MKUDE CHAMA KUKATWA MPUNGA SIMBA

✍na saboso Gin jr
Baada ya kutuhumiwa kuwa walikuwa na makosa ya kinidhanu, inaelezwa wachezaji Gadiel Michael, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Clatous Chama walifikishwa kwenye kamati ya nidhamu.

Taaifa zimeeleza kuwa CEO mpya wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza, amesema tayari walikutana na wachezaji hao na tayari wameshamaliza.

Bosi huyo amefunguka kuwa kuna mambo hayakuwa sawa na upande wao kama uongozi waliamua kukaa nao kikao kwa ajili ya kuyamaliza.

Hata hivyo, taarifa imesema kuwa Mazingiza ameeleza wachezaji hao wanne wataendelea na kazi kama kawaida lakini kuna adhabu ambazo watapewa huku wakiendelea na kazi.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema uwezekano wa kukata baadhi ya fedha zao unaweza ukafanyika.
#sportskitaa

ALICHOSEMA KOCHA ZAHERA KUHUSU MECHI DHIDI YA PYRAMIDS KESHO

Kocha mkuu wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema maandalizi yote yamekamilika kuelekea mchezo wa kesho wa mchujo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Zahera amesema wachezaji wake wapo kwenye hali nzuri na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa nyumbani ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano.

Raia huyo wa DR Congo ameongeza kuwa anaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao lakini wamejiandaa vizuri kuwakabili na hatimaye kupata matokeo. “Wachezaji wangu wako tayari kwa mchezo wa kesho, tunaamini utakuwa mgumu kwakua Pyramids ni wazuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi nyumbani,” alisema Zahera.

@yangasc @pyramidsfc @tanfootball @caf_online

#wapendasokaupdates
#CAFCC

Kocha Mkuu mpya wa Azam FC kukaa benchi..kuanzia kesho

#Repost @azamfcofficial
Kocha Mkuu mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, anatarajiwa kukaa benchi kuanzia mechi yetu ya kesho Jumapili dhidi ya Ruvu Shooting
:
Mtaalamu huyo wa ufundi kutoka nchini Romania mwenye leseni ya juu ya ukocha (UEFA Pro Licence), alishindwa kukaa benchini kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba kufuatia vibali vyake vya kufanyia kazi kutokamilika.

Kevin De Bruyne aendeleza kukiwasha manchester city

πŸ”΅ Kevin De Bruyne Sasa kahusika katika Magoli 1️⃣1️⃣ katika mechi 8️⃣ tu alizoanza ndani ya Premier League msimu huu, Idadi Kubwa kuliko Mchezaji Mwingine yeyote ndani ya Ligi..
πŸ…°οΈ v West Ham
πŸ…°οΈπŸ…°οΈ v Tottenham
πŸ…°οΈ v Bournemouth
βš½πŸ…°οΈ v Brighton
βš½πŸ…°οΈπŸ…°οΈ v Watford
πŸ…°οΈ v Everton
❌ v C. Palace
⚽ v Aston Villa

13 – Raheem Sterling kafunga Magoli 13 katika mechi zake 14 za Mashindano yote msimu huu, Idadi Kubwa kuliko Mchezaji mwingine yeyote kutoka Ligi Kuu Uingereza msimu huu 2019-20..
#PremierLeague #ManchesterCity

Messi afunga misimu 15 mfululizo ligi.ya mabingwa ulaya

Juzi Lionel Messi alikua mchezaji wa kwanza kufunga katika misimu 15 ya Ligi ya mabingwa mfululizo wakati Barcelona ikipata ushindi mwembamba huko Slavia Prague.

Nahodha Messi aliipa Barca ushindi wa mapema baada ya kupata pasi kutoka kwa kiungo Arthur.

Barcelona ambao wako juu kwenye ligi ya La Liga, kwa sasa wameshinda mechi sita mfululizo kwenye michuano yote.

Matokeo hayo yanafanya kikosi cha Ernesto Valverde kuwa kinara kwenye kundi F ikiwa na alama saba kutoka kwenye michezo mitatu, alama tatu juu ya Inter Milan na Borussia Dortmund.

Wapinzani yanga watua na ndege binafsi

Wachezaji wa Pyramids Fc waliwasili jana jioni jijini Mwanza kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga ambao utapigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Timu hiyo imetua Mwanza kwa usafiri wa ndege binafsi

Pyramids iliwatanguliza baadhi ya maafisa wake ambao wamekuwepo Mwanza kwa takribani siku tatu

Timu hiyo kuja nchini na ndege binafsi sio jambo la kushangaza, kwani ni timu yenye ‘ukwasi’

Jumapili watakuwa na kazi dimba la CCM Kirumba dhidi ya Yanga ambayo imedhamiria kuondoka na alama zote tatu kwenye mchezo huo

Design a site like this with WordPress.com
Get started