uliotumiwa na United kuwa ulikuwa wa kujihami zaidi

Timu ya Biashara United jana ilipata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mbeya City 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Baada ya kupoteza mechi nne na kutoa sare moja, hatimaye Biashara United ilishinda kupitia mabao ya Ally Kombo dakika ya 67 na Innocent Edwin dakika ya 89
Mbeya City inayonolewa na Juma Mwambusi nayo inasuasua msimu huu ikiwa haijaonja radha ya ushindi
Imeshuka dimbani mara tano, ilitoka sare mara nne kabla ya kipigo cha jana
Nao Coastal Union walitumia vyema uwanja wa nyumbani, Mkwakwani mjini Tanga baada ya kuichaoa Mwadui FC 2-1 huku Polisi Tanzania ikipata ushindi kama huo dhidi ya Mwadui Fc

Mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumatano, Oktoba 23, utachezwa uwanja wa Taifa
Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia majira ya saa 11 jioni
Hii itakuwa mara ya pili kwa Simba na Azam Fc kukutana kwenye uwanja huo msimu huu
August 17 zilikutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii Simba ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2
Mabao ya Simba yakifungwa na Sharaff Shiboub (2), Clatous Chama na Francis Kahata