WAARABU WA YANGA MAMBO MAGUMU

apinzani wa Yanga, Pyramids FC mambo magumu baada ya juzi kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa pili mfululizo kufuatia kulazimishwa suluhu dhidi ya Smouha.
Huo ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya
nchini Misri uliopigwa kwenye uwanja wao wa nyumbani ikiwa ni siku chache kabla
ya kuvaana na Yanga Oktoba 27, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Pyramids, mchezo uliopita wa ligi
ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Al
Gaish, licha ya kuendelea kukaa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi nane.
Wapinzani hao wa Yanga, wameshinda michezo yake miwili ya kwanza dhidi ya ENPPI na Tanta pekee yote iliicheza
kwenye uwanja wao wa nyumbani.
Timu hiyo inatarajiwa kutua nchini wiki hii
kuikabili Yanga kwenye mchezo wa
kwanza wa mtoano Kombe la Shirikisho
ambao utapigwa Uwanja wa CCM
Kirumba.
Yanga tayari ipo kambini Mwanza tayari
kukabiliana na wapinzani wao hao baada
ya kumaliza kucheza mchezo wa Ligi Kuu
Bara dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Wakati Pyramids ikitoa sare michezo
miwili na kushinda miwili, Yanga wenyewe
wamecheza michezo mitatu kati ya hiyo
wameshinda mmoja na Coastal Union
huku wakifungwa mmoja dhidi ya Ruvu
Shooting na sare moja dhidi ya Polisi
Tanzania.

#LikePageNewsUpdates

TFF YAPANGUA MECHI YA SIMBA NA AZAM

✍na saboso Gin jr
Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya Azam Jumatano ya kesho, Bodi ya Ligi kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imepangua ratiba ya mechi hiyo.

Awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 10 kamili katika Uwanja wa Taifa lakini baadaye ikapanguliwa na sasa itachezwa majira ya saa 11 za jioni.

Uamuzi wa kubadili muda wa mechi hiyo umekuja ili kuwapa nafasi mashabiki watakokuwa makazini kupata muda wa kuitazama mechi hiyo.

Mabadiliko mengine ni juu ya Uwanja ambapo awali ilipaswa mechi ichezewe Uhuru lakini kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe aliruhusu ipigwe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
#sportskitaa #sportskitaa

TFF YAPANGUA MECHI YA SIMBA NA AZAM

✍na saboso Gin jr
Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya Azam Jumatano ya kesho, Bodi ya Ligi kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) imepangua ratiba ya mechi hiyo.

Awali mechi ilipangwa kuchezwa saa 10 kamili katika Uwanja wa Taifa lakini baadaye ikapanguliwa na sasa itachezwa majira ya saa 11 za jioni.

Uamuzi wa kubadili muda wa mechi hiyo umekuja ili kuwapa nafasi mashabiki watakokuwa makazini kupata muda wa kuitazama mechi hiyo.

Mabadiliko mengine ni juu ya Uwanja ambapo awali ilipaswa mechi ichezewe Uhuru lakini kupitia Waziri mwenye dhamana ya michezo, Harrison Mwakyembe aliruhusu ipigwe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
#sportskitaa #sportskitaa

TATHIMINI MCHEZO WA MBAO FC DHIDI YA YANGA.

NA MESHACK MELELE

Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara kati ya klabu ya Mbao Fc na Yanga umemalizika kwa klabu yenye maskani yake mitaa ya jangwani kuibuka kwa ushindi wa goli moja kwa sifuri, katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa ccm kirumba Mwanza.

MIWANI YANGU ILICHOKIONA KATIKA MCHEZO HUU

01 PLAY ONE SIDE KILL THE GAME ANOTHER SIDE
Yanga kwa kiasi kikubwa katika mchezo huu mpira umechezwa katika eneo alilokuwepo mchezaji mrisho ngassa ambaye alikua mwiba sana katika upande aliocheza.

Timu muda mwingi ilijitengeneza kupitia miguu yake, wakati mchezo ukiendelea Yanga walibadilika kimfumo kutoka kucheza mfumo wa 4-2-3-1 mpaka 4-2-2-2 huku Mapinduzi Balama alicheza ndani kidogo, hali iliyoufanya upande wake kutengeneza nafasi kwa Yanga kupiga krosi kupitia upande aliko Ngassa kuja upande huu.

Kipindi cha kwanza Kupitia Juma abdul alijaribu kutumia nafasi hiyo (space formed) lakini haikufanikiwa, mpaka kipindi cha pili Balama alivyotengeneza assist kupitia upande huu.

02 UCHEZAJI WA DAVID MOLINGA
David Molinga katika mchezo huu alikua target man, aliweza haswa kuileta timu katika mchezo, kupitia vision eye aliona gap liliotengenezwa na mabeki wa Mbao na viungo wao.

Kila alipoenda katika gap hilo alifanya beki ya kati ya mbao kumfuata na kutengeneza nafasi nyuma yake, nafasi ambayo haikutumika ipasavyo na viungo washambuliaji wa Yanga akiwemo Nahodha Papy TShishimbi.

03 MATUMIZI YA MIPIRA MIREFU BADO NI TATIZO
Yanga baada ya kuona eneo la kati limeminywa na wingi wa wachezaji wa mbao waliocheza flat 4-4-2, walijaribu kuivunja safu hiyo kwa kupiga long balls(mipira mirefu) Kupitia Ally Ally

Mipira iliyopigwa ilizuiwa na vichwa vya mabeki wa mbao, ni jambo lilitazamiwa kutokea Yanga walitakiwa kucheza na mipira iliyotokana baada ya vichwa kupigwa(second balls) ambayo haikupigwa kimakini na wachezaji wa mbao

04 MBAO WALICHEZA KUTOKANA NA YANGA ZAIDI
Baada ya Yanga muda mwingi kuziua winga zake na kuzifanya zicheze ndani zaidi na kuwa 4-2-2-2, mbao nao wakaua mawinga wao wa pembeni na kucheza ndani zaidi, mpira ukachezwa katikati, wakabaki wakitegemea Yanga wakosee kwa makosa ya kimfumo ndio wayatumie.

MATUMIZI YA MIPIRA ILIYOKUFA(SET PIECES)
Yanga katika mchezo huu wamefanikiwa kupata free kicks kadhaa baada ya kufanyiwa madhambi, mpigaji wa free kicks zote alikuwa Molinga ambaye kwa kipindi cha karibuni ameweza kumshawishi Kocha kupiga faulo nyingi ndani ya mchezo

Kiuhalisia Molinga ni mzuri kupiga faulo ambazo ziko mbali kidogo kama yard 35 kutoka golini, faulo za karibu anaonekana kutokuwa mzuri, Balinya anaweza kupiga vizuri faulo za karibu tuliona namna alivyofunga dhidi ya township.

MWISHO
Yanga walistahili ushindi kutokana na na namna walivyocheza ingawa bado ball controls zao pindi wanapoipokea mipira sio nzuri.
Tuwakatakie maandalizi mema katika mashindano ya shirikisho afrika dhidi ya Pyramid.

TFF LATOA TAMKO LINGINE

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia
Rais wake, Wallace Karia, limesema bado
mpaka sasa halijatangaza Kocha Mkuu wa
Taifa Stars.
Karia amesema kuwa watanzania
hawapaswi kuwa na haraka juu ya kocha
mpya bado kwani hawajamtangaza.
Kauli ya Karia imekuja mara baada ya
kuelezwa kuwa kuwa kocha Mrundi,
Etienne Ndayiragije ndiye atachukua rasmi
nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri akiwa
na kikosi cha Stars tangu akaimu nafasi
ya Emmanuel Amunike.
Karia amekanusha uwepo wa taarifa hizo
akisema wao hawajazitoa na akiwataka
watanzania wawe na subira.
“Sisi bado hatujamtangaza kocha wa
Stars, watanzania wanapaswa kuwa na
subira, kama Azam walisema ni wao na si
sisi, subirini.”

#LikePageNewsUpdates

Chelsea wanajiandaa kuwapa mikataba mipya wachezaji wao

Chelsea wanajiandaa kuwapa mikataba mipya wachezaji wao kinda Tammy Abraham na Fikayo Tomori walioanza vyema msimu huu.
.
Tomori na Abraham wanatazamiwa kupewa mikataba itakayowafanya kusalia Darajani hadi mwaka 2024!. Hadi sasa vijana wameshakubali kusaini mikataba hiyo kinachosubiriwa ni makubaliano ya mishahara tu kati ya Chelsea na Mawakala wa wachezaji hao!
.
.
Prepared by @anode360
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Chelsea wanajiandaa kuwapa mikataba mipya wachezaji wao

Chelsea wanajiandaa kuwapa mikataba mipya wachezaji wao kinda Tammy Abraham na Fikayo Tomori walioanza vyema msimu huu.
.
Tomori na Abraham wanatazamiwa kupewa mikataba itakayowafanya kusalia Darajani hadi mwaka 2024!. Hadi sasa vijana wameshakubali kusaini mikataba hiyo kinachosubiriwa ni makubaliano ya mishahara tu kati ya Chelsea na Mawakala wa wachezaji hao!
.
.
Prepared by @anode360
Powered by @mcheza_tz @bussi_ntua @tshombee1 #sokaonlineupdates

Design a site like this with WordPress.com
Get started