KOCHA MANCHESTER UNITED: FERNANDES BADO HAJAFIKIA KUWA RONALDO

OLE Gunnars Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa kiungo wake Bruno Fernandes hawezi kufananishwa na Cristiano Ronaldo kama wengi wanavyosema badala yake anacheza kama Paul Scholes.

Fernades amesajiliwa na Unted kwenye usajili wa mwezi Januari akitokea Klabu ya Lisbon kwa kitita cha pauni milioni 67.8 huku wengi wakimfananisha na Ronaldo.

“Ronaldo ni mchezaji wa tofauti na tunamamini kwamba Fernandes atakuwa na maisha mazuri ndani ya kikosi chetu na tutafanya naye mengi mazuri kwa ajili ya timu.

“Huyu ni mchezaji mzuri kwa kufunga lakini pia anaweza kutoa pasi za mabao kumfananisha na Ronaldo bado hajafikia hatua hiyo,” amesema.

Visit website

YANGA WAFICHUA SIRI YA KUITWANGA LIPULI TAIFA

NAHODHA wa timu ya Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa walipewa mbinu na Kocha Mkuu Luc Eymael za kuwabana Lipuli jambo lililowapa ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Tshimbi amesema kuwa Eymael aliwaambia kwamba wanacheza na timu bora ni lazima wapambane kupata matokeo mapema jambo lililowapa nguvu ya kujiamini.“Kocha alituambia kwamba tunacheza na timu bora na ngumu ni lazima tupambane kupata matokeo mapema jambo ambalo lilitupa matokeo haraka.“Kipindi cha pili tulizidiwa mbinu ila tulilinda matokeo na tumefurahi kuondoka na pointi tatu muhimu,”.Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 34 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 17.Mabao ya Yanga yalifungwa na Mapinduzi Balama na Cernard Morrison wote walimaliza pasi za Juma Abdul huku lilel la Lipuli likifungwa na David Mwasa.

Visit website

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania yatoa maamuzi kulingana na mwenedo wa ligi kuu

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Februari 03, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
.
.

Mechi namba 157: Azam FC 1 v Mtibwa FC 1-Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi iliyochezwa Januari 30,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
.
.

Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya Makamishina kwa kosa la kutoa taarifa yenye mapungufu.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina
.
.

Mechi namba 150: Simba SC 3 v Namungo FC 2-Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Safisha amefungiwa miaka mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea katika mechi hiyo Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1)(a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
.
.

Mechi namba 75A :Friend Rangers(0) vs Dodoma FC(1)-Kiongozi wa Klabu ya Friends Rangers Heri Chibakasa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kupigana na washabiki wa timu pinzani
.
.

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1) kuhusu Udhibiti wa Waamuzi katika mechi iliyochezwa Februari 01,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.
.
.

Mechi namba 29A:Dar City Fc (1) vs African Sports(0)- Mwamuzi Salum Mkole amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kuonyesha udhaifu katika usahihi wa kutoa kadi katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 31,2020 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

TAREHE YA MWISHO YA USAJILI EPL YARUDISHWA ⁣SEPTEMBA 1.

Vilabu vya Ligi Kuu Uingereza vilikutana kupiga kura kupitisha mabadiliko kwa tarehe ya kufunga usajili kwa msimu wa 2020/21.⁣

Hii itahamisha tarehe ya mwisho kurudi Septemba 1 kama ilivyokua zamani.⁣

Tarehe ya kufunga usajili majira ya joto 2020 itakua mnamo Septemba 1 au usiku wa tarehe 31 Agosti 2020.⁣

Vilabu vilikubaliana hayo baada ya kujadili mada hiyo kwa muda mrefu kwenye Mikutano ya Wanahisa wa zamani.

Kikosi chetu bora cha hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika

Kikosi chetu bora cha hatua ya makundi klabu bingwa barani Afrika

1• Denis Onyango – Mamelod Sundowns

2• Athar El Tahir – Al Hilal

3• Motjeka Madisha – Mamelod Sundowns

4• Abdelkader Bedrane – Esperance

5• Ernest Luzolo Sita – As Vita

6• Andile Jali – Mamelod Sundowns

7• Glody Likonza – Tp Mazembe

8• Mohamed Afsha – Al Ahly

9• Abdelraouf Benguit – Esperance

10• Gaston Sirino – Mamelod Sundowns

11• Jackson Muleka – Tp Mazembe

Mfumo ni 4-4-2

Kocha wetu mkuu ni Pitso Mosimane wa Mamelod Sundowns

Kocha msaizi ni Mihayo Kazembe wa Tp Mazembe

Uwanja wetu ni Stade de Tp Mazembe Lubumbashi Congo

Bosi wetu ni Patrice Moripe wa Mamelod Sundowns😅

@anode360 | @stevenjema_268
| @joamap | @nazareth.j.upete | @khalidchukuchuku93 | @michezo_halisi | @kombeladunia_ | @90sportsplus | @shadrack_janga @danirito_thomson | @victor_simon81 | @frankvegullah | @rajuunially | @fullsokatz | @official_abdallah8 @kimbosmith_

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Kaizer Chiefs wamethibitisha kuwa kwenye mazungumo na mlinzi wao Daniel Cardoso

Kaizer Chiefs wamethibitisha kuwa kwenye mazungumo na mlinzi wao Daniel Cardoso juu ya kumuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo

Cardoso mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Chiefs mwaka 2015 akitokea Free State United ambapo mpaka sasa ameichezea michezo 80 na kufanikiwa kuifungia goli 5

Cardoso ni mzawa wa Afrika Kusini na kwa nyakati tofauti aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Afrika Kusini

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Mhango kuwakosa waajili wake wa zamani kwenye hatua ya 32 bora ya michuano ya Ned Bank Cup 2020 •

Kocha mkuu wa klabu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini Josef Zinnbaeur amethibitisha kuwa mshambuliaji wake Gabadinho Mhango ataukosa mchezo ujao wa hatua ya 32 bora wa michuano ya Ned Bank Cup dhidi ya Bidvest Wits kutokana na kuwa na kadi 3 za njano

Muhango ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Malawi alisajiliwa na Orlando akitokea Bidvest Wits ambayo watakutana nayo kwenye mchezo wa mtoano wa michuano huyo siku chache zijazo

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

Robo fainali ya kibabe klabu bingwa barani Afrika • Al Ahly Vs Mamelod Sundowns

Robo fainali ya kibabe klabu bingwa barani Afrika

Al Ahly Vs Mamelod Sundowns

Mwaka jana walikutana kwenye hatua kama hii na Al Ahly waliondoshwa kwa jumla ya goli 5-2

Mchezo wa kwanza Ahly wakiwa ugenini walikubali kupoteza kwa goli 5-0 na baadae wakashinda 2-0 Cairo nchini Misri

Safari hii National Al Ahly wataanzia nyumbani na wiki moja baadae watasafiri kuelekea Afrika Kusini kwaajili ya mchezo mmoja marudiano

Powered by @sports_lady_tz
#dailysporttz

5/2/1992 MWENYEZI ALITUZAWADIA NEYMAR DA SILVA SANTOS Jr. .

Miaka 28 iliyopita, manispaa ya Mogi das Cruzes, Sao Paulo, Brazil alizaliwa fundi Neymar Jr.
.
Kwa upande wangu moja kati ya wachezaji wachache katika kizazi hiki aliepewa kipaji cha hali ya juu sanaaa
.
Ingekuwa kwenye Economics, tungesema “if other factors remain costant” basi Neymar ndie anafuata baada ya Ronaldo na Messi
.
Ni kawaida viumbe vilivyobarikiwa hupitia majaribu, Neymar Jr ameishi maisha magumu sana, akitoka familia duni isiyo hata na uwezo wa kuweka umeme nyumbani japo inakaa mjini
.
Ila ni familia yenye utajiri wa upendo kati yao na utajiri wa imani ya dini, kwenye kila jambo waliamini katika “100% Jesus”
.
Neymar Jr amebarikiwa sana ball control, skills, pace, ila pia football brain
.
Skills zmetokana na kucheza soka liitwalo FUTSAL katika sakafu ya viwanja vya Basketball, ni soka lililojaa udambwi mwingi, huna udambwi basi ishia kuwa mshabiki, likitumia mpira usiodunda sana, hii ilimjenga sana
.
Akiwa na miaka 10 tayari ndie King of Streets, waBrazil walimpenda kuliko Zizou kwenye runinga, ile €57m. aliyonunuliwa kwenda Barca waliona kama ni ndogo sana
.
Wazazi wake walimpa sapoti kubwa sana katika soka, kila kabla ya mechi wazazi wake walimpa busu mmoja kulia mwingine kushoto, yeye busu alirudisha kwa burudani yake uwanjani
.
Comeback ya Barca vs PSG, perfomance bora kabisa ya Neymar, dakika ya 62 baada ya Cavani kuifungia PSG wachezaji wote walikata tamaa
.
Ila Neymar aliuona uwanja mdogo kama ule Basketball uliompa sukari ya na ladha katika mguu wake
.
Alikimbia kila eneo la uwanja, alipiga kila kona, free kick na kurushiwa kila mpira, dakika ya 88 anafunga bonge la freekick, inaleta tumaini
.
Ile assist ya goli la 6 na la ushindi ni nadra sana, ile chop pass katika mazingira yale na kipindi timu inataka ushindi ukikosea utaitwa bishoo, ila kwake ile ni natural tu si ubisho.
.
Dakika 35 tu za ubora kutoka kwa Neymar baada ya goli la Cavani zilitengeneza historia, wachezaji walimbeba na kumrusha na kumuona mkombozi, huyu ndie Neymar Jr akiwa fit na seriuos. Binafsi naamini ile ni 70% tu ya uwezo wake
.
Happy Birthday Neymar Jr
.
Imeandikwa na @danirito_thomson

Design a site like this with WordPress.com
Get started