Kiungo mkata umeme Gerson Fraga amesema anatambua Azam Fc ni moja ya timu bora kwenye ligi msimu lakini wao hesabu zao ni kuhakikisha wanashinda Jumatano
Simba na Azam Fc zitakutana Jumatano kwenye mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa uwanja wa Taifa
Akizungumza jana jioni baada ya mazoezi ya Simba yaliyofanyika uwanja wa Uhuru, Fraga alisema anawasubiri Azam Fc kwa hamu
“Azam Fc wana timu nzuri sana tunafahamu, lakini tunafanya maandalizi kabambe ili kuhakikisha tunshinda mchezo huo”
“Tumeusubiri sana mchezo huu ili tuendelee kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema
Nae mlinda lango Beno Kakolanya ambaye alidaka katika mchezo wa Ngao ya Jamii amesema pamoja na Simba kuibuka na udhindi kwenye mchezo huo, Azam Fc walitoa upinzani mkali hivyo wanapaswa kujiandaa kikamilifu ili kuhakikisha wanashinda tena Jumatano





Kikosi cha Yanga kiko mkoani Mwanza ambapo leo jioni watashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom



