Rekodi ya pytamids wakiwa ugenini

Pyramids.. Pyramids.. Pyramids! Wakiwa ugenini kule Congo Brazzaville, walipata bao kipindi cha kwanza. Mechi ikaisha 1-0. Wakashinda.

Wakiwa ugenini kule Algeria walipata bao dakika ya 11 kipindi cha pili. Mechi ikaisha 1-0. Wakashinda.

Kwa picha ya haraka haraka, kwa game hizo 2 zilizopita, hawa jamaa wana uwezo wa kutumia presha ya wenyeji kufunga mabao ya haraka, then ni wagumu kwenye safu yao ya ulinzi.

Nimetazama mechi zao 3 za Ligi.. Wanapenda kufunga mabao kipindi cha kwanza. Nini Yanga wafanye? Kuchunga sana presha yao ya uhitaji wa matokeo kwa pupa.

Wale Waalgeria walifungwa kwa krosi kutoka wingi ya kushoto. Wale Congo walifungwa kwa krosi kutoka wingi ya Kulia.

Unaona walivyo hatari kupitia pembeni. Wana uwezo wa kumiliki mpira lakini hutoka kwa kasi sana wanapovuka mstari wa kati

Ni mechi ambayo JUMA ABDUL na SONSO wanatakiwa kuwa katika viwango vyao bora zaidi.

Ni mechi ambayo ALLY ALLY anatakiwa kua bora sana kwenye mipira ya hewani.

Makame. Anahitahi kutuliza presha yake. Waarabu wanaweza kumtoa mchezoni kwa kutumia madhaifu yake ya kukosa utulivu

FeiToto, kama atapangwa, hii ni mechi ambayo anatakiwa kurejesha ubora wake kwa asilimia 100. Ile tabu aliyompa Makame kwa Zesco isiwepo leo.

Tshishimbi🙌 Game inafanana na yeye. Ana uwezo wa kuiamua hii mechi kama atacheza kwa utulivu mkubwa. Asiruhusu waarabu watulie na mpira katika eneo lao. Aongoze pressing.

Balama🙌 Yes.. Hii ni game yake ya kufunga na sio kuasist. Yeye pekee ndie atakaekua mchezaji huru eneo la mbele. Atumie faida ya nguvu/mikimbio ya Sadney kwenye kujitengenezea nafasi.

Sioni Sibomana akianza leo. Bado hajawa na ufiti wa asilimia 100. Mrisho Ngassa, kama atapewa game, basi akumbushwe mbali na kushambulia, jukumu lake la msingi leo ni kushuka kumsaidia Sonso.

Mechi ni ngumu sana kwa Yanga na Pyramids. Tension ni kubwa mno! Wasiwasi wangu uko kwa mabeki wa pembeni wa Yanga lakini Tshishimbi na Balama, kama watamka fresh, kimbinu hii ni game yao kuwabeba Wananchi.

Kila la kheri Yanga🙏
#kwako_mwalim_kashasha

Senzo aungana na simba Arusha

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingiza amejiwekea utaratibu wa kuungana na timu popote inapokwenda kucheza

Mazingiza atakuwepo uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuishuhudia timu yake ikichuana na Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu

Amefanya hivyo tangu alipoanza majukumu yake katika klabu ya Simba, hakika amekuwa chachu ya ushindi kila mara anapokuwa dimbani

Simba kukabiliwa na changamoto ya uwanja Sheikh Amri Abeid

Singida United na Simba zinakutana leo kwenye mchezo wa ligi kuu unaopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha

Hata hivyo mchezo huo unafanyika baada ya kufanyika kwa Tamasha la Fiesta katika uwanja huo

Lakini pia, uwanja wa Sheikh Amri Abeid ni moja ya viwanja ambavyo sehemu yake ya kuchezea ‘pitch’ sio nzuri

Jana Simba ilishindwa kufanya mazoezi yake ya mwisho uwanjani hapo kutokana na kuwepo kwa majukwaa

Hata hivyo Simba imekuwa ikijiandaa kucheza katika viwanja vya aina zote na kuweza kupata ushindi

Mchezo waliocheza dhidi ya Mashujaa FC kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma ni mfano wa mazingira ambayo Simba inaweza kukabiliana nayo

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wamepania kuendeleza wimbi la ushindi dhidi ya Singida United

Yanga kuisambaratisha pyramids ..CCM kirumba leo

Leo ni siku muhimu kwa mashabiki wa soka nchini hususani mashabiki wa Yanga ambao timu yao saa 10 jioni itashuka uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Pyramids Fc kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho

Yanga, mabingwa wa kihistoria Tanzania wana dakika 180 kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho kwa mara ya tatu

Lakini pia mafanikio yao ni faida kwa Tanzania kwani wataiongezea nchi pointi huko CAF na pengine Tanzania kuendelea kuwa na timu nne kwenye michuano ya mwakani

Matokeo ya ushindi leo yanaweza kuwa hatua nzuri kuelekea makundi ingawa bado watakuwa na kazi ya kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano ambao utapigwa wiki ijayo nchini Misri

Yanga imejifua takribani wiki nzima kujiandaa na mchezo huo, leo ndio siku ya kumaliza kazi pale CCM Kirumba

Ari na morali ya wachezaji iko juu, hali iko hivyo kwa mashabiki ambao siku ya jana mji wa Mwanza gumzo kubwa lilikuwa mchezo huo

Hakuna shaka mashabiki wengi watajitokeza CCM Kirumba kuiunga mkono timu yao, wale waliombali wataushuhudia mchezo huo kwenye runinga

Pamoja na yote yanayozungumzwa kuhusu klabu ya Pyramids Fc, hakuna lisilowezekana kwenye soka, muhimu zaidi Yanga itakuwa nyumbani

Faida ya uwanja wa nyumbani pamoja na uzoefu wa michuano hiyo ni silaha muhimu kwa Yanga leo

matokeo ya Soka Jana

Kamata matokeo ya Soka Jana
:
#VodacomPrimierLeague
FT Mtibwa Sugar 2-0 Polisi Tanzania
:
#EnglandPremierLeague
FT Manchester City 3 – 0 Aston Villa
FT Brighton & Hove Albion 3 – 2 Everton
FT Watford 0 – 0 AFC Bournemouth
FT West Ham United 1 – 1 Sheffield United
FT Burnley 2 – 4 Chelsea
:
#EnglandChampionship @sokaplace_
FT Sheffield Wednesday 0 – 0 Leeds United
FT Birmingham City 2 – 1 Luton Town
FT Huddersfield Town 2 – 1 Barnsley
FT Hull City 2 – 0 Derby County
FT Middlesbrough 0 – 0 Fulham
FT Millwall 2 – 0 Stoke City
:
#SpainLaLigaSantander
FT Leganes 1 – 0 Mallorca
FT Real Valladolid 2 – 0 Eibar
FT Atletico Madrid 2 – 0 Athletic Bilbao
:
#ItalySerieA
FT Lecce 1 – 1 Juventus
FT Inter 2 – 2 Parma
FT Genoa 3 – 1 Brescia
:
#GermanyBundesliga
FT FC Bayern München 2 – 1 FC Union Berlin
FT Schalke 04 0 – 0 Borussia Dortmund
FT Hertha BSC 2 – 3 Hoffenheim
FT Freiburg 2 – 1 RasenBallsport Leipzig
FT SC Paderborn 07 2 – 0 Fortuna Düsseldorf
FT Bayer Leverkusen 2 – 2 Werder Bremen
:
#FranceLigue1
FT Lille 3 – 0 Bordeaux
FT Montpellier 0 – 0 Angers
FT Lyon 2 – 0 Metz
FT Strasbourg 1 – 0 Nice
FT Brest 2 – 0 Dijon
FT Reims 0 – 0 Nimes
France – Ligue 2 October 26
FT Lorient 0 – 1 Troyes
:
#NetherlandsEredivisie
FT Willem II 2 – 1 RKC Waalwijk
FT Fortuna Sittard 4 – 1 VVV-Venlo
FT Vitesse 0 – 2 ADO Den Haag
FT Heracles 4 – 0 PEC Zwolle
:
#BelgiumFirstDivisionA
FT Sporting Charleroi 1 – 0 Royal Excel Mouscron
FT Royal Antwerp 3 – 1 Kortrijk
FT Zulte Waregem 2 – 0 Oostende
FT Genk 1 – 0 Cercle Brugge
:
#SouthAfricaPremierLeague
FT Lamontville Golden Arrows 2 – 1 Polokwane City
FT Stellenbosch FC 1 – 0 Orlando Pirates
FT Highlands Park FC 2 – 0 Chippa United FC
:
#LigiKuuWanawakeTanzania
FT Alliance Girls 3 – 0 Kigoma Sisterz
FT Simba Queens 2 – 2 Ruvuma Queens
FT Baobab Queens 1 – 5 JKT Queens
FT Mlandizi Queens 4 – 1 Panama Girls
FT TSC Queens 2 – 1 Marsh Queens
FT Tanzanite 0 – 3 Yanga Princess
:
#TanzaniaFdl
FT Mbeya Kwanza 0-1 Ihefu
FT Iringa United 0-0 Boma Fc
FT African Lyon 2-0 Dodoma Jiji
FT Maji Maji 0-0 Friends Rangers
FT Rhino Rangers 0-0 Transit Camp
FT Geita Gold 1-1 Arusha Fc
:
Imeandaliwa na @officialchristz wa @sokaplace_

Sheffield Utd: yatia mgomo.kufungwa ugenini

📊 Sheffield Utd:
🔴Inakuwa bado ni timu 1️⃣ kati ya 2️⃣ ambazo bado hazijafungwa uwanja wa Ugenini Msimu huu wa Premier League (Sambamba na Liverpool) – Rekodi ya Sheffield Ugenini W1 D4 L0
🔴 Wanaifikia Rekodi yao ya mfululizo wa mechi nyingi zaidi Ugenini bila Kupoteza katika historia yao ya Premier league – Mwaka 1994 Wakicheza game Tano bila Kupoteza.
🔴 Inakuwa timu ya kwanza katika ya Premier league Kutofungwa mechi tano za Ugenini katika Mwanzo wa msimu Tangu Hull City msimu wa 2008/2009.
….
FT: Brighton 3-2 Everton
FT: Watford 0-0 Bournemouth
FT: West Ham 1-1 Sheffield United
#PremierLeague #PLUpdates #SokaPlaceUpdates

Zahera akanusha kuwapa wachezaji miliono 100

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekanusha mbele ya waandishi wa habari leo kuwa yeye atawapa Milioni 100 wachezaji wa Yanga kama watashinda.

Kocha Zahera amesema kuwa yeye hakuahidi kuwa atawapa zawadi wachezaji wa Yanga Kama watashinda isipokuwa akibeti na atakapata ndipo atawapa kama wakishinda.

“Boo Mimi sikusema nitawapa pesa Milioni 100, jo nilisema kuwa Kama Mimi iko nabeti kwa Mfano mu sportpesa napata ntawapa Kama na wao wameshinda” alisema Kocha Zahera.

Taarifa iliyosambaa Jana kwenye mitandao ya kijamii ikinukuu taarifa iliyosikika Radio East Africa kuwa Kocha Zahera amesema atawapa Milioni 100 wachezaji wa Yanga wakishinda mechi dhidi ya Pyramids.

Kesho Jumapili Octoba 27 Mwaka huu timu ya Yanga SC wanacheza mechi ya Mashindano ya Caf Confederation dhidi ya Pyramids kutoka Misri, mchezo ukichezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Design a site like this with WordPress.com
Get started