Arsenal imepoteza game Nne kati ya Saba zilizopita za Premier League wakiwa Ugenini

4 – Arsenal imepoteza game Nne kati ya Saba zilizopita za Premier League wakiwa Ugenini dhidi ya Timu iliyotoka kupanda Daraja… Rekodi inaendeleq kuwatesa, Arsenal haijawahi kushinda game ya Premier League ugenini ikiwa tu wametoka kupigwa katika kipindi cha kwanza tangu Oktoba 2011 mpaka leo bado wanateseka… Mechi 12 vs Sheffield, wameshinda moja tu..
#SHUARS #PremierLeague

Tetesi za usajili Ulaya leo jumatatu

Real Madrid inawafuatilia winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19 na mshambuliaji wa Norway wa miaka 19- Erling Braut Haaland, anayechezea Red Bull Salzburg. (El Desmarque, via Mail)

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani na RB Leipzig Timo Werner,23 ambaye aliwahi kuhusishwa na tetesi za kujiunga na Liverpool. (Express)

Manchester United inajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uingereza Angel Gomes, 19, licha ya tetesi kuwa Barcelona inamtaka. (Sun)

Newcastle United inamfuatilia mshambuliaji wa Lille na Nigeria wa miaka 20 Victor Osimhen. (Chronicle)

Meneja wa Chelsea Frank Lampard anataka mshamsmbuliaji wa Ufaransa wa miaka 33, Olivier Giroud, ambaye hajafurahishwa na hatua ya kutojumuishwa katika kikosi cha kwanza aendelee kusalia Stamford Bridge. (Telegraph)

Chelsea imemuongeza aongeza mchezaji wa safu ya kati wa Atalanta na Ukraine Ruslan Malinovskyi, 26, katika orodha ya wachezaji amabao huenda wakahamia klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Express)

Beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 28, anasema angelijiunga na Everton msimu huu lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hakuridhishwa na ofa aliotolewa na klabu hiyo. (Het Laatste Nieuws, via Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, 28, anapanga kurejea katika ligi kuu ya ya England baada ya kupona jereha la mguu katika mechi ya klabu hiyo dhidi ya Sheffield United siku ya Jumatatu. (mail)

Meneja wa Uholanzi Ronald Koeman angependelea kuwa msimamizi wa klabu ya Barcelona siku moja na anasema kuwa mkataba wake una kifungu cha sheria kinachomruhusu kuajiriwa na baada ya mashindano ya Ulaya mwaka 2020, amesema mkurugenzi wa michezo wa shirikisho la kandanda la Uhuolanzi, Nico-Jan Hoogma.(Fox Sports, via Marca)

BBC

Ndayiragije amkaribisha Cioaba

Pichani juu kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akiwa sambamba na mtangulizi wake, Etienne Ndayiragije, anayekwenda kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Wawili hao wamekutana makao makuu ya Azam FC (Azam Complex) wakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, kukabidhiana kijiti, ikiwemo Ndayiragije kuwaaga wachezaji na kwenda kwenye majukumu yake mapya ya timu ya Taifa.

Wawa apata jeuri..mechi tatu za kirafiki

Beki Paschal Wawa amesema mechi tatu za kirafiki walizocheza zinawapa matumaini ya kufanya vizuri dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa keshokutwa Oktoba 23 uwanja wa Taifa.

Simba ilianza kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Bandari uwanja wa Uhuru ikashinda kwa bao 1-0 kisha ikakwea pipa kuwafuata Mashujaa mkoani Kigoma ikashinda bao 1-0 kabla ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Aigle Noir ya Burundi

Wawa amesema kuwa namna kikosi kilivyocheza michezo hiyo, wamezidi kuimarika huku wakiweza kufanyia kazi mbinu mbalimbali walizopewa na kocha Patrick Aussems

“Hatuna kingine ambacho tunakifikiria kwa sasa, kikosi kimecheza michezo mingi ya kirafiki jambo ambalo limetufanya tuwe na muunganiko mzuri, ni wakati wetu kuonyesha kile tulichojifunza kwa vitendo katika michezo yetu yote ikiwa ni pamoja na huu dhidi ya Azam FC”

uwanja wa Sheikh Amri Abeid kitumika ligi.kuu

– Uongozi wa Klabu ya Singida United Umethibitisha kwa watatumia uwanja wa Sheikh Amri Abeid Huko Mkoani Arusha kwa mechi mbili zijazo za Ligi Kuu Tanzania Bara ambazo wao watakuwa wenyeji wa game hizo..

– Akithibitisha hilo Mkurugenzi wa Klabu hiyo, Clement Sanga amesema kuwa ni kweli wamehama uwanja wao Wa Namfua huko Singida kwasababu ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Nchini “TFF” ili kupisha Marekebisho katika eneo la kuchezea yaani Pitch, Sanga amesema kuwa Pia wao walipokea malalamiko kutoka kwa Wachezaji wao kwamba uwanja hauna viwango na unawanyima wao fursa ya wao kupata Matokeo, hata wageni wa mechi wamekuwa wakilalamikia ubovu wa uwanja… Katika Mechi mbili zijazo Singida itavaana na Simba SC 27/10/2019 huku game ya pili ni dhidi ya JKT Tanzania 30/10/2019..
#VPLUpdates #VPL
@Harunlugoyah

Singida.united. yahamia.arusha

Singida United imetangaza kucheza mechi zake mbili za ligi kuu ya Vodacom kati ya Simba na JKT Tanzania kuchezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Uwanja wa Namfua ambao hutumiwa na Singida kama uwanja wa nyumbani umefungiwa na Bodi ya ligi kutokana na kutokidhi vigezo.

Awali Singida ilitangaza kutumia uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma katika kipindi chote ambacho Namfua ipo katika ukarabati kabla ya leo kutangaza mabadiliko hayo.

Mechi dhidi ya Simba imepangwa kuchezwa siku ya Jumapili, Oktoba 27 na ule wa JKT Tanzania utapigwa Oktoba 30.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa klabu hiyo Festo Sanga imesema kipindi hichi ambacho uwanja wa Namfua unaendelea na ukarabati watakuwa wanatumia dimba hilo la Arusha.

@officialsingidaunitedfc @simbasctanzania

#wapendasokaupdates

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ni “ukweli” kwamba Manchester United kila wakati imejiandaa kupaki basi

– Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa ni “ukweli” kwamba Manchester United kila wakati imejiandaa kupaki basi dhidi ya upande wake wanapokutana huko Old Trafford… Klopp na Liverpool yake walihitaji kusawazisha dakika za mwisho kupitia kwa Adam Lallana jana Jumapili ili kupata sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United ya Ole Gunnar Solskjaer, ambao wana pointi mbili juu ya eneo la kushuka daraja.

– Mjerumani huyo ameshindwa kupata ushindi katika mechi zake tano za Ugenini dhidi ya United… Ole Gunnar Solskjaer ndiye meneja pekee Jurgen Klopp amekutana nae zaidi ya mara moja kwenye Ligi Kuu na akashindwa kupata Ushindi.

🗣”Mwaka huu, mwaka jana, mwaka juzi, walijipanga kuzuia tu,” alisema… “Ndivyo ilivyo. Ni sawa. Hakuna kukosoa. Ni ukweli tu… Alisema Klopp 😆😆.
#PremierLeague #ManchesterUnited #Liverpool
@Harunlugoyah

Liwandowski aweka rekodi.mpya bundesliga

– IN-FORM Robert Lewandowski amekuwa ni Mchezaji ni wa pili katika historia ya Bundesliga kufunga katika kila moja ya mchezo katika mechi zoote Nane za mwanzo wa msimu wa Ligi, baada ya kuifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang aliyoweka mnamo 2015-16.

– Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Poland pia ni mchezaji wa kwanza wa Bayern Munich kufunga mabao katika mechi nane mfululizo za Ligi tangu nyota wa zamani wa Kimataifa wa Uholanzi, Roy Makaay mnamo 2005… Hii ni mara ya pili kwa Lewandowski mwenye umri wa miaka 31 kufunga magoli 12 katika mechi nane za ufunguzi wa msimu wa Bundesliga, akiwa amefanya hivyo pia mnamo 2015-16.

– Mshambuliaji wa zamani wa Bayern na Ujerumani Gerd Muller (1968-69) na Mshambuliaji wa zamani wa FC Koln, Christian Muller (1964-65) ndio wachezaji wengine pekee waliofanikisha kiwango kama hicho katika Ligi Hiyo Kuu ya Ujerumani.
#Lewandowski #Bundesliga
@Harunlugoyah

Design a site like this with WordPress.com
Get started