
Mambo kadhaa niliyoyaona kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Yanga, dhidi ya Mbao FC.
.
.
Mfumo wa Yanga na Mbao ni moja wa 4-4-2 ila majukumu mbali mbali ya kimbinu yaliamua kwenye mchezo huu ukitizama mchezo moja moja wa hizi timu mbili unaona kabisa Yanga, wana wachezaji wazuri kuliko mbao. .
.
Eneo la kiungo Feisal Salum,leo ametumika kiungo mkabaji amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya majukumu yake shida kubwa ilikuwa kwa Tshishimbi, ambaye alikuwa akicheza namba 8 sio mtulivu anakaa na mpira sana pasi hazifiki nilikuwa nashindwa kumuelewa anazunguka uwanja mzima.
.
.
Balama Mapinduzi, kiungo mshambuliaji wa pembeni ni mtulivu sana akiwa na mpira anajua afanye nini mda huu mpira yote alikuwa akipeleka kwenye eneo la ushambuliaji, asilimia 80 lillikuwa bado tatizo kwa Yanga. .
.
Ali Ali, leo kaonyesha kiwango kizuri kwenye eneo pa beki wa kati anakaba vizuri mpira ya juu yote ilikuwa ikiishia kwake Yondani, hakuwa na wakati mgumu sana 🙌.
.
.
Yule beki wa pembeni wa Mbao Fc, Emannuel Charles anajua sana anashambulia ni mzuri wa kupiga krosi anajua kukaba binafsi nimependa sana uwezo wake. .
.
Saidy Junior, kipindi cha kwanza mchezo haukumuhitaji ila yeye alikuwa anahuhitaji, muda mwingi alikuwa akicheza faulo sana kipindi cha pili kuingia kwa Waziri Junior, kulikuja kumresheja mchezoni muda ulikuwa sio rafiki kwao. .
.
Safu ya ulinzi ya Mbao imecheza kwa nidhamu sana ya hali ya juu ilikuwa ni ngumu kwa kiasi chake kuipita.
.
.
NB: hivi Yanga, na Waarabu ni lini?? CCM Kirumba pale sio mchezo. .
.
✍🏻@azizi_mtambo_15







.




